(PICHA NA RICHARD BUKOS, DENIS MTIMA, MAYASA MARIWATA, SHANI RAMADHANI, HAMIDA HASSAN, IMELDA TARIMO/GPL)
Alhamisi, 29 Mei 2014
TAZAMA MAZISHI YA MSANII WA BONGO MOVIE RECHO, KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM.
Alhamisi, 10 Aprili 2014
HABARI MPYA KWA WATANZANIA WOTE
MAWAKALA WA AJIRA NA KAZI WANAPATIKANA MBEYA, WENYE MAHITAJI MNAKARIBISHWA.
| Meneja wa Kampuni ya New Position Co.Ltd, Juma Burah akizungumza jambo na waandishi wa habari(hawapo pichani) ofisini kwake. |
| Meneja akionesha tangazo la kuthibitishwa kwa kampuni yake na Wizara ya Kazi na Ajira katika gazeti la Mtanzania |
| Meneja aikionesha moja ya mashine ambazo wanahitaji vijana wenye fani ya Mauzo kwa ajili ya kuuza na kusambaza kwa wafanyabiashara. |
| Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwajibika kazini.
KAMPUNI ya New Position Co Ltd, ni
kampuni iliyosajiliwa kisheria chini ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa namba 105407
yenye lengo la kuwaunganisha waajiri na waajiri popote nchini Tanzania.
Kampuni hiyo ni wakala wa ajira na kazi
ambayo kazi yake ni kuwatafutia ajira wahitimu wa ngazi mbali mbali
wanaohangaika kuomba kazi katika mashirika mbali mbali ikiwa ni pamoja na
mashirika au makampuni yanayohitaji wafanyakazi.
Akizungumza na mtandao huu, Meneja wa
Kampuni hiyo, Juma Burah amesema watanzania wengi hawajui jinsi ya kuandika
barua za kuomba kazi pamoja na wasifu wao(CV) jambo lililopelekea kuanzisha
kampuni kwa lengo la kuwakomboa vijana.
Amesema mwombaji wa kazi anapaswa
kupeleka vyeti vyake na shilingi elfu kumi na tano(15,000/=)ambazo zitasaidia
kupewa mafunzo jinsi ya kuandika cv, barua ya maombi pamoja na kujieleza wakati
wa usaili ili muombaji aweze kumudu ushindani uliopo.
Ameongeza kuwa kazi ya kampuni mbali na
kutafuta ajira na kazi pia inaibua fursa za ajira kupitia mtandao ambapo sifa
za muombaji huwekwa mtandaoni ili wenye kuhitaji wafanyakazi huwapata
kiurahisi.
Meneja huyo ameongeza kuwa tangu kusajiliwa
kwa kampuni hiyo imepita miezi sita lakini wamepata mafanikio makubwa kwa
kuwawezesha wafanyakazi zaidi ya 300 kupata mafunzo na kuajiriwa katika sekta
mbali mbali.
Ameongeza kuwa mbali na kampuni
kuwatafutia kazi watu mbali mbali pia Kampuni yenyewe inanafasi 50 za wataalamu
wa fani ya IT, Mauzo na mapokezi.
Kampuni hiyo pia inaubia na kampuni ya
BOLSTO inayohusika na uuzaji wa mashine mbali mbali za Kielectroniki kama vile
EFDs ambazo ziko za aina tofauti tofauti
ambazo ni Prima, Dp25, Best LC, Ultima na Easy Machines inayofanya kazi
ya uwakala wa fedha kama Mpesa, Tigo Pesa, Zuku, Dstv nk.
Amesema pia kampuni hiyo inanafasi 20 za
kazi kwa ajili ya kuuza na kusambaza mashine hizo ambapo muuzaji atanufaika na Kamisheni
kutokana na mauzo ya mashine hizo
Kampuni hiyo inapatikana katika Jengo la
Crdb Ghorofa ya kwanza kushoto au unaweza kupiga simu namba 0718 470499 au kwa
barua pepe info@newposition.com au tembelea
wavuti wao wa www.new-positions.com. Mbeya mjini.
|
Jumatatu, 10 Machi 2014
WAFANYABIASHARA WA MCHANGA NA KOKOTO JIJI LA MBEYA WAJA JUU KUILALAMIKIA WIZAZRA YA NISHATI NA MADINI
Bwana
nidhamu wa wachimbaji na wasafirishaji bidhaa hizo Peter Hezron N’gwavi
amesema kuwa kitendo cha tozo na leseni kitafanya vijana waliojiajiri
kuanza kufanya vitendo vya uhalifu kutokana na ukosefu wa mitaji.
Mkurugenzi
wa Jiji Mussa Zungiza amesema kuwa madai yao hayahusu ofisi yake bali
wenye dhamana ya kujibu kero hizo ni mamlaka husika ambayo ni Wizara ya
Nishati na Madini hivyo atawaomba wawakilishi wao waweze kujibia kero
zao.
Mwanasheria wa jiji akifafanua jambo
Mhandisi
wa Jumanne M. Nkana ambaye ni Afisa Mfawidhi ofisi ndogo ya TMAA Mbeya
amesema kuwa waraka wa kulipia bidhaa za Mchanga,Kokoto na Mawe
ulipitishwa na Bunge Mwaka 2010 ndipo ulipoanza kutumika rasmi kwa tozo
la asilimia 3 kwa bei ya bidhaa iliyopo Sokoni.
Wafanyabiashara
ya Madini ya mchanga,kokoto na mawe Jiji la Mbeya wameandamana kwenda ofisi ya
Mkurugenzi wa Jiji kwa kutumia maroli kupinga waraka wa Wizara ya Nishati na
Madini unaowataka watumiaji wa bidhaa hiyo kulipia shilingi elfu mbili mia tano
kuanzia Machi 3 mwaka huu.
Maandamano
hayo yalipokelewa na Mkurugenzi wa Jiji Mussa Zungiza ofisini kwake ambapo
alikana kutoa waraka huo na kufafanua kuwa waraka huo umetolewa na Wakala wa
Ukaguzi wa Madini[Tanzania Minerals Audit Agency-TMAA].
Akitoa
malalamiko yao mbele ya Mkurugenzi Bwana nidhamu wa wachimbaji na wasafirishaji
bidhaa hizo Peter Hezron N’gwavi amesema kuwa kitendo cha tozo na leseni
kitafanya vijana waliojiajiri kuanza kufanya vitendo vya uhalifu kutokana na
ukosefu wa mitaji.
Mkurugenzi
wa Jiji amesema kuwa madai yao hayahusu ofisi yake bali wenye dhamana ya kujibu
kero hizo ni mamlaka husika ambayo ni Wizara ya Nishati na Madini hivyo
atawaomba wawakilishi wao waweze kujibia kero zao.
Mhandisi wa
Jumanne Mohammed ambaye ni Afisa Mfawidhi ofisi ndogo ya TMAA Mbeya amesema
kuwa waraka wa kulipia bidhaa za Mchanga,Kokoto na Mawe ulipitishwa na Bunge
Mwaka 2010 ndipo ulipoanza kutumika rasmi kwa tozo la asilimia 3 kwa bei ya
bidhaa iliyopo Sokoni.
Hata hivyo
Mohammed amesema kuwa leseni za uchimbaji wa bidhaa za ujenzi hazihusiani na
madereva wanaobeba bidhaa hiyo
hivyo wao wanapobeba bidhaa hizo wanapaswa kupata kibali kuoka kwa mmiliki wa
mgodi wa madini hayo ambapo kibali hicho hutolewa bure katika ofisi yake
iliyopo eneo la Mwanjelwa Jengo la IFAD.
endelea kufuatilia blog hii kwa matukio zaidi
Ijumaa, 7 Machi 2014
HILI NDILO BUNGE LA KATIBA LA TANZANIA
TUKIO KATIKA PICHA: TAZAMA WABUNGE WALIVYOPIGWA BUTWAA JANA KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA
| Halima Mdee akibadilisha style za "mishangao" wakati "Sinema" ya bure ikiendelea |
![]() |
| Mbuneg MosesMachali |
![]() |
| Christophe Ole Sendeka, naye hakuwa nyuma kwenye "sheshelumbe" la Jana Alhamisi Machi 6, 2014 |
![]() |
| Hebu muone uyu naye..... |
| Waziri Mkuu, Mizengo Pinda(Katikati) na wazito wengine, wakimsikiliza Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila baada ya kutokea kizaa zaa |
| Wajumbe wa bunge maalum la Katiba, wakitoka ukumbini baada ya kuahirishwa kwa muda kufuatia sintofahamu iliyotokea |
![]() |
| Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari.. KAZI IPO KWA KWELI KAMA MAMBO YENYEWE NDIO HAYA |
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)




