Ijumaa, 27 Desemba 2013
HABARI PICHA...!
Jumatano, 25 Desemba 2013
WAKATI NYIE MNAKULA NA KUSHEREKEA SIKUKUU YA CHRISMAS ONA WENENU SUDANI KUSINI
Huku Umoja wa Mataifa ukijiandaa kutuma maelfu ya
wanajeshi zaidi wa kutunza amani Sudan Kusini, viongozi wa jamii ya
kimataifa wanaendelea kutoa wito wa kusitishwa mapigano yanayoendelea
nchini humo.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry,
ametoa wito kwa rais wa Sudan Kusini, Salva Kirr, na aliyekuwa makamo
wake, Salva Kirr, kuanzisha mazungumzo ya amani.Uchina pia imetoa wito kuwa mapigano yasitishwe.
Kuna taarifa kwamba kumetokea mapambano Malakal, mji mkuu wa jimbo la mafuta la Upper Nile state.
Wanajeshi wa serikali wanasema wameukomboa mji muhimu wa Bor.
Mwandishi wa BBC anasema haikuelekea kuwa ghasia zitamalizika karibuni - ghasia zilizozidisha uhasama wa kikabila na kupelekea maelfu kuhama makwao.
Jumanne, 24 Desemba 2013
HALI HII SUDANI KUSINI MPAKA LINI? MAUAJI KILA KONA
Waathirika wa mapigano Sudan Kusini
Taarifa mpya zimeibuka zikieleza
kuwepo kwa mauaji ya kikabila yaliyofanyika katika kipindi cha zaidi ya
wiki moja ya ghasia nchini Sudan Kusini.
Mwandishi wa habari mmoja kutoka mji mkuu wa
Sudan Kusini, Juba, amewakariri watu walioshuhudia mauaji hayo wakisema
zaidi ya watu 200, wengi wao wakitoka kabila la Nuer , wameuawa kwa
kupigwa risasi na majeshi ya usalama.Mtu mwingine kutoka Juba amesema watu wenye silaha kutoka kabila la Dinka walikuwa wakiwashambulia kwa risasi watu kutoka maeneo ya Nuer.
Ghasia hizo zimekuja huku kukiwa na hali ya kugombea madaraka kati ya Rais Salva Kiir, kutoka kabila la Dinka, na aliyekuwa naibu wake Riek Machar kutoka kabila la Nuer.
Serikali ya Sudan Kusini imekanusha kuhusika na ghasia za kikabila.
Taarifa hizo zimekuja wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza askari 5,500 wa Umoja wa Mataifa katika kikosi cha askari 7,000 wa Umoja wa Mataifa waliopo Sudan Kusini.
Waasi wanaomuunga mkono makamu wa rais aliyefukuzwa Riek Machar walitwaa miji mikubwa wiki iliyopita.
Maelfu ya watu wamekimbia mapigano.
MLIPUKO WAPIGA JENGO LA USALAMA MISRI
Mlipuko waharibu sehemu ya jengo la usalama Misri
Mlipuko mkubwa katika jengo moja la usalama kaskazini mwa Misri umesababisha watu wapatao 14 kuuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa.
Maafisa nchini humo pamoja na vyombo vya habari
vya serikali wamesema, mlipuko huo, ambao umeripotiwa kusababishwa na
bomu lililotegwa katika gari, umesababisha kuporomoka sehemu ya jengo
hilo katika mji wa Mansoura.Waziri Mkuu wa Mpito Hazem Beblawi ameelezea tukio hilo kama "kitendo cha ugaidi".
Mashambulio dhidi ya majeshi ya usalama na polisi nchini Misri yameongezeka tangu jeshi nchini humo limtoe madarakani rais wa Kiislam Mohammed Morsi mwezi Julai, 2013.
Mpaka sasa hakuna kikundi kilichodai kuhusika na shambulio hilo.
Bwana Beblawi amekiambia kituo cha televisheni cha ONTV: "Serikali itafanya kila iwezalo kuwasaka wahalifu wote waaliotekeleza, kupanga na kusaidia kufanyika kwa shambulio hilo."
Athari za mlipuko huo zilipatika katika maeneo ya umbali wa kilomita 20 kutoka eneo la tukio.
Televisheni ya Misri imewaomba watazamaji wake kwenda hospitali kutoa damu.
Kikundi cha Muslim Brotherhood - kinachomuunga mkono Bwana Morsi na kilichopigwa marufuku na serikali ya mpito ya Misri, kimelaani shambulio hilo.
"Muslim Brotherhood kinachukulia kitendo hiki kama shambulio la moja kwa moja katika umoja wa watu wa Misri," kimesema katika taarifa yake.
Mkuu wa usalama amejeruhiwa'
Mlipuko huo ulipiga jengo hilo Jumatatu usiku wa manane.Zaidi ya watu 100 walijeruhiwa. Taarifa za vyombo vya habari zinasema mkuu wa usalama wa jimbo ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa.
Mlipuko huo ulivunja vioo vya madirisha ya majengo jirani na athari zake kufika umbali wa kilomita 20 kutoka eneo la tukio.
Mansoura - mji wenye idadi ya watu 480,000 - ni makao makuu ya mkoa wa Dakahliya katika jimbo la Nile Delta.
Tangu kuondolewa madarakani kwa Bwana Morsi - rais wa kwanza wa Misri aliyechaguliwa kwa njia za kidemokrasia - wafuasi wake wamekuwa wakiandaa maandamano makubwa wakitaka kuachiliwa huru kwa kiongozi wao.
Zaidi ya wanachama 2,000 wa Muslim Brotherhood wamekamatwa, na 450 kati yao, siku ya Jumatatu walianza mgomo wa kususia chakula wakipinga kudhalilishwa.".
Bwana Morsi kwa sasa anakabiliwa na kesi tatu tofauti za uhalifu zikihusishwa na nafasi yake akiwa madarakani.
Kesi ya kwanza ilifunguliwa tarehe Novemba, lakini imeahirishwa hadi Januari 8, 2014.
Jumatatu, 23 Desemba 2013
HII NDIYO AJALI YA TRENI ILIYOTOKEA KIBERA HUKO NAIROBI KENYA
Waokozi wana wasiwasi kuwa pengine watu kadha
wamenasa chini ya treni iliyopinduka katika mitaa ya Kibera, Nairobi -
eneo la watu maskini.
Watu kama kumi walijeruhiwa wakati mabehewa mane ya mizigo yalipopinduka juu ya vibanda kando ya njia ya reli.Waokozi wanajaribu kutafuta nafasi katika mtaa wenye nyumba zilizogandana sana, ili kuleta mashini ya kunyanyua mabehewa ili kuwafikia wale walionasa.
Mabehewa yalianguka juu ya vibanda vilivyo karibu na njia ya reli.
Magazeti yanaarifu kuwa kazi za uokozi zimezingika kwa sababu watu wengi wamezonga eneo hilo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)