Jumapili, 22 Septemba 2013

MBEYA CITY FC YAPATA MASHABIKI LUKUKI BAADA YA KUTOA SARE YA GOLI 2-2 NA SIMBA FC HAPO JANA

 KIPINDI CHA PILI KIKIWA KINAENDELEA
 MASHABIKI WAKIWA WANAFUATILIA MECHI KWA UKARIBU 
 MBEYA CITY WAKIWA WAMEPATA GOLI LA PILI
 MBEYA CITY FC WAKISHANGILIA GOLI LAO LA PILI
 MASHABIKI WA MBEYA CITY FC WAKIWA WANASHANGILIA GOLI LA PILI


KOCHA MKUU WA MBEYA CITY FC BWANA MWAMBUSI WA KWANZA KUTOKA KUSHOTO AKIFUATILIA MECHI KWA UMAKINI.
 MASHABIKI WA SIMBA WAKIWA WAMEPOA BAADA YA M BEYA CITY FC KURUDISHA GOLI
 MASHABIKI WA MBEYA CITY FC WAKIWA WENYE FURAHA 
HAPA ILIKUWA NI PATA SHIKA NGUO KUCHANIKA BAADA YA SHABIKI WA SIMBA KUINGIA ENEO LA MASHABIKI WA YANGA.
 MPIRA UMEKWISHA
 WACHEZAJI WA SIMBA WAKIWA WANATOKA NJE YA UWANJA BAADA YA MPIRA KWISHA
 WACHEZAJI WA MBEYA CITY FC WAKIWA WANATOKA UWANJANI BAADA YA MPIRA KWISHA
 MASHABIKI WALIO TOKA MBEYA KUSHANGILIA MBEYA CITY FC WAKIWA NJE YA UWANJA WAKIENDELEA KUSHANGILIA MPIRA.

Jumamosi, 21 Septemba 2013

BREAKING NEWS...NAIROBI

Magaidi wateka watu dukani Nairobi

 

Waliojeruhiwa baada ya magaidi kuvamia duka Nairobi
Jengo la maduka liloshambuliwa Nairobi 
SHAMBULIO LA NAIROBI LAUA WATU KADHAA

Watu waliokuwa na silaha wamefyatua risasi mjini Nairobi, Kenya, kwenye eneo la maduka katika mtaa wa Westlands.
Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti piya yalitumika.
Inaarifiwa watu watano wamekufa.
Mwandishi wetu mjini Nairobi anaeleza kuwa washambuliaji inaarifiwa walivaa vilemba kama vya al-Shabaab, lakini haikuthibitishwa kama wapiganaji hao wamehusika.
Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo la maduka liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands, na kuna taarifa ya watu waliojeruhiwa wakitolewa hapo kwa machera.
Inaarifiwa kuwa watu wengi wamenasa ndani ya jengo.
Magari yaliyoegeshwa nje ya maduka yameharibika

 

 

Ijumaa, 20 Septemba 2013

Polisi wakosoa uchunguzi wa Marikana



Wafanyakazi wa Marikana waligoma wakidai nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi

Polisi nchini Afrika Kusini wameikosoa tume inayochunguza mauaji ya wafanyakazi thelathini na nne katika mgodi wa madini ya platinum huko Marikana Agosti mwaka uliopita kusema kuwa walidangaya.
Katika taarifa idara ya polisi imesema kuwa madai dhidi yao ni ya kuudhi na hayana msingi.
Wamesisitiza kuwa walitumia risasi kujilinda walipokuwa wakijaribu kuwatawanya na kuwapokonya silaha wafanyikazi hao waliokuwa wakigoma.

87 wauawa na Boko Haram Nigeria



Mashambulizi yameongezeka tangu jeshi la Nigeria kuanza vita dhidi ya Boko Haram

Wapiganaji wa Boko Haram wamewaua watu 87 katika shambulio katika Jimbo la Borno nchini Nigeria.
Mashahidi wanasema kuwa wapiganaji hao waliteketeza nyumba kadhaa katika tukio hilo la kutisha mnamo Jumanne usiku.
Shambulio hili limetokea siku chache baada ya makabiliano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa Boko Haram

Hakimu achomwa kisu mahakamani


Wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakimuhudumia hakimu Satto Nyangoha aliyechomwa kisu shavuni jana, akiwa mahakamani na mlalamikaji katika kesi ya wizi wa baiskeli, Emmanuel Izengo

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la Nguzo Nane, Kata ya Kambarage Mjini Shinyanga, Satto Nyangoha amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu katika shavu lake la kushoto baada ya kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa baiskeli.
Kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na mlalamikaji katika kesi hiyo,