Jumatatu, 4 Novemba 2013

KUFAIL MTIHANI SIYO KUFAIL MAISHA...ONA JINSI MWANAFUNZI ALIVYOJINYONGA HADI KUFA KUOGOPA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE

 
Mwanafunzi aliyekuwa akisoma  shule  ya  sekondari  Sabasaba  mjini  Iringa akijiandaa kurudia  kufanya  mtihani  wa  taifa  wa kidato  cha nne kupitia  kituo  cha Krelluu mjini  Iringa Khamis Mkundo  mkazi  wa Mwangata  C katika manispaa ya  Iringa amejiua kwa kujinyonga  kwa kamba kwa kile  alichodai  kuchoshwa na kufeli  mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.

Katika  barua  yake  ndefu aliyoiandika  kijana  huyo amesema  kuwa amefanya  hivyo si kwa kujipendea  ila amechukizwa na hatua yake ya  kufeli mara kwa mara  hivyo  kuamua  kujiua ili  kuepuka aibu katika mtihani ujao ambao anaamini angefeli.

Shemeji  wa  kijana  huyo Aden Tagalile ameueleza mtandao  matukiodaima.com  kuwa  tukio  hilo limetokea mida ya saa 12 na saa 1  usiku wa  leo baada ya kuwepo kwa mazungumzo ya muda  mrefu  kwa kijana  huyo kuonyesha kuchukia hatua yake ya kuendelea kuristi  mtihani  wa kidato cha nne  bila mafanikio.

Kijana huyo  alisema hajapenda  kuona anaendelea  kufeli na kuwa  yupo tayari kwa lolote  kukwepa aibu ambayo ipo mbele  yake.
 
Hata  hivyo kufuatia mazungumzo hayo, kijana huyo aliagana na ndugu zake akiwemo kaka  yake anayeishi nae kwa kila mmoja kuondoka nyumbani  hapo kabla  ya kijana  huyo kukutwa amejinyonga.

Mwenyekiti  wa serikali  ya mtaa huo Sarehe Mgimwa amethibitisha  kutokea kwa kifo  hicho na kuonyesha ujumbe ambao kijana  huyo ameuacha .
 
 
 
 
HII NI BARUA ALIYOIANDIKA KABLA HAJAJINYONGA AKIWATAJA BAADHI YA 

MARAFIKI NA WAZAZI WAKE AKIWATAKIA MAISHA MEMA 

CHANZO..Matukio Daima.com

M23 YAWATAKA WAFUASI KUSITISHA MAPIGANO

Wanajeshi wa serikali ya DRC katika vita dhidi ya M23 
Kiongozi wa wapiganaji wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ametangaza kuwa watasitisha mapigano katika vita vyao na jeshi la serikali.

Bertrand Bisimwa alisema kwenye taarifa kwamba anawasihi wapiganaji wote haraka waache uhasama na wanajeshi, ili kuwezesha mazungumzo ya amani kuendelea.

Wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, hivi karibuni wamewasukuma nyuma wapiganaji na kuwatoa katika ngome zao nchini.

Mazungumzo ya amani yanafanywa mjini Kampala, Uganda.

Jumamosi, 2 Novemba 2013

MBEYA CITY,AZAM HAZISHIKIKI LIGI KUU TANZANIA BARA...ZAMNG'OA TENA YANGA KILELENI






















HIVI NDIVYO MCHEZO ULIVYOKUWA KATI YA MBEYA CITY v ASHANTI UNITED

HADI MWAMZI ANAPULIZA KIPYENGA

MBEYA CITY 1-O ASHANTI UNITED

NA KWA MCHEZO HUU MBEYA CITY WAMEJINYAKULIA POINT TATU MHIMU NA 

KUFIKISHA POINT 26 NA KUSHIKA NAFASI YA PILI NYUMA YA AZAM FC KWENYE 

MSIMAMO WA LIGI

PICHA ZOTE NA Free Media To Blogs

TUKIO ZIMA LA MAUAJI YA DEREVA BODABODA ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA LA JUMA JIJINI MBEYA HILI HAPA

 HAWA NI BAADHI YA MADEREVA BODABODA WAKITOA USHIRIKIANO




 HAPA NDIYO ENEO ALILOUAWA MAREHEMU JUMA
MWILI WA MAREHEMU JUMA UKIWA UMEFUNIKWA

PICHA ZOTE NA FREE MEDIA TO BLOGS

MTOTO AKALIA NA KUCHEZEA KITI CHA PAPA FRANCIS I AKIWA NA FURAHA ZOTE