Jumanne, 29 Oktoba 2013

HUU UWE MFANO WA KUIGWA NA VITUO VINGINE VYA RADIO HAPA TANZANIA

KITUO CHA RADIO ROCK FM 96.9 MBEYA CHASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA MITATU NA KUTOA ZAWADI KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA TUMAINI UYOLE MBEYA

Mkurugenzi wa kituo cha ROCK FM 96.6 Allen Ezekia akiwakabidhi zawadi watoto wa kituo cha tumaini 

BABA MZAZI LAWENA NSONDA ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kutimiza miaka 3 ya kituo cha ROCK FM akikabidhi zawadi wa watoto wa kituo hicho cha tumaini pia LAWENA alitoa zawati ya vyereheni viwili vya kushonea nguo katika kituo hicho
Mkurugenzi wa kituo cha Tumaini Elias Katani akipokea zawadi kwa niaba ya watoto wa kituo chake toka kwa mkurugenzi wa ROCK FM ya jijini Mbeya
Watoto wa kituo cha tumaini wakishukuru kwa zawadi walizopewa na kituo cha ROCK FM
Lawena Nsonda amewatka wadau mbali mbali kujitokeza kuwasaidia watoto yatima kwani ni jukumu letu sote katika kuwalea
Mkurugenzi wa kituo cha Tumaini Elias Katani akishukuru kwaniaba ya watoto kwa zawadi walizopatiwa na Rock Fm 96.6 
Mratibu Elimu kituo hicho Obadia Mbilinyi akisoma taarifa fupi ya kituo hicho cha Tumaini
Mara baada ya kutoka toa zawadi kwa watoto yatima sherehe iliendelea katika viwanja vya TIA Mbeya
Moja ya watangazaji wa Rock Fm Harubu Kabwe akimkaribisha mkurugenzi wake aje apate keki katika sherehe hiyo
BABA MZAZI LAWENA NSONDA akimlisha keki mkurugenzi wa ROCK FM 96.9 Allen Ezekia katika sherehe ya kutimia miaka 3 sherehe zilizofanyka katika uwanja wa chuo cha TIA Mbeya
Mkurugenzi wa kituo cha ROCK FM 96.6 Allen Ezekia akiwashukuru wasikilizaji wa Rock fm waliojitokeza katika sherehe hiyo ya kutimiza miaka 3 na kuwaahidi kuwa watazidi kuwaletea habari za uhakika na kuburudisha
 Mgeni rasmi katika sherehe hiyo BABA MZAZI LAWENA NSONDA akiwahutubia wananchi waliohudhuria sherehe za kutimia miaka 3 ya kituo cha ROCK FM 96.9 
Burudani mbali mbali zilikuwepo katika sherehe hiyo ya kutimiza miaka 3 ya ROCK FM 96.9 
Dachi Nationale Band wakitumbuiza katika sherehe ya kutimiza miaka 3 ya ROCK FM 96.9
Watangazaji wa kituo cha Radio ROCK FM 96.9 wakiwa katika picha ya pamoja

Na Mbeya yetu

YAJUE MAGAZETI YA LEO TAREHE 29.10.2013...KINANA AZIMA MAPINDUZI UVCCM,MALINZI AWATOA KIFUNGONI VIGOGO TFF NA MNYAMA AUAWA KWA KULAMBA LAMBA LAMBA ZA AZAM

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Jumatatu, 28 Oktoba 2013

BBC SEMA KENYA YAFANYA KWELI...SHUHUDIA KATIKA PICHA

Walioshiriki mjadala wa BBC Sema Kenya katika kaunti ya Laikipia.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/27/131027110942_sk_nanyuki_photos_12_976x549_bbc_nocredit.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/27/131027105109_sk_nanyuki_photos_01_976x549_bbc_nocredit.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/27/131027105704_sk_nanyuki_photos_05_976x549_bbc_nocredit.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/27/131027110426_sk_nanyuki_photos_09_976x549_bbc_nocredit.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/27/131027111118_sk_nanyuki_photos_13_976x549_bbc_nocredit.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/27/131027110800_sk_nanyuki_photos_11_976x549_bbc_nocredit.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/27/131027111949_sk_nanyuki_photos_main_976x549_bbc_nocredit.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/27/131027110044_sk_nanyuki_photos_07_976x549_bbc_nocredit.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/27/131027105350_sk_nanyuki_photos_03_976x549_bbc_nocredit.jpg
Mjadala huu ulimulika umilikaji wa mashamba, na maendeleo ya wenyeji wa kaunti ya Laikipia.
Hiki ni kipindi cha mjadala na ambacho hupeperushwa kupitia redio, televisheni na kwenye tovuti.
Kipindi hiki kinazuru maeneo tofauti ya nchi, lengo likiwa ni kuwapa wananchi fursa ya kuelezea hoja zao, kupata taarifa na kushiriki katika mjadala wa kitaifa.
Tangu kilipozinduliwa mwaka jana, Kipindi cha Sema Kenya kimefaulu kuandaa mijadala mikali iliojumuisha wananchi ikiangazia masuala ya usalama, mihadarati, ukabila, ugatuzi, ugavi wa ardhi na marekebisho ya sheria za ugavi wa ardhi.
Watu wanaweza kushiriki katika mazungumzo haya ya kitaifa kupitia tovuti ya BBC, mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.
Aidha, njia nyingine Sema Kenya inawafikia wananchi ni kupitia mashirika ya kijamii ambayo kipindi hiki kinashirikiana nao.
Mtindo wa Sema Kenya:
Lugha: Sema Kenya inaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili.
Utafiti: Sema Kenya inategemea utafiti wa kina kufanikisha makala haya.
Wanaoshiriki: Kinahusisha watu wa tabaka mbalimbali; vijana kwa wazee, wanawake na wawakilishi wa vikundi maalum.
Huwaleta pamoja wananchi na viongozi wao: Wananchi wa kawaida na jamii zilizotengwa wanapata fursa ya kuwahoji viongozi wao.
Mada ya mjadala huamuliwa na washiriki katika kipindi hiki.
Haibagui, haipendelei na inashirikisha kila moja kupitia redio na kwenye tovuti.
Mjadala huendelea kwenye mtandao wakati kipindi kikiwa hewani hata baada ya kutia tamati kwenye redio.
Sikiliza na ushiriki kwa Sema Kenya
Televisheni: KBC kila Jumapili saa kumi na mbili jioni
Redio: Idhaa ya Dunia ya BBC (Nairobi 93.9FM, Mombasa 88.1FM) kila Jumapili saa saba alasiri.
 

AFRIKA NA MATUKIO KATIKA PICHA

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028123736__70679408_01_zim_jacaranda2_ap.jpg
Washidani katika mashindano ya mwanadada mrembo zaidi ya Miss Jacaranda nchini Zimbabwe wakionyesha hapa viatu vyao tayari kwa kutembea kwa madaha ukumbini
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028123749__70679410_02_tanzania_afp2.jpg 
Mjini Moscow Miss Tanzaia 2013 Betty Omara hapa anaonekana akirembwa kabla ya kupigwa picha. Shindano la mwanamke mrembo zaidi ulimwenguni litafanyika nchini Urusi mwezi Novemba ,9
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028130609__70694968_nigeria_fashion_afp.jpg
Hapa wanamitindo wa kiume wakiwa mjini Lagos wakishiriki onyesho la mitindo 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028123801__70694745_04_nigeriaz_breakdance_afp.jpg
Vijana wanadansi wa Nigeria wanaojulikana kama Space Unlimited wanashiriki mashindano ya kimataifa ya wakali wa Breakdance nchini Ujerumani siku ya Jumamosi
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028130646__70694972_somalia_afp.jpg
Siku ya Alhamisi kijana huyu alionekana mjini Mogadishu akiwabeba Samaki kutoka baharini katika eneo la Hamarweyne, si mavuno hayo?
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028124004__70694817_09_cameroon_pope_ap.jpg
Papa Francis hapa anaonekana akiongea na Chantelle Biya mke wa Rais wa Cameroon wakati alipokutana naye mjini Vatican siku ya Ijumaa
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028124025__70694857_11_tunisia_heart_ap.jpg
Mwanamke huyu alikuwa nchini Tunisia na hapa anaonekana akiweka alama ya moyo kwenye ngao ya polisi wakati wa maandamano siku ya Jumatano mjini Tunis
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028123933__70694796_07_kenya_westgate_afp.jpg
Hii ni DVD yenye filamu kuhusu shambulizi la Westgate inayouzwa na mchuuzi mjini Nairobi. Watu 67 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa kwenye mashambulizi ya kigaidi dhidi ya jengo la Westgate mwezi jana. Kundi la Alshabaab lilikiri kufanya shambulizi hilo. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028123918__70694794_06_kenya_soldiers_ap.jpg
Hawa ni wanajeshi wanawake wa Kenya wakiwa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo wakati wa sherehe za kuwakumbuka mashujaa wa Kenya 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028130241__70694877_12_morcco_afp.jpg
Wacheza soka wa Morocco, wanasherehekea baada ya kuingiza bao katika mechi waliyoshinda dhidi ya Croatia siku ya Ijumaa kwa mababo 3-1 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028130541__70694910_14_madagascarbrooms_reuters.jpg
Mjini Antananrivo, kijana huyu anaonekana akiuza vifagio 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028130553__70694942_15_mada_bananas_ap.jpg
Katika mji huohuo, mtoto huyu alipigwa picha akiwa nyuma na ndizi zilizo katika kibanda cha babake cha kufanyia biashara kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/28/131028130620__70694970_liberia_ivory_afp.jpg
Watu mjini Zwedru Liberia, wanapeperusha bendera ya Ivory Coast, huku rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara na mwenzake wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf wakihudhuria mkutano wa viongozi wa kijamii siku ya Jumamosi. Liberia ni nyumbani kwa wakimbizi zaidi ya 62,000 wa Ivory Coast waliotoroka ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2010

USIKOSE WIKI IJAO