Alhamisi, 26 Septemba 2013
MTOTO WA MIAKA MINNE AWAAMBIA MAGAIDI WA WESTGATE KUWA NI WABAYA
MATOKEO YA KOMBE LA CAPITAL ONE ROUND YA TATU 25/09/2013

MANCHESTER UNITED 1-O LIVERPOOL
BIRMINGHAM 3-1 SWANSEA
NEWCASTLE 2-O LEEDS
TRANMERE O-2 STOKE CITY
WEST BROM 1-1 ARSENAL
WAZIRI PINDA APOKELEWA KWA MABANGO KWA BABU LOLIONDO
“Wananchi wanataka amani kwani migogoro imeshasababisha vifo na mali nyingi kupotea sasa tunataka amani,"
Wakazi wa Kata ya Samunge, wilayani Ngorongoro Mkoa wa Arusha,
jana walimpokea Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa mabango wakiomba Serikali
iligawe Jimbo la Ngorongoro na ikomeshe mapigano ya kikabila.
Jumatano, 25 Septemba 2013
TETEMEKO LA ARDHI LAUA WATU 270 PAKISTAN
Zaidi ya watu 300 wamejeruhiwa
Tetemeko kubwa la ardhi limewauwa watu 270 katika mkoa wa Kusini Magharibi wa Balochistan nchini Pakistan.
Tetemeko hilo la kipimo cha 7.7-lilipiga Jumaanne alasiri . Nyumba nyingi zilibomolewa na watu wengi walipaswa kulala nje
Baada ya tetemeko hilo ,kisiwa kidogo kiliibuka nje ya mwambao karibu na bandari ya Gwadar.
Watu walikusanyika ufukweni kushuhudia kisiwa
hicho kipya ambacho kinakadiriwa kua na urefu wa mita 200 na upana wa
mita 100 na kiinuka mita 20 kutoka upeo wa bahari .
Balochistan ndio mkoa mkubwa wa Pakistan lakini ukiwa na watu wakaazi wachache kupita yote
Eneo hilo hukumbwa na mitetemeko ya mara kwa
mara na mnamo mwezi wa Aprili watu 35 waliuwawa katika tetemeko ambalo
kitovu chake kilikua Kusini Mashariki mwa Iran mnamo mwezi wa April
Tetemeko hilo lilikua la nguvu hata watu wa miji
iliyo mbali ya Karachi, Hyderabad, na mji mkuu wa India, Delhi walihisi
mtikisiko wake.
Vijiji vizima inaarifiwa vilifyekwa katika wilaya ya wakaazi masikini ya Awaran
Msemaji wa serikali ya Balochistan, Jan Buledi,
amesema waliopatwa na maafa zaidi ni katika mji wa Awaran na vijiji
vinavyouzingira na ameonya idadi ya vifo huenda ikaongezeka. Takriban
watu 340 wamejeruhiwa.
Msemaji huyo amesema kuna ukosefu mkubwa wa huduma za matibabu na hospitali hazina nafasi za kutosha kuwatibu majeruhi .
Alisema helikopta zinawasafirisha majeruhi mahututi hadi mjini Karachi na wengine wanahudumiwa katika wilaya jirani.
Jeshi la Pakistan lilikua miongoni mwa makundi
ya kwanza kutoa msaada kwa kua tayari limekua huko miaka kadhaa sasa kwa
sababu ya uasi wa watu wanaotaka kujitenga kwa mkoa huo wa Balochistan.
Jeshi limesema limetuma zaidi ya wanajeshi 200 ,
wana matibabu na mahema kutoka mji mkuu wa mkoa huo Quetta, lakini
shughuli za uokozi zinatatizwa kwa hali ya milima ya eneo hilo.
SHAMBULIO LA WASTGATE LAATHIRI MASHINDANO YA MAGONGO
Mashindano ya magongo
Mashindano
ya magongo kwa mataifa ya Afrika yaliyopangiwa kuanza Alhamisi wiki hii
mjini Nairobi huenda yakaahirishwa kutokana na mkasa wa jumba la
Westgate lililovamiwa na magaida wa Al Shabaab, na zaidi ya watu sitini
kuuawa
Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa magongo cha
Kenya Nashon Randiak anasema shirikisho la kimataifa,FIH, lina wasiwasi
kuhusu usalama wa wachezaji mjini Nairobi baada ya magaidi wa Al Shabaab
kulivamia jengo la kibiashara la Westgate jijini Nairobi.
Licha ya Randiak kuwaeleza kwamba hali sasa ni
shwari baada ya magaidi wote kuuwa na wanajeshi wa Kenya shirikisho la
kimataifa limesema linataka mkuu wa polisi nchini Kenya kuwahakikisha
usalama wa wachezaji.
Randiak ameshangazwa na msimamo huo akisema
mashambulizi ya magaidi hutokea kote duniani hivyo anashangaa ni kwanini
hili la Kenya linachukuliwa ni kama la kipekee..
Mataifa yanayotarajiwa kushiriki kwa wanaume ni
Kenya, Ghana na Afrika Kusini na kwa wanawake ni Kenya, Tanzania,Ghana
na Afrika Kusini. Timu ya Tanzania ikiongozwa na katibu wa chama cha
magongo mkoa wa Dar es salaam Mnonda Magani tayari imeshawasili mjini
Nairobi.
Timu ambazo zimejiondoa kwa sababu mbali mbali na sio hiyo ya Westgate ni pamoja na Nigeria, Namibia, Misri na Ushelisheli.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)