Jumanne, 28 Julai 2015

MATUKIO KATIKA PICHA...SIASA SIYO UGOMVI NI KUZIDIANA KETE TU










Dkt Magufuli akiwa na mbowe hii inaonyesha kuwa mbowe anakubali mziki wa magufuli mpaka kashindwa kujizuia kapanda gali moja na Dkt Magufuli.

Endelea kufuatilia kupitia blog ya kijanja

MZIMU WA AJALI ZA BARABARANI UNAENDELEA KUTUMALIZA...EEE MUNGU TUSAIDIE




Watu wanne wanasadikiwa kufariki dunia baada ya Basi la Kampuni ya Sabuni Express linalofanya safari zake kati ya Karagwe na Mwanza kugongana uso kwa uso na Gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser iliyokuwa imebeba Masister eneo la Bugorora,ikitokea Bukoba mjini kuelekea Mutukura.

Chanzo na mwandishi wa ITV na Radio One

SIASA NI MCHEZO MCHAFU....UKISEMA WA NINI WENZIO WANASEMA WATAMPATA LINI?


Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now. 
Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: k
wa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais. Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? 
Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande. Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.
 Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. 
Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.
Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi. Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala. Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.

endelea kufuatilia

Jumapili, 12 Julai 2015

Urais CCM........Magufuli Apata Ushindi wa Kishindo

Chama  cha  mapinduzi, CCM kimemteua  Dr .Magufuli  kuwa  mgombea  wa  Urais  2015. Uteuzi wa  Dr. Magufuli  umetokana na  ushindi  wa  kishindo  alioupata  baada  ya  mkutano  mkuu  kukutana jana   usiku  kwa  ajili  ya  kupiga  kura  ili  kupata  jina...oja  kati  ya  matatu  yaliyokuwa  yamependekezwa  na  Halmashauri  kuu  ya  CCM.

 Matokeo  ni  kama  ifuatavyo
1.Magufuli.....87%
2. Amina.......10%
3.Migiro......3%

Endelea kufuatilia kupitia hapa hapa kwenye blog yako ya kijamii

Jumamosi, 11 Julai 2015

CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO TAZARA MBEYA SACCOS LTD KIMETOA MIKOPO KWA WANACHAMA WAKE YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 60

WAFUATAO NI BAADHI YA WANACHAMA WALIONUFAIKA NA MIKOPO HIYO.
Bwana Yusto Barnabas (kushoto)

Bi.Teddy Ndimbo

Bwana Luka Mahenge (kushoto)

 Bi. Bupe Kalinga

Bwana. Godfrey Mwakalindile (Kulia)

Bi. Rose Mwandiwa (Kulia)

Bi. Erikanali Nyari..(Kulia) akiwa badala ya Deborah Nyari

Bi. Salome Magwaza (katikati)

Endelea kutembelea blog hii kwa habari zaidi