Jumatano, 18 Septemba 2013

TCRA WAANZA KUWANOA MA BLOGGERS TANZANIA

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akiwasilisha mada ya kwanza juu ya Ukubwa wa Sekta ya Mawasiliano hapa nchini wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.


Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akifafanua jambo wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sekta ya Washangiaji na Watoa Huduma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Dkt. Raynold Mfungahema akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.


 Baadhi ya Viongozi na Bloggers wakiwa wanafuatilia kwa umakini Mafunzo
 Sehemu ya Wapiga Picha kutoka Vyombo mbali mbali vya habari wakiendelea na zoezi la kuchukua matukio mbali mbali wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Blogggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Bloggers mbali mbali hapa nchini  wakiwa kwenye Warsha hiyo ya siku mbili iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es Salaam.

 Kutoka Kulia ni Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joesph Mwaisango akiwa na Blogger Rashid Mkwinda wakifuatilia kwa umakini mafunzo
 Baadhi ya Bloggers wakifuatilia Jambo kwa umakini
 Kutoka kushoto ni Fredy Anthony ambaye anatokea Blogs za Mikoa pamoja na Muwakilishi wa Full Shangwe Blog
 Kutoka kushoto ni Dotto Kahindi kutoka Blog ya Tabia Nchi akiwa na Adela Kavishe

 Mkurugenzi wa Google Africa Joe Mucheru akitoa mada wakati wa Mafunzo kwa Bloggers
 Mmoja ya watoa Maada katika Maswala ya Mitandao ya Kijamii Liz Wachuka akizungumza jambo wakati wa Mafunzo kwa Bloggers.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akijibu Maswali ambayo yaliulizwa na Bloggers wakati wa semina hiyo
 Meza kuu wakifuatilia Mada kwa umakini
 Liz Wachuka Akijibu maswali yaliyo ulizwa na Bloggers
 Afisa Habari wa TCRA Doris Saivoye  akizungumza Jambo wakati wa Mafunzo kwa Bloggers.

Wabunge wa Nigeria wapigana bungeni


Wabunge wa bunge la waakilishi Nigeria wamerushiana ngumi wakati wa vikao vya Jumanne baada ya kuzuka bungeni suitofahamu kuhusu mrengo wa wabunge waliojitenga na chama tawala. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.
 
Chama tawala cha PDP kimekuwa kikikumbwa na mgogoro wa ndani kwa muda sasa
Kituo kimoja cha kibinafsi cha televisheni, pamoja na vituo vingine vilionyesha picha za mbunge mwanamke akimtosa kidole usoni kwa ghadhabu mbunge mwenzake wakati mbunge mwanamume akionekana akichukua kiti nusura kumgonga mwenzake.
Wabunge wengine walionekana wakipigana ngumi.
Mgogoro inasemekana ulianza baada ya

Jumatatu, 16 Septemba 2013

YANGA WAMEKATA RUFAA MECHI YAO DHIDI YA MBEYA CITY



Kabla ya mchezo huo kuanza kulitokea vurugu za mashabiki baada ya mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Mbeya City kulipiga mawe basi la Yanga wakati linaingia uwanjani pamoja na gari dogo aina ya Noah lililokuwa limebeba viongozi wa Yanga nalo lilipigwa mawe na kioo cha nyuma cha gari kuvunjika.
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamekata rufaa kwa kamati ya Ligi kutaka mchezo wao dhidi ya Mbeya City uliofanyika Jumamosi iliyopita urudiwe kwenye uwanja huru.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine ulimalizika kwa sare ya 1-1 na kufanikiwa kuingiza Sh100 milioni baada ya mashabiki 20,000 kushuhudia mechi hiyo.
Kabla ya mchezo huo kuanza kulitokea vurugu za mashabiki baada ya mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Mbeya City kulipiga mawe basi la Yanga wakati linaingia uwanjani pamoja na gari dogo aina ya Noah lililokuwa limebeba viongozi wa Yanga nalo lilipigwa mawe na kioo cha nyuma cha gari kuvunjika.
Wakizungumza jijini Mbeya, Ofisa habari wa Yanga, Baraka Kizuguto akisaidiana na mjumbe wa kamati ya sekretarieti ya Yanga, Patrick Naggi walisema, “Tunachohitaji mechi irudiwe na ichezwe kwenye uwanja huru.”

MADAWA YA KULEVYA YAWA GUMZO NCHINI TANZANIA

Wanigeria waliotimuliwa Kenya kwa kujihusisha na dawa za kulevya watumia Uwanja wa Ndege Dar kurejea tena. Mmoja adakwa na pakiti 400 za heroin baada ya kusafiri kwa gari  kupitia Namanga
Raia wa Nigeria aliyefukuzwa Kenya miezi minne iliyopita kwa kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya, amekamatwa tena nchini humo akiwa na pakiti 425 za heroin, akiaminika kwamba alipitia Tanzania.
Mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Enobemhe Emmanuel Peter inaaminika alishukia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, akitokea Nigeria na kisha kwenda Kenya kwa barabara, kupitia mpaka wa Namanga mkoani Arusha.
Peter alikamatwa pamoja na mwanamke ambaye ni

Mdhalilishaji aliyejidai kuwa Justin Bieber



Hunter alijidai kuwa Justin Bieber ili watoto wamtumie kanda za video za ngono
Rober Hunter aliwahidi watoto kuwa angekuwa na uhusiano wa kimapenzi nao  
Mwanamume mmoja nchini katika kitongoji cha Middlesbrough, Uingereza aliyejidai kuwa mwanamuziki maarufu duniani , Justin Bieber, ili kuwahadaa watoto kuweza kumtumia kanda za video wakiwa wanafanya vitendo vya ngono, amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela.
Robert Hunter, mwenye umri wa miaka 35, na ambaye alijidai kuwa 'Justin Bieber Hunter 'alikamatwa baada ya msichana mmoja kutoka Tasmania kufahamisha polisi kumhusu.
Polisi walimkamata nyumbani kwake akiwa na