Ijumaa, 1 Novemba 2013

LIGI KUU TANZANIA BARA YAINGIA DOSARI NI BAADA YA MASHABIKI WA SIMBA KULETA VURUGU UWANJANI

 
Kikosi cha Klabu ya Simba ya Tanzania

Polisi jijini Dar es Salaam Tanzania wamelazimika kutumia Mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki wa Klabu ya Simba,baada ya kumalizika mechi ya Ligi kuu soka Tanzania bara siku ya Alhamis ambapo Simba ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Kagera Sugar.
Vurugu hizo zimezuka mwishoni mwa mechi ambayo timu ya Simba imezidi kuporomoka hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo kufuatia matokeo ya sare ya bao 1-1.
Baada ya Simba kuongoza bao 1 hadi dakika ya 90 Kagera Sugar waliposawazisha kwa Penati iliyotiwa kimiani na beki wa zamani wa Simba Salum Kanoni ambapo mashabiki wanaoaminika kuwa wa Simba walianza kung'oa viti uwanjani hali iliyosababisha askari polisi kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya mashabiki hao.
Simba ilianza kuliona lango la Kagera Sugar katika dakika ya 45 baada ya mshambuliaji raia wa Burundi Amis Tambwe kufunga bao la kwanza lililodumu hadi mapumziko.
Katika Kipindi cha pili Simba walianza kucheza kwa kujihami hali iliyosababishga Kagera kukaribia lango lao mara kwa mara na hatimaye wakafanikiwa kusawazisha katika dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo Simba imeporomoka hadi nafasi ya nne wakiwa na pointi 21,huku Azam, wakishika nafasi ya kwanza kwa kuwa na pointi 23 sawa na Mbeya City lakini wakitofautiana kwa magoli ya kufunga.
Yanga ni ya tatu kwa kuwa na pointi 22.

UHABA WA CHAKULA KWENYE KAMBI ZA WAKIMBIZI HURUMA

DADAAB NA KAKUMA ZAKUMBWA KWA KIASI KIKUBWA
 
Dadaab ndio kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani 

Shirika la chakula duniani WFP pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi (NHCR) yametangaza kuwa kuanzia tarehe moja mwezi Novemba, shirika la WFP litalazimika kupunguza kiwango cha chakula ambacho kinatolewa kwa wakimbizi zaidi ya nusu milioni wanaoishi katika kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma.
Hali hii kwa mujibu wa mashirika hayo inatokana na WFP kukosa rasilimali za kutosha kuendesha shughuli zake za kuwalisha wakimbizi katika kambi hizo.
"tumefanya kila tuwezalo kujaribu kuzuia hili , lakini imetulazimisha kupunguza kiwango cha chakula tunachotoa kwa wakimbizi hao kwa asilimia 20, kuanzia mwezi Novemba na Disemba ili tuweze kuhakikisha hifadhi yetu ya chakula itatumika hadi mwishoni mwa mwaka,’’ shirika la habari la Reuters lilimnukuu Ronald Sibanda mkuu wa shirika la WFP nchini Kenya.
"Tunatumai kuwa hali hii itakuwa tu ya muda huku tukiwaomba wahisani wetu kuja kuwasaidia mamia ya wakimbizi wanaotegemea msaada wa chakula wa WPF ili kukimu mahijati yao,’’ aliongeza kusema bwana Sibanda.
Shirika hilo linahitaji dola milioni kumi kila mwezi ili kutoa chakula karibu tani elfu kumi kwa wakimbizi katika kambi hizo mbili zilizoko Kaskazini mwa Kenya.
Hata hivyo chakula kilichoko sasa kinaweza kutosheleza wakimbizi 535,000 walio kwenye kambi hadi mwishoni mwa mwaka na huenda wakapunguza chakula hicho zaidi ikiwa shirika hilo halitapata msaada zaidi.
Bwana Sibanda amesema kuwa anaamini jamii ya kimataifa inaelewa umuhimu wa mpango wao kuwasaidia wakimbizi katika kambi za Dadaab na Kakuma na kwamba wana wasiwasi kuwa kupuguka kwa msaada wa chakula kwa wakimbizi ni jambo litakalokuwa na atahri kubwa sana.
Mpango wa WFP kuwasaidia wakimbizi nchini Kenya umekumbwa na changamoto nyingi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Mchango wa Marekani wa dola milioni ishirini unatarajiwa kutolewa mwezi Machi mwaka 2014 lakini shirika hilo litahitaji dola milioni ishirini kuendelea na shughuli zake kati ya mwezi Januari na Februari kuhakikisha kuwa wakimbizi wanapata lishe bora na chakula kwa ujumla kwani wengi wao hawana chanzo kingine cha chakula.

Alhamisi, 31 Oktoba 2013

MIILI 87 YA WAHAMIAJI YAPATIKANA JANGWANI

 
Jangwa la Sahara
Waokozi nchini Niger wanasema kuwa wamepata miili 87 ya watu waliofariki baada ya magari yao kuharibika walipokuwa wanajaribu kuvuka jangwa la Sahara.
Mmoja wa waliokuwa wanaendesha shughuli ya ukozi Almoustapha Alhacen, alisema kuwa miili yao ilikuwa katika hali mbaya ya kuharibika na kuwa ilikuwa imeliwa sehemu moja na wanyama pori.
Miili hiyo inaaminika kuwa ya wafanyakazi wahamiaji na familia zao. Wengi walikuwa wanawake na watoto.
Niger ni kivukio kikubwa cha wahamiaji wanaokuwa safarini kufika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuelekea Ulaya.
Lakini wengi wa wanaofanikiwa kukamilisha safari hiyo huishia kufanya kazi katika mataifa ya Afrika Kaskazini.
Kulingana na Bwana Alhacen, moja ya magari ambayo wahamiaji hao walikuwa wanatumia kwa usafiri, liliharibika walipotoka mji wa Arlit mwishoni mwa mwezi Septemba, au mwanzoni mwa Oktoba.
Maafisa wa usalama pia wamesema kuwa gari la pili liliharibika lilipokuwa njiani kurejea Arlit ili kutengenezwa.
Inaonekana kuwa miongomi mwa wasafiri hao takriban watu 10 walisafari kurejea Arlit na kutoa taarifa ya wenzao kukwama jangwani.
Iliarifiwa kuwa miili mitano ilipatikana.
Mnamo siku ya Jumatano, wafanyakazi wa kujitolea pamoja na wanajeshi, walipokuwa wanawatafuta wahamiaji hao, wakafanikiwa kupata maiti zaidi umbali wa kilomita 10 kutoka katika mpaka wa Algeria.
Kati ya maiti 48 waliopatikana, kulikuwa na miiili ya watoto na vijana na Alhacen alisema kuwa walikuwa wanaelekea nchini Algeria kutafuta vibarua vya mishahara midogo sana.
Akizungumza kutoka katika kiwanda cha kuchimba madini ya Uranium, Kaskazini mwa Agadez, aliambia BBC kuwa hiyo ndiyo iliuwa siku mbaya kwake baada maishani mwake baada ya kupata miili hiyo.

Jumatano, 30 Oktoba 2013

11 WAFARIKI KWENYE AJALI YA TRENI NAIROBI HIVI PUNDE

 
Watu 11 wamethibitishwa kufariki katika ajali iliyohusisha treni na basi iliyokuwa imewabeba watu wakielekea kazini katika mtaa wa Umoja viungani mwa mji wa Nairobi.

Basi hiyo inayoaminika kuwa na watu 34 iligongwa na treni kwenye njia ya reli kuelekea mjini. Kwa mujibu wa shirika la Red Cross, idadi ya majeruhi imefika 34 na wamepelekwa katika hospitali kuu ya Kenyatta.

Baadhi ya waliojeruhiwa wanasemekana kuwa katika hali mbaya.

Walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa basi hilo lilisukumwa umbali wa mita hamsini baada ya kugongwa kwa upande.

Inaarifiwa watu sita walifariki papo hapo na wengine wawili kufariki baadaye kutokana na majeraha waliyoyapata.

Wengine wengi wamejeruhiwa kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu.

Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP aliyeshuhudia ajali hiyo alisema kuwa basi iliharibiwa vibaya baada ya kugongwa kwa upande na treni ihiyo ilikuwa inasafiri kwa kasi kubwa.

Ajali hiyo imetokea asubuhi wakati wa msongamano wa watu na magari huku watu wengi wakiwa katika haraka kuu kuelekea kazini

UTANI WA SIMBA NA YANGA SASA WAHAMIA MBEYA CITY NA TANZANIA PRISON...! ONA JINSI UWANJA WA SOKOINE MBEYA ULIVYCHAFUKA HAPO JANA TAR.29/10/2013

 JUKWAA LA MASHABIKI NA WAPENZI WA MBEYA CITY













 WACHEZAJI WAKISHANGILIA GOLI LAO LA KWANZA







 ANGALIA PENALTY HIYO INAPIGWA NA DEOGRATIUS JULIUS
















MASHABIKI WA MBEYA CITY WAKIWA WAMEBEBA JENEZA







 KAMA KAWAIDA YA TIMU HII MWISHO WA MCHEZO HUWA INAPENDA KUTOA SHUKRANI KWA MASHABIKI WAO







 HADI MWISHO WA MCHEZO MBEYA CITY 2-O PRISON

PICHA ZOTE NA FREE MEDIA TO BLOGS