Jumamosi, 31 Agosti 2013

IGP Mwema ameibiwa upanga wa dhahabu wa kilo tatu




Jeshi la Polisi limeingia katika kashfa nzito baada ya mkuu wake, Inspekta Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga wa dhahabu ambao ni mali ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO).

Upanga huo wenye uzito wa takriban kilo tatu na wenye thamani ya zaidi ya fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni kielelezo kwa nchi inayokabidhiwa uongozi wa SARPCCO.

Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa SARPCCO, ambapo upanga huo ulikabidhiwa kwa IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo.

Hilo ni tukio la pili la wizi la mali zinazohusu ofisi ya IGP, ambapo mwaka jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa kompyuta ndogo (laptop), ikiwa na taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa hakuna taarifa za kupatikana kwa kompyuta hiyo.

IGP Mwema alikabidhiwa upanga huo Septemba 5, 2012, katika mkutano saba wa SARPCCO uliofanyika Zanzibar na kuhudhuriwa na wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi 13, pamoja na mashirika ya kimataifa.

Upanga huo ambao unakwenda sambamba na bendera ya SARPCCO, ni moja ya vielelezo vya nchi iliyochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa shirikisho hilo, ambaye moja kwa moja anakuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi katika nchi husika.

Kwa mujibu wa taratibu za SARPCCO, vielelezo hivyo hutakiwa kuwekwa ofisini kwa kiongozi husika, ikiwa ni alama ya kila mgeni atakayeingia ofisini hapo kutambua uwepo wa wadhifa huo wa kimataifa.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa IGP aligundua kutoweka kwa upanga huo wiki iliyopita, wakati akijiandaa kwenda kuukabidhi kwa mwenyekiti mpya wa SARPCCO, ambaye ni IGP wa Namibia.

Taarifa za ndani ya jeshi hilo zilibaini kuwa, IGP alilazimika kuondoka bila upanga huo alipokwenda Namibia wiki iliyopita kuhudhuria mkutano wa nane wa SARPCCO, uliofanyika Jumapili iliyopita mjini Windhoek.

Kwa mujibu wa uchunguzi, IGP Mwema alikabidhi upanga unaofanana na huo ambao siyo wa dhahabu, alioazimwa kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia, Inspekta Jenerali, Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga, na kukabidhiwa kama ishara ya kukabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Uchunguzi ulibaini kuwa IGP Mwema alitoa ahadi ya kurejesha upanga halisi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, au Serikali ya Tanzania italazimika kutengeneza mwingine kulipa uliopotea.

Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha kuwa kashfa hiyo ametupiwa Mkuu wa Polisi Zanzibar, Kamishna Mussa Ali Mussa pamoja na dereva wake, ikidaiwa kuwa upanga huo baada ya kupokewa na IGP Mwema, Septemba mwaka jana uliwekwa kwenye gari la kamishna huyo.

Kichwa cha binadamu chapatikana katika ofisi ya mkuu wa polisi

Polisi nchini Kenya
Polisi nchini Kenya wanachunguza kisa ambacho kichwa cha mtu aliyeuawa kilipatikana kimewekwa nje ya afisi ya mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya polisi Johnston Kavuludi jijini Nairobi.
Kifurushi hichi kilichokuwa kimefungwa kwa karatasi ya plastiki, vilevile kilikuwa na mikono miwli ya binadamy iliyojaa damu.
kando ya kifurishi hicho kulikuwa na ilaani iliyoandiskwa ''Kavuludi wewe ndiye utakayefuata''.
Tangu uteuzi wake, kamishna huyo ameongoza harakati za kujaribu kuifanyia marekebisho idara ya polisi ambayo inadaiwa kuwa fisadi zaidi Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa idara ya polisi, hakuna mshukiwa aliyekamatwa kauhusiana na tukio hilo na kuwa bado wangali wanachunguza mwili huo ulikuwa wa nani.
Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na uhasama kati ya tume hiyo inayoongozwa na Kavuludi na ofisi ya mkuu wa polisi, huku zikilumbana kuhusu nani ana madaraka ya kuliendesha idara hiyo.

Chanzo na BBC Swahili

Chelsea yashindwa kutamba mbele ya Bayern URFA Super CUP



Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye mechi ya jana...Ndani ya Dak 90 timu hizo zilikuwa (2-2)

Wachezaji wa Bayern wakifurahia ushindi wao baada ya kuiondosha Chelsea kwa Penalty (5-4) baada ya Rumelo Lukaku kukosa Penalty ya mwisho

Ijumaa, 30 Agosti 2013

Maandamano kufanyika Misri licha ya kitisho cha serikali

Matukio ya Kisiasa

Maandamano kufanyika Misri licha ya kitisho cha serikali

Chama cha Udugu wa Kiislamu kimepanga kuandamana baada ya sala ya Ijumaa dhidi ya serikali ya mpito nchini humo. Maandamano hayo yameitishwa licha ya serikali kutishia kutumia nguvu kupambana na waandamanaji.
Maandamano haya ya leo yanatarajiwa kupima ni kwa kiwango gani vikosi vya usalama vimelidhoofisha kundi hilo na hii itajulikana tu kwa namna watu watakavyojitokeza katika maandamano hayo.
Kulingana na wakaazi huko, maandamano ya leo yanahofiwa kuzua machafuko zaidi katika nchi hiyo iliyokumbwa na msukosuko wa kisiasa.
Maandamano Misri Maandamano Misri
Umwagikaji mkubwa wa damu ulishuhudiwa wiki mbili zilizopita baada ya polisi kushambulia kambi za waandamanaji waliokuwa wanapinga hatua iliyochukuliwa Julai 3 ya kumuondoa madarakani kiongozi wao Mohammed Mursi kwa njia ya mapindzi ya kijeshi.
Hali hiyo ilisababisha vurugu ya wiki nzima zilizowauwa watu takriban 1,000, wengi wao wakiwa wafuasi wa Mursi. Inadaiwa kuwa baadhi ya wafuasi hao walijibu mashambulizi kwa kuchoma makanisa, majengo ya serikali na pia kushambulia vituo vya polisi.
Pande zote mbili zaombwa kusuluhisha tofauti zao
Katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press, kiongozi wa kundi lililokuwa la waasi la Gamaa Islamiya, Abboud el-Zommor, alizihimiza pande zote mbili serikali na upinzani kukaa pamoja na kutatua tofauti zao ili kusimamisha umwagikaji wa damu nchini humo.
Huku hayo yakiarifiwa serikali imeongeza majeshi yake katika maeneo tofauti nchini humo huku ikilishutumu kundi la Udugu wa Kiislamu kuitisha maandamano na kuzua ghasia.
Kiongozi wa Udugu wa Kiislamu Mohamed El-Beltagi Kiongozi wa Udugu wa Kiislamu Mohamed El-Beltagi
Wakati huo huo utawala wa Misri umeendelea kuwakamata viongozi wa kundi hilo kwa madai ya kuchochea ghasia. Tayari viongozi wawili, Mohammed el-Beltagy na Khaled el-Azhari, walikamatwa hapo jana.
Polisi wanasema waliwakamata kwa sababu ya kuchochea maandamano na kuteswa kwa polisi aliyekamatwa na waandamanaji mjini Cairo.
Kwa upande wake. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imesema itapambana vikali na watu ambao wanajaribu kuyumbisha usalama wa nchi na kwamba polisi wamepewa amri ya kutumia nguvu katika kulinda mali ya umma na ile ya watu binafsi nchini humo.
Wizara hiyo imesema pia kuwa maandamano ya leo yana lengo la kusababisha vurugu.
Mwandishi: Amina Abubakar/Reuters/AP
Mhariri: Mohammed Khelef

DIAMOND AFANYA MAKUBWA KATIKA UZINDUZI WA VIDEO YAKE, AMKABIDHI GARI MUHIDIN GURUMO

1 1Mwanamuziki Diamond Platnum akimkabidhi funguo ya gari aina ya Toyota Funcargo mwanamuziki mkongwe nchini mzee Muhidin Gurumo kama zawadi yake kwa mkongwe huyo wa muziki baada ya kustaafu rasmi kuimba muziki, Diamond alitoa zawadi hiyo kwa Gurumo katika hafla yake ya uzinduzi wa video yake mpya ya wimbo Nomber One aliyoirekodi huko Afrika Kusini ikigharimu kiasi cha dola elfu 30.000 zaidi ya milioni arobaini za Tanzania, Video hiyo imetengenezwa kwa viwango vya kimataifa na itaweza kumtangaza vyema kijana huyo wa kitanzania katika ulimwengu wa muziki hasa kimataifa, Hafla hiyo imefanyika kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam na imehudhuriwa na wasanii pamoja na waigizaji wa filamu na watu maarufu mbalimbali
Mzee  Muhidin Gurumo akimshukuru Diamond kwa kumzawadia gari jambo ambalo kwake ni kama ndoto kwakuwa amestaafu akiwa hana usafiri “Yaani sijui hata mke wangu nikimwambia atanielewaje manake ni jambo la kushangaza kwangu” Alisema mzee Gurumo 3Diamond akimuongoza mzee Gurumo kwenda kumuonyesha gari 5Diamond akimuonyesha Mzee Gurumo gari 6Akimuelekeza jambo baada ya mzee Gurumo kuingia kwenye gari 7 
Diamond akizungumza machache kushukuru mashabiki wake na watu mbalimbali waliomsaidia kufikia hapo alipo



Diamond na madansa wake wakitumbuiza katika hafla hiyo 10Wasanii mbalimbali pamoja na MaDJ walikuwepo katika hafla hiyo hapa ni Dully Sykes na MawanaFA wakiwa na baadhi ya MaDJ 11Maurice Njowoka kutoka Cocacola wa pili kutoka kushoto na Mwanamuziki AY wa tatu kutoka kushoto pamoja na wadau wengine wakiwa katika hafla hiyo 12 
Mwigizaji Jaquiline Wolper naye alitia timu  13Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akiwa na mama yake Diamond 15Wadau mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo 16 17Mzee Gurumo akihojiwa na waandishi wa habari 18Hawa marafiki zangu wakakumbushia miaka kadhaa waliyofunga ndoa kwa kulishana mishikaki ilipendeza katikati ni Nancy Sumari akishuhudia 19Kulia ni Irene Uwoya kushoto Salma Msangi  20Kushoto AY na Salama Jabir wakipiga story na wadau mbalimbali 21 22Kutoka kulia ni Raymond Kigosi, Irene Uwoya na JB wakiwa katika hafla hiyo.
9