Haya ni miongoni mwa mashambulizi makubwa ya kigaidi ambayo yamewahi kutekelezwa katika kanda ya Afrika Mashariki.
Septemba. 21, 2013: Magaidi
walitumia maguruneti na bunduki kushambulia jengo la kifahari la
Westgate mjini Nairobi, Kenya lenye maduka na mikahawa themanini na
kuwaua watu zaidi ya sitini huku zaidi ya 175 wakijeruhiwa.Kundi la
kigaidi la Al-Shabab lilikiri kufanya shambulizi hilo.
Oktoba 2011-Machi 2013: Al
Shabaab na wapiganaji wake walifanya mashambilizi kadhaa nchini Kenya na
kuwaua zaidi ya watu sitini wakilipiza kisasi kile walichosema ni hatua
ya Kenya kupeleka majeshi yake nchini huo kupigana dhidi yao. Serikali
ya Kenya ilituma vikosi vyake nchini Somalia baada ya al-Shabab kufanya
mashambulizi kadhaa katika maeneo ya mipakani pamoja na kuwateka nyara
watalii wa kigeni.
Mnamo mwezi Julai tarehe 11,mwaka 2010:
Wanamgambo wa Al Shabaab walilipua misururu ya mabomu katika mji mkuu
wa Uganda Kampala, katika mkahawa ambako mashabiki wa soka walikuwa
wanatizama fainali ya michuano ya kombe la dunia, kwenye skrini kubwa.
Takriban watu 76 waliuawa. Kundi la Al-Shabab lilisema kuwa mashambulizi
hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Uganda kujihusisha na vita dhidi
ya kundi hilo Somalia.
Tarehe 28 mwezi Novemba, mwaka 2002:
Kundi hilo la kigaidi lilishambulia hoteli ya kifahari iliyokuwa
inamilikiwa na waisraeli, katika eneo la Kikambala karibu na mji wa
Mombasa na kuwaua watu 13. Dakika chache kabla ya shambulii hilo,
magaidi hao waliifyatulia makombora ndege ya kiisiralei iliyokuwa
inaruka katika uwanja wa kimataifa wa Mombasa, lakini waliikosa.
Mnamo tarehe saba Agosti, 7 mwaka 1998:
Kundi lengine la kigaidi la Al-Qaida ilishambulia balozi za Marekani
mjini Nairobi na Dar es Salam. Mashambulizi hayo yaliwaua watu 224 ,
wengi wakiwa wakenya . Raia 123 wa Marekani pia waliuawa. Wengine wengi
pia walifuawa nchini Tanzaia.
Jumanne, 24 Septemba 2013
Jumatatu, 23 Septemba 2013
JAMAA WANAOITIKISA KENYA NDIYO HAWA HAPA
Wapiganaji wa Al Shabaab
Hizi ni silaha za Al Shabaab walizonasa wanajeshi wa AU
Kundi la wapiganaji wa kisomali la al-Shabaab,limevamia jumba la
kifahari lenye maduka na mikahawa nchini Kenya. Al Shabaab lenya mizizi
yake nchini Somalia, limeweza kuondolewa kutoka miji mikubwa ya Somalia
ikiwemo Mogadishu na sehemu zengine za Somalia , ingawa bado linasalia
kuwa tisho kubwa kwa kanda nzima.
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyata amewaomba wakenya kuwa watulivu
Raisi
wa Kenya uhuru kenyata amewaomba wakenya kuwa watulivu wakati Huu
ambapo vikosi vya usalama vinafanya jitihada kuhakikisha watu waliobaki
kaitka jengo la WEST GATE wanaokolewa huku akisisitiza kuwa serikli yake
itapambana na magaidi popote pale walipo.
Rais Kenyatta ametoa kauli hiyo wakati akihutubia taifa jana juu
ya tukio la kuuwawa kwa watu wapatao 68 na wengine zaidi ya 200
kujeruhiwa,ambapo alitoa hotuba hiyo mbele ya ya viongozi mbalimbali
wa kisiasa akiwemo aliekuwa waziri mkuu wan chi hiyo raila odinga.
Aidha rais uhuru kenyatta amesema vita hii haihusu dini yoyote wala
kabila lolote bali ni vita ya ugaidi.
Tukio hilo limetokea tangu jumamosi sept 21 ambapo mpaka sasa bado
kuna watu wameshikiliwa na wavamizi hao ndani ya jengo hilo la WEST GATE
MALL lakini serikali ya kenya imewahakikishia wananchi kuwa inafanya
jitihada zote kuwaokoa watu walioko ndani ya jengo hilo.
Askari wa Kenya wakiwa katika harakati za uokoaji
KENYA BADO HALI NI MBAYA MAUAJI BADO YANAENDELEA
Jeshi la Kenya linasema kuwa limedhibiti jengo hilo ingawa hali bado ni mbaya
Wakenya waliofanikiwa kuondoka katika jengo la Westgate kwa usaidizi wa polisi
Huku hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa
katika jengo la Westgate lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika
ndani ya jengo hilo lenye maduka na mikahawa zaidi ya themanini.
Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka nyara raia
ambao idadi yao haijulikani. Walikuwemo ndani ya jengo wakiendelea na
shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab
walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)