Alhamisi, 29 Mei 2014

TAZAMA MAZISHI YA MSANII WA BONGO MOVIE RECHO, KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Majeneza yenye miili ya Recho na mwanaye.Miili ya Rachel Haule 'Recho' na mwanaye ikishushwa kwenye gari maalum baada ya kuwasili Viwanja vya Leaders ikitokea nyumbani Palestina, Dar tayari kwa kuagwa.Waombolezaji wakiwa na simanzi baada ya mwili kuwasili Leaders.


Mwenyekiti wa Bongo Muvi Steven Nyerere akiweka shada la maua katika kaburi.
Ndugu wa marehemu wakiweka mashada.
Wasanii wa Bongo Muvi kutoka kushoto Ant Lulu akiwa na wenzake.
Watumishi wa Mungu katikati wakifanya maombi baada ya maziko.
Mchumba wa marehemu George Saguda (kushoto) akiweka udongo katika kaburi la Rachel na mwanae
Msanii Blandina Chagula 'Johari' akiweka mchanga
Mjomba wa marehemu, Evance Haule (kushoto) akiweka mchanga katika kaburi la marehemu.
Ndugu wa marehemu wakiweka mchanga katika kaburi la marehemu Recho Haule.
Mafundi wakichanganya zege.
Mafundi wakisawazisha zege.
(PICHA NA RICHARD BUKOS, DENIS MTIMA, MAYASA MARIWATA, SHANI RAMADHANI, HAMIDA HASSAN, IMELDA TARIMO/GPL)

Alhamisi, 10 Aprili 2014

HABARI MPYA KWA WATANZANIA WOTE

MAWAKALA WA AJIRA NA KAZI WANAPATIKANA MBEYA, WENYE MAHITAJI MNAKARIBISHWA.


Meneja wa Kampuni ya New Position Co.Ltd, Juma Burah akizungumza jambo na waandishi wa habari(hawapo pichani) ofisini kwake.

Meneja akionesha tangazo la kuthibitishwa kwa kampuni yake na Wizara ya Kazi na Ajira katika gazeti la Mtanzania


Meneja aikionesha moja ya mashine ambazo wanahitaji vijana wenye fani ya Mauzo kwa ajili ya kuuza na kusambaza kwa wafanyabiashara.

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwajibika kazini.



KAMPUNI ya New Position Co Ltd, ni kampuni iliyosajiliwa kisheria chini ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa namba 105407 yenye lengo la kuwaunganisha waajiri na waajiri popote nchini Tanzania.
Kampuni hiyo ni wakala wa ajira na kazi ambayo kazi yake ni kuwatafutia ajira wahitimu wa ngazi mbali mbali wanaohangaika kuomba kazi katika mashirika mbali mbali ikiwa ni pamoja na mashirika au makampuni yanayohitaji wafanyakazi.
Akizungumza na mtandao huu, Meneja wa Kampuni hiyo, Juma Burah amesema watanzania wengi hawajui jinsi ya kuandika barua za kuomba kazi pamoja na wasifu wao(CV) jambo lililopelekea kuanzisha kampuni kwa lengo la kuwakomboa vijana.
Amesema mwombaji wa kazi anapaswa kupeleka vyeti vyake na shilingi elfu kumi na tano(15,000/=)ambazo zitasaidia kupewa mafunzo jinsi ya kuandika cv, barua ya maombi pamoja na kujieleza wakati wa usaili ili muombaji aweze kumudu ushindani uliopo.
Ameongeza kuwa kazi ya kampuni mbali na kutafuta ajira na kazi pia inaibua fursa za ajira kupitia mtandao ambapo sifa za muombaji huwekwa mtandaoni ili wenye kuhitaji wafanyakazi huwapata kiurahisi.
Meneja huyo ameongeza kuwa tangu kusajiliwa kwa kampuni hiyo imepita miezi sita lakini wamepata mafanikio makubwa kwa kuwawezesha wafanyakazi zaidi ya 300 kupata mafunzo na kuajiriwa katika sekta mbali mbali.
Ameongeza kuwa mbali na kampuni kuwatafutia kazi watu mbali mbali pia Kampuni yenyewe inanafasi 50 za wataalamu wa fani ya IT, Mauzo na mapokezi.
Kampuni hiyo pia inaubia na kampuni ya BOLSTO inayohusika na uuzaji wa mashine mbali mbali za Kielectroniki kama vile EFDs ambazo ziko za aina tofauti tofauti  ambazo ni Prima, Dp25, Best LC, Ultima na Easy Machines inayofanya kazi ya uwakala wa fedha kama Mpesa, Tigo Pesa, Zuku, Dstv nk.
Amesema pia kampuni hiyo inanafasi 20 za kazi kwa ajili ya kuuza na kusambaza mashine hizo ambapo muuzaji atanufaika na Kamisheni kutokana na mauzo ya mashine hizo
Kampuni hiyo inapatikana katika Jengo la Crdb Ghorofa ya kwanza kushoto au unaweza kupiga simu namba 0718 470499 au kwa barua pepe info@newposition.com au tembelea wavuti wao wa www.new-positions.com. Mbeya mjini.

Jumatatu, 10 Machi 2014

WAFANYABIASHARA WA MCHANGA NA KOKOTO JIJI LA MBEYA WAJA JUU KUILALAMIKIA WIZAZRA YA NISHATI NA MADINI

 
 

 
 
 
Bwana nidhamu wa wachimbaji na wasafirishaji bidhaa hizo Peter Hezron N’gwavi amesema kuwa kitendo cha tozo na leseni kitafanya vijana waliojiajiri kuanza kufanya vitendo vya uhalifu kutokana na ukosefu wa mitaji.
 

 
 
Mkurugenzi wa Jiji Mussa Zungiza amesema kuwa madai yao hayahusu ofisi yake bali wenye dhamana ya kujibu kero hizo ni mamlaka husika ambayo ni Wizara ya Nishati na Madini hivyo atawaomba wawakilishi wao waweze kujibia kero zao.
 
 
 
 Mwanasheria wa jiji akifafanua jambo 
 
Mhandisi wa Jumanne M. Nkana ambaye ni Afisa Mfawidhi ofisi ndogo ya TMAA Mbeya amesema kuwa waraka wa kulipia bidhaa za Mchanga,Kokoto na Mawe ulipitishwa na Bunge Mwaka 2010 ndipo ulipoanza kutumika rasmi kwa tozo la asilimia 3 kwa bei ya bidhaa iliyopo Sokoni.
 
 
 
 
 
 
 
 
Wafanyabiashara ya Madini ya mchanga,kokoto na mawe Jiji la Mbeya wameandamana kwenda ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji kwa kutumia maroli kupinga waraka wa Wizara ya Nishati na Madini unaowataka watumiaji wa bidhaa hiyo kulipia shilingi elfu mbili mia tano kuanzia Machi 3 mwaka huu.

Maandamano hayo yalipokelewa na Mkurugenzi wa Jiji Mussa Zungiza ofisini kwake ambapo alikana kutoa waraka huo na kufafanua kuwa waraka huo umetolewa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini[Tanzania Minerals Audit Agency-TMAA].

Akitoa malalamiko yao mbele ya Mkurugenzi Bwana nidhamu wa wachimbaji na wasafirishaji bidhaa hizo Peter Hezron N’gwavi amesema kuwa kitendo cha tozo na leseni kitafanya vijana waliojiajiri kuanza kufanya vitendo vya uhalifu kutokana na ukosefu wa mitaji.

Mkurugenzi wa Jiji amesema kuwa madai yao hayahusu ofisi yake bali wenye dhamana ya kujibu kero hizo ni mamlaka husika ambayo ni Wizara ya Nishati na Madini hivyo atawaomba wawakilishi wao waweze kujibia kero zao.

Mhandisi wa Jumanne Mohammed ambaye ni Afisa Mfawidhi ofisi ndogo ya TMAA Mbeya amesema kuwa waraka wa kulipia bidhaa za Mchanga,Kokoto na Mawe ulipitishwa na Bunge Mwaka 2010 ndipo ulipoanza kutumika rasmi kwa tozo la asilimia 3 kwa bei ya bidhaa iliyopo Sokoni.

Hata hivyo Mohammed amesema kuwa leseni za uchimbaji wa bidhaa za ujenzi hazihusiani na madereva wanaobeba bidhaa  hiyo hivyo wao wanapobeba bidhaa hizo wanapaswa kupata kibali kuoka kwa mmiliki wa mgodi wa madini hayo ambapo kibali hicho hutolewa bure katika ofisi yake iliyopo eneo la Mwanjelwa Jengo la IFAD.

Alimaliza kwa kuwataka wanaotaka kufanya biashara hiyo wafuate taratibu za kisheria ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima kwani hali hiyo inaikosesha Serikali pato halali linalotokana na watu wachache wanaojinufaisha bili kufuata taratibu.
 
endelea kufuatilia blog hii kwa matukio zaidi   
 

SOMA VICHWA VYA MAGAZETI YA LEO HAPA

 

 
 
 
 
 
 

Ijumaa, 7 Machi 2014

HILI NDILO BUNGE LA KATIBA LA TANZANIA

TUKIO KATIKA PICHA: TAZAMA WABUNGE WALIVYOPIGWA BUTWAA JANA KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Halima Mdee, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA), akiwa haamini kinachoendelea kwenye ukumbi wa bunge wakati wajumbe wa bunge hilo walipocharuka jana na hivyo kumlazimisha mwenyekiti wa muda wa bunge hilo Pandu Ameir Kificho, kuliahirisha kwa muda ili kuepusha uchafuzi zaidi wa "Hali ya Hewa"

Halima Mdee akibadilisha style za "mishangao" wakati "Sinema" ya bure ikiendelea

Mbuneg MosesMachali

Christophe Ole Sendeka, naye hakuwa nyuma kwenye "sheshelumbe" la Jana Alhamisi Machi 6, 2014


BUNGE maalum la Katiba, Jana Alhamisi Machi 6, 2014, liligeuka uwanja wa “Mapambano” kama ile vita iliyotikisa ulimwengu, vita ya Kosovo kule eneo la Balkan.

Hata hivyo sio mapambano ya ngumi bali Majibishano makali yalizuka wakati wajumbe wakiendelea kujadili kanuni zitakazokuwa dira ya kuliongoza bunge hilo maalum, ambalo linaketi pale “mjengoni” kwenye ukumbi wa Bunge la Tanzania mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho, alilazimika kuliahirisha bunge hilo kwa takriban masaa manne, baada ya sintofahamu iliyohanikiza ukumbi huo unaochukua takriban watu 700.

Malumbano hayo yalikuwa ni kati ya wajumbe na mwenyekiti wakati mwingine wajumbe kwa wajumbe, picha kadhaa zilizopigwa na waandishi wa habari wakati sakata hilo likiendelea, zinaonyesha, wajumbe kama vile, Christopher Ole Sendeka, Waziri wa sheria na katiba wa Zanzibar, Abubakar Khamisi Bakari,Moses Machali na wajumbe wengine kadhaa, wakitoa maneno makali dhidi yao wao wenyewe na wakati mwingine wakimtuhumu mzee Kificho kwa upendeleo.

Baadhi ya wajumbe wa bunge hilo, kama Halima Mdee, kuna wakati alionekana akiwa ameshikwa na butwaa asiamini kinachoendelea ukumbini.

Kasheshe hizo zinajiri huku wajumbe hao wakiwa hata kuapishwa bado, na wachambuzi wa mambo wanabashiri kuwa hata mpango wa Ikulu wa kutaka hotuba ya uzinduzi wa bunge hilo kufanyika wiki hii huenda usifanikiwe kwani hata uchaguzi wa mwenyekiti bado kufanyika na kazi ya kuapisha wajumbe hao zaidi ya 600 huenda ikachukua hadi siku tatu.


Hebu muone uyu naye.....

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda(Katikati) na wazito wengine, wakimsikiliza Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila baada ya kutokea kizaa zaa

Wajumbe wa bunge maalum la Katiba, wakitoka ukumbini baada ya kuahirishwa kwa muda kufuatia sintofahamu iliyotokea

Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari..
KAZI IPO KWA KWELI KAMA MAMBO YENYEWE NDIO HAYA