Ijumaa, 13 Septemba 2013

Padre Mwang'amba wa Kanisa Katoliki Zanzibar kamwagiwa tindikali huko Mlandege katika cafe ya Sun Shine.



kisiwa cha zanzibar

Polisi huko visiwani Zanzibar wanachunguza tukio la kasisi wa kanisa katoliki kushambuliwa kwa tindikali.
Imeelezwa kuwa Kasisi huyo Anselmo Mwang'amba, alimwagiwa tindikali akitoka mgahawa mmoja wa kutumia mtandao mjini Zanzibar. Tukio hilo linatokea ndani ya mwezi mmoja tangu wasichana wawili wa kiingereza kushambuliwa.
Hili ni janga jingine kwa Zanzibar ambayo imekuwa ikizongwa na matukio ya aina hii kwa muda sasa.
Mkurugenzi wa upelelezi wa Zanzibar, Yusufu Ilembo ameieleza BBC kuwa bado hawajakamata mtu yoyote kuhusika na tukio hilo ingawa amethibitisha kuwa uchunguzi tayari umeanza.
Ameeleza kuwa Kasisi Mwang'amba aliungua usoni na mabegani na kwamba anaendelea kutibiwa.
Katika miaka ya karibuni Zanzibar imekabiliwa na mikasa ya watu kushambuliwa hivi na kuzua hisia kuwa chuki za kidini.
Mapema mwaka huu kasisi mwingine wa kanisa katoliki alishambuliwa kwa risasi na kuuawa.
Mwezi uliopita Zanzibar ilitikisika kutokana na wasichana wawili wangereza kushambuliwa kwa tindikali na watu wasiojulikana.
Kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu pia alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.

Cape Verde yaadhibiwa na FIFA


Kikosi cha Cape Verde hakitashiriki mchuano wa kombe la dunia mwaka 2014
 
Cape Verde imebanduliwa nje ya kinyanganyiro cha kufuzu kwa dimba la dunia Mwakani kwa nchi za Afrika.
Kwa mujibu wa tovuti ya shirikisho la soka duniani FIFA, Cape Verde ilikosea kwakumshirikisha mchezaji aliyekuwa amepigwa marufuku katika mechi yao dhidi ya Tunisia Jumamosi iliyopita
Kwa mujibu wa FIFA Fernando Verela hakufaa kucheza katika mechi hiyo waliyoshinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Tunisia . FIFA sasa imebadilisha matokeo hayo na kuipa Tunisia ushindi mkubwa wa mabao 3-0 .
Cape Verde ilipo kundi B ilikuwa inaongozwa na Tunisia kama inavyoonekana hapa chini.
Kundi B
Tunisia - 14
Cape Verde - 9
Sierra Leone - 8
Eq Guinea - 2
Kauli hiyo imeipa Tunisia alama za kutosha kuipiku Cape Verde kutoka kileleni mwa kundi B ikiwa na alama 14 .Cape Verde ni ya pili na alama 14.
Shirikisho la soka la Cape Verde lilimetozwa faini ya dola $ 6400 .

UNHCR - Tanzania haijawafukuza wakimbizi


wahamiaji haramu wahamishwa TZ sio wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, ofisi ya Tanzania limekanusha taarifa katika baadhi ya vyombo vya habari kwamba, Tanzania imewarejesha nyumbani kwa nguvu, wakimbizi 25,000 wa Burundi mwezi mmoja uliopita.

MWANAMKE AMCHOMA MOTO MWANAUME ALIYEMBAKA



 Mwanamke mmoja aliyebakwa alikuwa anaact kama anataka kumsamehe mwanaume aliyembaka miezi michache iliyopita akiwa amemtishia kisu.Mwanamke huyo aliamua kumkaribisha nyumbani kwake ili wafahamiane vizuri na pia wajadiliane maamuzi kuhusu kesi yao ya ubakaji nje ya maamuzi ya mahakama.

 Habari zilizokusanywa na Reportghananews.com zinasema kuwa,mwanaume huyo alipofika tu,mwanamke (aliyebakwa) alimpa sehemu ya kukaa alafu akamwambia kwamba anaenda kumwandalia chakula,ila alikuwa na kisasi akilini mwake.
Mwanamke huyo aliyebakwa alipanga na kaka zake kumpa fundisho mbakaji huyo.  
Kwa msaada wa kaka zake alimmwagia mafuta ya taa mbakaji huyo na kumchoma moto.

‘Changudoa’, ombaomba 200 wakamatwa Dar


Mgambo wa Jiji wakiwateremsha ombaomba kwenye gari baada ya kuwakamata katika operesheni maalumu Dar es Salaam jana na kuwafikisha kwenye Mahakama ya Jiji ambapo walisomewa shtaka la uzururaji

Ombaomba zaidi ya 200 na wasichana wanaofanya biashara ya ngono maarufu kama ‘dada poa’  usiku wa kuamkia jana walikamatwa kwenye operesheni maalumu ya kuwaondoa katika maeneo mbalimbali ya jiji,iliyofanywa kwa ushirikiano wa Polisi na askari wa jiji.
Ombaomba na kinadada hao walikamatwa kwenye