Jumanne, 6 Februari 2018

MAANDALIZI YA DOUBLE A F.C KUELEKEA LIGI YA WILAYA SITA BORA

TAREHE 05/02/2018 DOUBLE A F.C WALICHEZA NA LUMBILA F.C NA DOUBLE A KUIBUKA NA USHINDI WA GOLI 1-0 GOLI LILILOFUNGWA NA JUSTINE WANYAKA








Alhamisi, 9 Februari 2017

KAMA HUKUBAHATIKA KUMWONA MWANAFUNZI ALIYEKAMATWA NA MADWA YA KULEVYA MBEYA-HUYU HAPA


SAKATA LA UNGA NCHINI LAINGIA WIKI YA PILI SASA

Yusuf Manji kawasili Polisi Leo badala ya Kesho Kuitikia Wito wa Makonda

Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha Polisi cha Kati leo saa 4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi.

Manji amefika leo badala ya kesho ambapo yeye na wengine 64 walitakiwa kufika kituoni hapo.

Manji ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na waandishi wa habari na kusema hatoweza kufika kituoni hapo siku ya Ijumaa.

Amewasili leo na gari aina ya Range Rover rangi nyeusi huku.

Manji amefika kituoni hapo  akiwa na wanasheria wake 8 ambapo wanasheria 6 ni raia wa Tanzania na wanasheria wawili ni raia wa Uingereza. Aidha, mashabiki wa Yanga wamejitokeza kwa wingi kituoni hapo kumuunga mkono kiongozi wao.

Mbali na Manji, wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Pamoja na Fremaan Mbowe, Askofu Josephat Gwajima, Iddi Azan. 

Endelea kufuatilia habari motomoto

Jumamosi, 29 Oktoba 2016

FUATILIA MATOKEO YA LIGI KUU ULAYA MAARUFU KAMA EPL HAPA

Arsenal

Klabu ya Arsenal imekwea hadi nafasi ya kwanza kwenye ligi ya England baada ya kupata ushindi wa mechi yake ya saba kwa kuilaza Sunderland 4-1 ugani Light.
Alexis aliipa gunners bao la uongozi katika dakika ya 19 baada ya kuandaliwa pasi na Alex Oxlade Chamberlain.
Hata hivyo uongozi huo ulidumu hadi dakika ya 65 baada ya Defoe kuipa Sunderland bao la kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti.
Petr Cech alimtega mshambulizi Duncan Watmore na kupewa kadi ya njano.
Dakika chache baadaye, Wenger alifanya mabadiliko uliomwezesha Giroud kuchukua nafasi ya Alex Iwobi aliyeonekana kuwa na kazi ngumu dhidi ya mabeki wa Sunderland.
Arsenal alichukua uongozi kunako dakika ya 71 baada ya nguvu mpya Oliver Giroud kuunganisha pasi ya beki Kieran Gibbs,kwenye wavu. Gibbs alichukua nafasi ya Nacho Monreal anayeuguza majeraha.
Sunderland
Ushambulizi wa Sunderland ulitishia uongozi wa Arsenal, lakini Giroud aliipa Arsenal matumaini ya kuondoka na alama tatu katika dakika ya 76 baada ya kufunga kupitia krosi ya Kona iliyiochanjwa na kiungo Mesut Ozil.
Dakika mbili baadaye Alexis Sanchez alizidisha uchungu kwa mashabiki wa Sunderland walioonekana kuondoka uwanjani kwa kupachika bao la nne. Sanchez alimtesa kipa Jordan Pickford baada ya Ramsey kumuandalia pasi. Bahati ya beki Kieran Gibbs haikutimia baada ya mkwaju wake kugonga lango, lakini Sanchez alifunga kazi na kuihakikishia Arsenal ushini huo muhimu.
Arsenal inaongoza ligi ikiwa na alama 23 ingawa klabu za Machester City na Liverpool bado hazicheza.
Ushindi huo umeipa Arsenal motisha huku ikisubiri kuialika Tottenham Hotspurs uwanjani Arsenal wikendi ijayo.