Jumapili, 13 Julai 2014
HII NI ZAIDI YA UJUAVYO....UGONJWA WA EBOLA NI JANGA KWA AFRIKA HASA MAGHARIBI
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetaka "hatua za dharura" zichukuliwe
ili kudhibiti kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola Africa magharibi, ambao
umewauwa zaidi ya watu 400. Ugonjwa huu ndio mkubwa zaidi duniani kuzuka
kutokana na visa vyake, vifo na kusambaa katika maeneo.
Kumekuwepo na visa visivyopungua 600 nchini Guinea - ambapo ugonjwa huo
ulianza kuzuka miezi minne iliyopita mjini Guekedou, ambao ulikuwa kituo
kikubwa cha biashara, kilichowavutia wauzaji na wanunuzi kutoka mataifa
kadhaa.
Shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres (MSF) tayari limeonya
kuwa kusambaa kwa ebola hakuwezi kudhibitiwa. Shirika hilo lina
wafanyikazi 300 wa kimataifa na vile vile wa kitaifa wanaofanya kazi
nchini Guinea, Sierra Leone pamoja na Liberia, ambako ugonjwa huo
unaenea kwa kasi. Mataifa mengine yako
macho iwapo ugonjwa huo utasambaa
Zaidi.
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Ebola ni ugonjwa unaosababishwa
na virusi na ambao dalili zake za mwanzo huweza kuwa kushikwa na homa,
kuwa dhaifu, kuumwa na misuli na kuumwa na koo. Na huo ni mwanzo tu:
kile kinachofuata ni kutapika, kuendesha na -wakati mwingine- kuvuja
damu.
Virusi hivyo huenea kwa haraka sana, na hadi sasa hakuna dawa
inayotambulika kuweza kuvitibu, kwa hivyo wanaotoa huduma za matibabu
huvalia mavazi yanayowakinga kutokana na kuambukizwa kwa ugonjwa huo.
Kulingana na uzito wa athari za ugonjwa huo, hadi kufikia asilimia 90 ya
walioambukizwa huaga dunia. Anayehakikisha usafi anawakaribia wagonjwa
wanaosubiri matokeo baada ya kupimwa damu.
Vipimo vya maabara vitaonyesha kwa saa kadhaa iwapo sampuli ya damu inayopimwa ina virusi vya Ebola au la.
Baada ya kukumbana na virusi hivyo katika sehemu iliyotengwa, mavazi na viatu husafishwa kwa Chlorine.
Kando na kutoa huduma za kliniki, kikundi hicho hutoa hamasisho kuhusu
ugonjwa huo. Hapa Touloubengo, familia tano ambazo nyumba zao zilikuwa
zimesafishwa siku kadhaa zilizopita kutokana na kuaga dunia kwa mmoja
wao wanakabidhiwa magodoro.
Sio kila mtu aliye salama. Hapa familia ya Kinda Marie Kamano, akiwemo
dadake (katikati), pamoja na wanajamii wengine wanahuzunika katika
mazishi yake karibu na nyumba yake.
Takriban watu 600 wamefariki kutokana na homa ya Ebola Afrika Magharibi
Endelea kufuatilia
Jumamosi, 12 Julai 2014
Duniani kote tunatakiwa kuomba amani ilejee
Miili ya Wapalestina waliouawa kwa mashambulizi yanayofanywa na Israel
Umoja wa Mataifa umesema robo
tatu ya Wapalestina waliouawa kwa mashambulizi ya ndege yanayoendelea
yanayofanywa na Israel huko Gaza ni raia wa kawaida.
Maafisa wa Palestina wanasema raia mia moja ishirini wameuwawa tangu mashambulio kuanza.
Magari ya deraya yakiwa vitani
Israel imesema inafanya mashambulio hayo, ili
kujaribu kuwazuia wapiganaji wa Hamas, ambao wamekuwa wakirusha mamia ya
makomborakwenye ardhi ya Israel.
Israel inalaumu wapiganaji wa Hamas kwa kutumia raia kama ngao kwa kuweka vifaa vya kivita kwenye makazi ya watu.
Professor Manuel Hassassian mwakilishi wa
Palestina nchini Uingereza, ameiambia BBC, Israel kwa kuwalenga Hamas
hukutakwepa kuwadhuru raia.
Alisema idadi kubwa ya raia wamekufa siyo sababu Hamas inajificha kati ya raia, yaani inawatumia raia kama kinga.
Gaza, kwa hivo wanapowalenga Hamas
kamawanavosema, wanawalenga wa-Palestina wote. Siyo Gaza peke
yake.Katika Ufukwe wa Magharibi piya, Israil imekuwa ikiwauwa kiholela,
na huko hakuna makombora yaliyolegwa dhidi ya Israil" Alisema
Hassassian.
Alhamisi, 10 Julai 2014
HII NI ZAIDI YA MVUA YA MAGOLI: KICHAPO KWA TIMU YA BRAZIL
Bao la kwanza la Ujerumani lilipokewa kwa vifijo na nderemo na mashabiki
waliokuwa wamejaa pomoni kushuhudia timu yao ikimenyena na mabingwa
mara sita wa kombe la dunia Brazil
Mechi hii ilikua ya kwanza ya nusu fainali katika kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil
Wengi wamesema wachezaji wa Ujerumani walikuwa 'balaa' yaani walikuwa wakali katika mechi hiyo
Kipa wa Ujerumani hakuwa na chochote cha kufanya kwani hali ilikuwa ngumu kweli.
Ilikuwa sherehe kila pembe ya dunia kutoka kwa mashabiki wa Ujerumani na
hata nyumbani baada ya timu yao kuingiza mabao matano katika dakika za
kwanza 29 za mechi hiyo
Mabao yaliendelea kuingizwa hadi yakafika saba mwishoni mwa mechi.
Brazil hata hivyo walikomboa bao moja la kupanguzia machozi, ila
halikutosha kuondoa aibu waliyoipata katika mchuano huu ambao umewaacha
wengi vinywa wazi
Mashabiki wa Brazil walikuwa wanajionea giza uwanjani magoli yakiingizwa na Ujerumai kutoka pembe zote za uwanja
Ujerumani sasa watajiandaa kumenyana na mshindi wa mechi kati ya Uholanzi na Argentina Brazil itasalia kupigania nafasi ya tatu
Huzuni ulitanda Brazil na kote duniani kwa mashabiki wa Brazil
Lakini nahodha wa muda wa Brazil David Luiz amewataka mashabiki wa timu
hiyo kote duniani kuwasamehe wachezaji waliokuwa uwanjani
Selecao,walipoadhibiwa kichapo cha mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi
ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Kwa sasa hadi fainali za kombe la dunia ni sherehe kote kote nchini Ujerumani
ENDELEA KUFUATILIA MATUKIO ZAIDI YA KOMBE LA DUNIA KUPITIA HAPAHAPA BLOG YA KIJANJA
NITAWALETEA TENA MATUKIO YA BRAZIL KUTAFUTA NAFASI YA TATU AMA YA NNE!
Alhamisi, 29 Mei 2014
TAZAMA MAZISHI YA MSANII WA BONGO MOVIE RECHO, KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM.
(PICHA NA RICHARD BUKOS, DENIS MTIMA, MAYASA MARIWATA, SHANI RAMADHANI, HAMIDA HASSAN, IMELDA TARIMO/GPL)
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)












