Alhamisi, 5 Septemba 2013

Rooney awajibu wakosoaji wake

Jeraha alilopata Rooney
Wayne Rooney amechapisha picha ya jeraha alilopata kichwani baada ya wakosoaji wake kuhoji kujitolea kwake kuchezea timu ya taifa.

Rooney alijeruhiwa na mchezaji mwenzake wa Manchester United Phil Jones,kwa kumkanyaga kichwani na hivyo kumlazimisha kukaa nje ya mechi za England kufuzu kushiriki kombe la dunia zitakazochezwa Uijumaa na Jumanne.
Alisema kuwa baadhi ya watu wanaonekana kuhoji kujitolea kwake na kusema kuwa amejiondoa kwenye miuchuano ya kufuzu kwa kombe la dunia.

"nina uhakika watu wataona kwa nini sitaweza kucheza.''
Rooney, mwenye umri wa miaka 27, aliongeza kuwa hakuna sababu inayoweza kumzuia kuwasaidia wachezaji wenzake kuweza kufuzu kwa kombe la dunia.

Kocha mkuu wa Man United David Moyes alisema kuwa Rooney huenda asicheze kwa wiki tatu kutokana na jeraha alilopata Jumamosi kabla ya timu hiyo kushindwa na Liverpool, mechi ambayo Rooney hakuweza kucheza kutokana na jeraha.

Mchezaji mwenzake wa timu ya taifa Theo Walcott ameelezea kutishwa na picha hiyo akisema inafanana na picha zinazoonekana tu kwenye filamu.
Rooney ni mmoja wa wachezaji watatu ambao wamejiondoa kutoka kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa sababu ya jeraha alilopata.
Wengine ni Glen Johnson na Jones.

Wabunge wa Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF watoka nje

 
 Wabunge wa Vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi, na Chadema wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge kupinga muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba bungeni dodoma jana.

Dodoma.Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni jana jioni walitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge, baada ya kupuuzwa kwa mwongozo wao wa kutaka kuahirishwa kujadiliwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, hadi hapo Zanzibar itakaposhirikishwa.
Wabunge waliotoka bungeni jana yapata saa 12.15 ni kutoka vyama vya Chadema, CUF na NCCR-
 Mageuzi huku Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP, Augustine Mrema akiendelea kubaki ukumbini.
Kitendo cha wabunge hao wa upinzani kilionekana kuwakera baadhi ya wabunge wa CCM, ambao walisikika wakiwakejeli kwa kupiga meza huku wakisema: “Kwendeni zenu, tumewazoea.”
Wakati wabunge hao wakiondoka, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alikuwa akiwasisitiza wabunge wanaobakia wawe watulivu, maana kuna usalama wa kutosha ndani ya ukumbi huo.

“Mnaotoka nimewaona wote na mnanijua,” alisikika Naibu Spika Ndugai akiwatahadharisha wabunge wa upinzani waliosusa mjadala huo.
Wabunge wa CCM waliendeleza vituko ambapo baada ya wapinzani kutoka, wabunge Juma Nkamia (Kondoa Kusini), Hilary Aeshi ( Sumbawanga Mjini) na Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini) walikwenda kukaa katika viti vya kambi ya upinzani.

Kabla ya kutoka kwa wabunge hao wabunge wawili kutoka CUF waliomba mwongozo wa Spika, wakitaka muswada huo kuondolewa ili kuwapa nafasi Wanzanzibar kutoa maoni yao.
Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mohamed Mnyaa (CUF) aliomba mwongozo akitaka muswada huo uondolewe, hadi hapo Wazanzibar watakaposikilizwa.
Alisema kuwa kwa maoni ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala wamesikiliza maoni ya wadau wengi, lakini Zanzibar hawakwenda kuwasikiliza wadau wa eneo hilo.

“Na hili suala zima katika masuala ya katiba linahitaji usawa wa washirika, tunazungumza kitu kinachohusiana na Zanzibar na Tanzania Bara, ili kupata maoni ya nchi nzima kuna uhalali gani wa Bunge hili kuendelea na mjadala huu?” alihoji.
Hata hivyo, alikatizwa na kelele za Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (CCM), ambaye alitoa taarifa kuwa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ilialika wajumbe mbalimbali ikiwamo Zanzibar.

“Miongoni wa wajumbe walioalikwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na wadau mbalimbali ambao walikuja mbele ya Katiba,” alisema Pindi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo........habari zaidi na Mwananchi Com.LTD

MICHUANO YA KOPA COCA COLA NYANDA ZA JUU KUSINI VIWANJA VYA IYUNGA -MBEYA

Iringa FC kopa Coca Cola Cup

Mwalimu wa Timu ya Iringa FC kopa Coca Cola akitoa maelekezo kwa vijana wake

 Mwalimu wa michezo timu ya Iringa FC Kopa Coca Cola

Timu Iringa Fc Kopa Coca Cola chini ya umri wa miaka 15

Vijana wa Iringa FC kopa Coca Cola wakifanya mazoezi katika viwanja vya Iyunga-Mbeya

MICHUANA YA KOPA COCA COLA CHINI YA MIAKA 15 IKIENDELEA KATIKA VIWANJA VYA IYUNGA-MBEYA

Timu ya Sumbawanga ikijinoa kwa mazoezi katika viwanja vya Iyunga-Mbeya
Sumbawanga FC Kopa Coca Cola

Nahodha wa timu ya Sumbawanga akiongoza mazoezi

Mwalimu wa michezo timu ya Sumbawanga FC kopa Coca Cola

Waalimu wa timu ya Sumbawanga wakitoa Mazoezi kwa vijana wao

Sumbawanga FC kopa Coca Cola

Wajua kwa nini unahitaji kulala?

Usingizi unasaidia kukuza celi za ubongo wako

Wanasayansi wanaamini kuwa wamepata sababu moja mpya ya kwa nini tunahitaji usingizi.
Wanasema kuwa kulala kunasaidia katika kujenga celi mpya za ubongo.
Usingizi unasaidia kuzalisha upya celi za ubongo ambazo nazo hujenga kemikali inayojulikana kama Myelin ambayo ni muhimu katika kulinda ubongo wetu kwa ambavyo unafanya kazi.

Matokeo ya utafiti huu ambayo yalijitokeza katika panya wa mahabara, huenda yakachochea maelezo zaidi kuhusu umuhimu wa usingizi katika kukabarabati celi za ubongo na kukuza celi mpya pamoja na kuulinda kutokana na magonjwa.
Daktari Chiara Cirelli na wenzake kutoka chuo kikuu cha Wisconsin waligundua kuwa Panya hao walipokuwa wanalala, ndipo kemilaki hiyo ilikuwa inatengezwa kwa wingi na celi za mwili.
Ongezeko la kemikali pia ilitegemea aina ya usingizi ambao Panya walilala hasa uliohusishwa na ndoto.

Kinyume na hilo, celi zilionekana kufariki wakati Panya walipokuwa wako macho wazi.

Na hii ndio maana usingizi ni muhimu jambo ambalo wamekuwa wakilihoji wanasayansi kwa miaka mingi. Yaani nini umuhimu wa usingizi?
Ni wazi kuwa tunahitaji kulala ili kupumzika na ili ubongo wetu ufanye kazi vyema....lakini mambo ya kibayolojia yanayofanyika tunapokuwa tumelala ndio yameanza tu kugunduliwa.

Daktari Cirelli alisema kuwa : "kwa muda mrefu, watafiti wa usingizi wamekuwa wakilenga tofauti iliyopo kati ya celi za neva wakati wanyama wanakuwa hawajalala na wakti wamelala. Kwa sasa ni bayana kuwa celi zengine kwenye mfumo wa neva hubadilika kutokana na usingizi.''
Watafiti hao wanasema kuwa matokeo yao yanapendekeza kuwa ukosefu wa usingizi,unaweza kusababisha maradhi ya ubongo yanayoathiri celi zake.

Watafiti hao pia wanataka kuchunguza ikiwa vijana kukosa usingizi wakati wanapokuwa huenda ikaathiri ubongo wao katika siku za usoni.
Usingizi ni muhimu kwa mfumo wa neva mwilini ili uweze kufanya kazi vyema.
Usingizi pia husaidia katika uzalishaji wa homoni zinazowafanya watoto na vijana kukuwa.