Jumatatu, 23 Septemba 2013

hali bado ni mbaya sana huko Kenya


Jengo la Wastgate likifuka moshi
 
vikosi vya usalama vyaingia

JAMAA WANAOITIKISA KENYA NDIYO HAWA HAPA


 Wapiganaji wa Al Shabaab 
Hizi ni silaha za Al Shabaab walizonasa wanajeshi wa AU
Kundi la wapiganaji wa kisomali la al-Shabaab,limevamia jumba la kifahari lenye maduka na mikahawa nchini Kenya. Al Shabaab lenya mizizi yake nchini Somalia, limeweza kuondolewa kutoka miji mikubwa ya Somalia ikiwemo Mogadishu na sehemu zengine za Somalia , ingawa bado linasalia kuwa tisho kubwa kwa kanda nzima.

Raisi wa Kenya Uhuru Kenyata amewaomba wakenya kuwa watulivu

Raisi wa Kenya uhuru kenyata amewaomba wakenya kuwa watulivu wakati Huu   ambapo vikosi vya usalama vinafanya jitihada kuhakikisha watu waliobaki kaitka jengo la WEST GATE wanaokolewa huku akisisitiza kuwa serikli yake itapambana na magaidi popote pale walipo.
Rais Kenyatta ametoa kauli hiyo  wakati akihutubia taifa jana  juu ya tukio la kuuwawa kwa watu wapatao 68 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa,ambapo alitoa hotuba hiyo  mbele ya ya viongozi mbalimbali  wa kisiasa akiwemo aliekuwa waziri mkuu wan chi hiyo  raila odinga. Aidha rais uhuru kenyatta amesema vita hii  haihusu dini yoyote wala kabila lolote bali ni vita ya ugaidi.
Tukio hilo limetokea tangu jumamosi sept 21 ambapo mpaka sasa bado kuna watu wameshikiliwa na wavamizi hao ndani ya jengo hilo la WEST GATE MALL lakini serikali ya kenya imewahakikishia wananchi kuwa inafanya jitihada zote kuwaokoa watu walioko ndani ya jengo hilo.
 
Askari wa Kenya wakiwa katika harakati za uokoaji

KENYA BADO HALI NI MBAYA MAUAJI BADO YANAENDELEA


 


Jeshi la Kenya linasema kuwa limedhibiti jengo hilo ingawa hali bado ni mbaya
 
Wakenya waliofanikiwa kuondoka katika jengo la Westgate kwa usaidizi wa polisi

Huku hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa katika jengo la Westgate lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika ndani ya jengo hilo lenye maduka na mikahawa zaidi ya themanini.
Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani. Walikuwemo ndani ya jengo wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.

Jumapili, 22 Septemba 2013

Al Shabaab walivyolipiza kisasi Kenya


ASKALI AKIWA MAKINI KULINDA AMANI KENYA
 
VIKOSI VYA UOKOAJI VIKIOKOA MAJERUHI HAPO KENYA
RAIA WA KENYA WAKIWA HAWAAMINI KILICHOWAKUTA
 
Taharuki ilianza saa saba mchana Jumamosi baada ya watu wanaokisiwa kuwa kumi kuvamia duka kubwa la Nakumat ndani ya jengo la kifahari la Westgate
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/21/130921184536_kenya_attack_976x549_bbc_nocredit.jpg
Baadhi walifanikiwa kunusurika kifo kwa usaidizi wa polisi waliofika mara moja kuanza kukabiliana na washambuliaji 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/22/130922064442_kenya_nairobi_attack_976x549_reuters.jpg
Hali ya usalama imeweza kudhibitiwa , eneo lililoshambuliwa limezingirwa na wanajeshi wakisaidiwa na polisi na watu wlaifika kuwatafuta jamaa zao wamezuiwa. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/21/130921191328_kenya_attack_976x549_bbc_nocredit.jpg
Polisi waliweza kufika mara moja katika eneo la shambulio kukabiliana na wapiganaji ambao idadi yao kamili haijaweza kusemwa
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/21/130921184854_kenya_attack_976x549_bbc_nocredit.jpg
Polisi wakiwa katika harakati za kuwaokoa baadhi ya wakenya waliokuwemo ndani ya jengo hilo 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/21/130921184215_kenya_attack_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Washambuliaji wa kundi la kigaidi la Al Shabaab walivamia jengo hilo na kuwapiga risasi kiholela watu waliokuwemo
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/22/130922070703_kenya_nairobi_attack_976x549_reuters.jpg 
Baadhi ya manusura waliofanikiwa kuokolewa kutoka katika jengo la Westgate
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/22/130922064604_kenya_nairobi_attack_976x549_reuters.jpg 
Kikosi cha wanajeshi wa KDF wanasema kuwa wanafanya kila hali kuhakikisha kuwa wanamgambo walio ndani ya jengo hilo hatimaye wattaweza kukamatwa
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/21/130921185007_kenya_attack_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Hali ilikuwa mbaya kwani washambuliaji waliwapiga risasi kiholela wakenya waliokuwa ndani ya jengo hilo na hawa wanaonekana kukimbilia usalama wao