Jumatano, 27 Novemba 2013
AFRIKA KATIKA PICHA
Shabiki wa Tunisia aliyejipaka rangi ashauriana na mtani wake wa Cameroon baada ya mechi jijini Younde huko Cameroon.
Ilikua ni mechi ya marudiano ya kufuzu kwa kombe la dunia ambapo timu ya
“the Lions” walishinda kwa mabao 4-1 na kujikatia tikiti ya kushiriki
kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil. Kulikua na karamu na sherehe
baadaye mjini Younde.
Algeria pia walijikatia tikiti kucheza Brazil baada ya kucheza mechi ya
marudiano, awamu ya pili siku ya jumanne kwa kuilaza Burkina Faso bao
1-0 ,ambayo ilikua furaha kwa mashabiki katika mji mkuu wa Algiers.
Kulikua na mvua mkubwa Afrika Kusini Magharibi mwa mkoa wa Cape wikendi
na kusababisha mafuriko sehemu kadhaa. Matofali yaliyotengenezwa
yanavunjika pakiwa na maji mengi
Maonyesho ya kudumu ya nyaraka kuhusu maisha ya Nelson Mandela
yalifunguliwa siku ya jumatatu katika kituo cha makumbusho cha Nelson
Mandela jijini Johannesberg. Hivi ni vitabu vya Nelson Mandela
alivyokuwa navyo gerezani katika kisiwa cha Robben alikokua amefungwa
kwa juhudi zake za kupinga ubaguzi wa rangi. Aliachiliwa baada ya miaka
27, mwaka wa 1990 na kuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo kuchaguliwa kwa
miaka nne kupitia democrasia
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na mkewe Grace wahudhuria sherehe ya
mahafali ya binti wao Bona katika chuo kuku huko Singapore Jumamosi.
Pia Jumanne,kijana mmoja katika soko la Gorongosa katikati mwa Msumbiji anajikinga kwa kutumia mwavuli.
Siku iliyopita, mwandamanaji nchini Tunisia avaa bereti na beji
inayoonyesha picha ya aliyekuwa kiongozi wa Iraq Saddam Hussein,wakati
wa maandamano dhidi ya muungano wa kiislamu unaoongozwa na chama tawala
cha muungano katika mji mkuu Tunis.
Siku hio,vijana wawili wadogo wanalima shamba lililoko kando ya barabara
kuu inayounganisha jiji kuu la Mogadishu na Baido lililo karibu na
shamba lenye rotuba karibu na Afgoye inayojulikana kwa mavuno bora
nchini Somali
Walinzi wa Somal, wakishika doria katika fuo za bahari mjini Bosasso, katika eneo lililojitenga na Somalia la Puntland
Katika kijiji kimoja Kaskazini mwa Kenya ,kijana asimama kando kando na
fahali aliyenona kabla ya kuwasilishwa kwa kamishna mkuu wa Uingereza
kutoka kwa jamii ya Wasamburu ya Nanuyak kama zawadi ili kusheherekea
kuzaliwa kwa mwana mfalme George Mwakani.
Mji mkuu wa Kenya Nairobi uliandaa maonyesho ya magari siku ya
Jumapili,huku gari aina ya Peugeot 203 ya mwaka 1959 ikiwemo kati ya ya
magari 70 kwenye maonyesho katika uwanja wa mashindano wa Ngong.
Kijana mmoja katika jiji kuu la Mali Bamako,ajaribu kuyagonga mapera
kutoka kwa mti siku ya jumatano. Uchaguzi wa kiubunge utafanyika nchini
humo jumapili.
Ijumaa, 22 Novemba 2013
BABU SEYA NA MWANAE MAISHA YAO YOTE JELA
Nguza Viking na mtoto wake Papii wakitoka mahakamani
Mahakama ya Rufaa nchini
Tanzania imetupilia mbali ombi la warufani wawili Nguza Viking na
mwanaye, ambao waliomba mahakama hiyo kufanya marejeo ya uamuzi wake wa
awali wa kuwapata na hatia kama ambavyo hukumu dhidi yao ilivyotolewa na
mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2004.
Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya na watoto
wake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na
kulawiti watoto.Mwaka 2010, rufaa yao ilisikilizwa katika Mahakama ya Rufaa, na kuwaachia huru Nguza Mashine na Francis Nguza baada ya kuwaona hawana hatia katika makosa yote waliyoshitakiwa.
Baada ya rufaa hiyo, Babu Seya na mwanaye Papii Kocha walipatikana na hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Tarehe 30 Oktoba mwaka huu, Mahakama ya Rufaa iliyoketi chini ya jopo la majaji watu, likiongozwa na Nathalia Kimaro, akisaidiana na Mbarouk Mbarouk na Salum Masati walisikiliza hoja za pande zote kuhusu ombi la kufanyika mapitio ya uamuzi wa awali wa mahakama hiyo.
Alhamisi, Mahakama ya Rufaa baada ya kufanya mapitio ikiwa imeketi chini ya majaji watatu, imeendelea kuwaona warufani hao wawili kuwa na hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu yao.
Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili wao Mabere Marando uliomba kupitiwa upya kwa uamuzi huo, ukidai kuwepo kasoro katika ushahidi uliowatia hatiani, ikiwemo kukosekana kwa mashahidi muhimu katika kesi hiyo.
Majaji walisema kuwa kuna uthibitisho kuwa warufani hao wawili waliwabaka watoto wa shule ya msingi mwaka 2003.
Kesi hiyo imewashtua mashabiki wa mwanamuziki Viking nchini Tanzania na kanda nzima ya Afrika Mashariki.
Mwanamuziki huyo mwenye kuimba nyimbo za Rhumba, ambaye ni mzaliwa wa DRC, ameishi Tanzania kwa miaka mingi na kuwa na mashabiki wengi.
Mwandishi wa BBC Ben Mwang'onda mjini Dar es Salaam anasema kuwa Nguza Viking na mtoto wake Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha ambaye pia ni mwanamuziki, walifika mahakamani hapo kusikiliza hatma yao.
Walionekana kuwa watulivu wakati majaji walipotupilia mbali ombi lao kutaka hukumu yao kubatilishwa.
Walihukumiwa kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule ya msingi waliokuwa kati ya umri wa miaka sita na nane wote waliokuwa katika shule ya msingi ya Mashujaa wilayani Kinondoni mjini Dar es Salaam.
Wakili wa muimbaji huyo alisema kuwa mwanamuziki huyo hana matumaini tena ya kupewa rufaa kwani hili ndilo ombi lake la mwisho.
Alhamisi, 21 Novemba 2013
MWATHIRIWA WA UBAKAJI AKAMATWA SOMALIA
Sio mara ya kwanza kwa mwathiriwa wa ubakaji kukamatwa baada ya kusimulia yaliomkumba Somalia
Msichana mmoja amekamatwa mjini
Mogadishu Somalia, baada ya kusimulia kituo kimoja cha redio nchini humo
kuhusu alivyobakwa na watu waliomtishia kwa bunduki.
Mwandishi aliyemhoji msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 pia amezuiliwa.Umoja wa Mataifa unataka uchunguzi ufanywe kuhusu madai hayo ukiwema kuwa unapiga darubini uhuru wa vyommbo vya habari na ambavyo serikali itachunguza kisa hiki.
Serikali ya Somalia inasema kuwa lazima haki itendeke.
Mapema mwaka huu , mwathiriwa mmoja wa ubakaji pamoja na mwandishi wa habari walifungwa jela mwaka mmoja ingawa waliachiliwa baadaye kutokana na uamuzi wa kesi ya rufaa.
Ubakaji na waandishi wa habari wanaoripoti visa vya ubakaji au dhuluma nyinginezo za kingono, ni mada ambayo huhofiwa kuzungumziwa nchini Somalia na kesi hii ndio ya hivi karubui kuhusu polisi kumkamata mwathiri wa ubakaji pamoja na mwandishi habari aliyemhoji.
Msichana huyo aliambia kituo cha redio cha Shabelle, kuwa alibakwa na waandishi habari wenzake wawili wakiwa akiwa ameshikiliwa bunduki.
"mmoja alinitishia kwa bunduki na kunipeleka chumbani kwa nguvu , na kunivamia huku akinivunjia heshima yangu, '' msichana huyo alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema katika video kwenye mtandao wa Redio Shabelle.
"ninaomba serikali kuchukua hatua dhidi ya wabakaji hawa, huenda wamewatendea unyama huu wasichana wengine wasio na uwezo wa kujitetea,'' alisema msichana huyo.
Video hiyo imepeperushwa kwenye mitandao mingine ya habari nchini humo.
Polisi walimkamata mwanamke huyo pamoja na mwandishi wa habari Mohamed Bashir Hashi, aliyemhoji pamoja na mkuu wa idhaa ya Redio Shabelle Abdulmalik Yusuf.
Hakuna hata mshukiwa mmoja, aliyetuhumiwa amechukuliwa hatua za kisheria.
Hata hivyo serikali ya Somalia imesema kuwa ubakaji na dhuluma dhidi ya wanawake ni mambo ambayo hayaruhusiwi hata kidogo, ingawa haikutamka chochote kuhusiana na kesi hii.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)