Alhamisi, 21 Novemba 2013

MWATHIRIWA WA UBAKAJI AKAMATWA SOMALIA

 
Sio mara ya kwanza kwa mwathiriwa wa ubakaji kukamatwa baada ya kusimulia yaliomkumba Somalia
Msichana mmoja amekamatwa mjini Mogadishu Somalia, baada ya kusimulia kituo kimoja cha redio nchini humo kuhusu alivyobakwa na watu waliomtishia kwa bunduki.
Mwandishi aliyemhoji msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 pia amezuiliwa.
Umoja wa Mataifa unataka uchunguzi ufanywe kuhusu madai hayo ukiwema kuwa unapiga darubini uhuru wa vyommbo vya habari na ambavyo serikali itachunguza kisa hiki.
Serikali ya Somalia inasema kuwa lazima haki itendeke.
Mapema mwaka huu , mwathiriwa mmoja wa ubakaji pamoja na mwandishi wa habari walifungwa jela mwaka mmoja ingawa waliachiliwa baadaye kutokana na uamuzi wa kesi ya rufaa.
Ubakaji na waandishi wa habari wanaoripoti visa vya ubakaji au dhuluma nyinginezo za kingono, ni mada ambayo huhofiwa kuzungumziwa nchini Somalia na kesi hii ndio ya hivi karubui kuhusu polisi kumkamata mwathiri wa ubakaji pamoja na mwandishi habari aliyemhoji.
Msichana huyo aliambia kituo cha redio cha Shabelle, kuwa alibakwa na waandishi habari wenzake wawili wakiwa akiwa ameshikiliwa bunduki.
"mmoja alinitishia kwa bunduki na kunipeleka chumbani kwa nguvu , na kunivamia huku akinivunjia heshima yangu, '' msichana huyo alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema katika video kwenye mtandao wa Redio Shabelle.
"ninaomba serikali kuchukua hatua dhidi ya wabakaji hawa, huenda wamewatendea unyama huu wasichana wengine wasio na uwezo wa kujitetea,'' alisema msichana huyo.
Video hiyo imepeperushwa kwenye mitandao mingine ya habari nchini humo.
Polisi walimkamata mwanamke huyo pamoja na mwandishi wa habari Mohamed Bashir Hashi, aliyemhoji pamoja na mkuu wa idhaa ya Redio Shabelle Abdulmalik Yusuf.
Hakuna hata mshukiwa mmoja, aliyetuhumiwa amechukuliwa hatua za kisheria.
Hata hivyo serikali ya Somalia imesema kuwa ubakaji na dhuluma dhidi ya wanawake ni mambo ambayo hayaruhusiwi hata kidogo, ingawa haikutamka chochote kuhusiana na kesi hii.
 

MAGAZETI YA LEO 21.11.2013

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Jumatano, 20 Novemba 2013

HIVI NDIVYO MAUAJI YA WATU YALIVYOTOKEA KATIKA NGOME YA HEZBOLLAR

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115932_blast_afp-1.jpg 
Takriban watu 22 wameripotiwa kufariki katika milipuko miwili ambayo ililenga ubalozi wa Iran mjini Beirut, mji mkuu wa Lebanon
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115934_blast_afp-2.jpg
Afisaa mmoja mkuu katika ubalozi huo Ebrahim Ansari alikuwa miongoni mwa waliofariki. Maafisa wamesema kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115936_blast_ap-3.jpg
Picha nyingi za mashambulizi hayo zilionyesha magari yakiteketea pamoja na miili ya watu ikiwa imetapakaa kwenye barabara za eneo hilo. Majumba pia yaliharibiwa vibaya
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115938_blast_ap-4.jpg
Iran inaunga mkono kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Hezbollah ambalo limewapeleka wapiganaji nchini Syria kuunga mkono serikali ya Rais Bashar al Assad. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115940_blast_afp-5.jpg
Duru zinasema kuwa moja ya milipuko hio, ilisababishwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga, wakati shambulio la pili lilitokana na bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115942_blast_reuters-6.jpg
Shirika la habari la Reuters linanukuu kituo cha televisheni cha CCTV, kikionyesha mwanamume mmoja akikimbia kutoka katika ubalozi wa Iran na kisha kujilipua
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115944_blast_reuters-7.jpg
Balozi wa Iran nchini Beirut alithibitisha kifo cha bwana Ansari, ingawa haijulikani ikiwa alikuwa ndani ya ubalozi au katika jengo jirani 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115946_blast_ap-8.jpg
Syria imelaani vikali mashambulizi hayo. Mgogoro wa kisiasa nchini Syria umechochea kuongezeka kwa hali ya wasiwasi nchini Lebanon.

Jumanne, 19 Novemba 2013

MASHINE ZA TRA ZAZUA BALAA DSM

 
HAWA NI BAADHI YA WANANCHI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAKIANDAMANA 
 
KUPINGA AMRI YA TRA KUWATAKA WANUNUE MSHINE ZA KI-ELECTRONIC NA 
 
KUZITUMIA KWA SHUGHULI ZA KIBIASHARA

OFISI YA HABARI YASHAMBULIWA JIJINI PARIS UFARANSA

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/18/131118144201_paris-6.jpg 
Msako umeanza mjini Paris Ufaransa, baada ya mtu aliyekuwa amejihami kushambulia ofisi za za vyombo vya habari  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/18/131118144204_paris-7.jpg 
 Mpiga picha mwenye umri wa miaka 27, alijeruhiwa vibaya katika jengo hili la Liberation na dereva mmoja alilazimika kupitia eneo la Champs Elysees kabla ya kuruhisiwa kupita
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/18/131118144207_paris-8.jpg
Polisi wanaendelea na uchunguzi wao, huku ulinzi ukiwa umedhibitiwa katika ofisi za vyombo vya habari. Polisi wanamsaka mwanamume aliyevamia ofisi kituo cha televisheni cha BFMTV mnamo siku ya Ijumaa. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/18/131118144211_paris-9.jpg
Mshambuliaji alivamia ofisi hiyo mjini Paris na kuanza kushambulia watu kwa bunduki
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/18/131118144209_paris-10.jpg
Polisi sasa wako nje ya ofisi kuu za vyombo vya habari kushika doria mjini Paris
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/18/131118144214_paris-11.jpg
Vyombo vya habari mjini Paris vinasema kuwa mtu huyo aliyekuwa amejihami na kumteka nyara dereva mmoja alimwambia kuwa alikuwa amejihami kwa maguruneti
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/18/131118144217_paris-12.jpg
Kulikuwa na hofu kuwa mwanamume huyo alikuwa anaelekea katika jengo refuu zaidi mjini Paris la Eiffel
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/18/131118144219_paris-13.jpg
Watu wametakiwa kukaa majumbani mwao. Hata hivyo wanasema kuwa mshukiwa ametulia 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/18/131118144221_paris-14.jpg
Maafisa wakuu wakiwemo Waziri wa mambo ya ndani Manuel Valls, alizuru ofisi za Liberation baada ya shambulizi