Jumatano, 26 Novemba 2014

NEWS ALERT: MAHAKAMA KUU IMESIMAMISHA MJADALA WA RIPOTI YA ESCROW KUJADILIWA BUNGENI UPDATES:


Tumepata taarifa muda huu kutoka kwa mtu aliyeko Mahakama Kuu kuwa 
 
kutokana na taarifa iliyokuwa inaelezwa kuwa jopo la majaji watatu wa 
 
Mahakama Kuu watasikiliza kesi iliyofunguliwa na IPTL na PAP kuzuia bunge 
 
kujadili suala la Escrow.



Imeamriwa na Mahakama Kuu chini ya jopo la majaji watatu kuwa 
 
wamesimamisha mjadala wa Ripoti ya Escrow hadi hoja za msingi zitakapo 
 
fanyiwa kazi.
CHANZO: ITV TANZANIA

Ijumaa, 24 Oktoba 2014

DIOMOND PLATINUMZ KIKAANGONI MIAKA MITATU JELA

 
Kufuatia tukio la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuonekana jukwaani na sare zinazoaminika kuwa za Jeshi la Wananchi (JWTZ) kisha kukamatwa kwa kundi lake la Wasafi Classic Baby (WCB) na meneja wake, Babu Tale, kuna uwezekano wa jamaa huyo kufungwa jela miaka miwili au mitatu.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya jeshi la polisi, baada ya jeshi kutoa tamko kuwa ni kinyume cha sheria, juzi Diamond alitakiwa kwenda kujisalimisha polisi lakini hakufanya hivyo jambo lililosababisha wenzake kukamatwa na kuwekwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Oysterbay, Kinondoni jijini Dar.
Ilisemekana kwamba baada ya Wasafi (madensa wa Diamond) kukamatwa, Babu Tale naye alifikishwa katika kituo hicho ambapo maafisa kadhaa wa jeshi la polisi walionekana katika eneo hilo wakiweka ulinzi mkali.

Chanzo hicho kilieleza kwamba, siku ya tukio Oktoba 21, mwaka huu, uongozi wa Diamond ulipewa muda wa kujieleza kabla ya saa 2:00 asubuhi lakini haukufanya hivyo ndipo hatua hiyo ikachukuliwa.
Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji kwa nini jeshi la polisi lilimshikilia Babu Tale peke yake bila Diamond lakini vyanzo vilieleza kuwa mwanamuziki huyo huenda alikuwa safarini.

Ilielezwa kwamba wanaomsaka Diamond na waliowakamata Wasafi ni wanajeshi wa Military Police (MP) ambao waliwabwaga jamaa hao kituoni hapo kisha kuendelea na mambo yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar, Camillus Wambura alisema bado hajawasiliana na kituo cha Oysterbay kuhusu suala hilo na hajapata taarifa kwa kuwa kesi hiyo inachunguzwa na iko chini ya Mkuu wa upelelezi wa Mkoa.

Akijibu kuhusu taarifa za uongozi wa Diamond na Diamond kupewa muda wa kujieleza, Kamanda Wambura alijibu:
Uchunguzi unafanywa huko (Oysterbay). Kwa sasa hivi sina taarifa hiyo nina mambo mengi sana. Kwa hiyo kwa sasa hivi uchunguzi unafanywa chini ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa. Sijapata nafasi ya kujua wamefikia wapi katika uchunguzi wa suala hilo.”

Mapema wiki hii, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari likipiga marufuku raia kuvaa sare za jeshi.
Kwa mujibu wa mwanajeshi wa JWTZ ambaye aliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo, taaluma yake ya sheria imemfanya kuchimba kwa undani suala hilo na kugundua kuwa endapo Diamond atapatikana na hatia atapigwa faini au kwenda jela miaka miwili au mitatu au vyote, yaani faini na kifungo.
Alisema kosa la Diamond ni kushindwa kutii wito kwani alitakiwa kuripoti mwenyewe polisi hivyo lazima atapanda mahakamani kujibu shitaka hilo na lile lenyewe la kutumia sare za jeshi hilo.Chanzo hicho kilidai kwamba si mara ya kwanza kwa jamaa huyo kuingia kwenye kashikashi kama hiyo kwani kuna kipindi alikwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo alionekana na sare hizo stejini na akapewa onyo lakini safari hii amejiongeza tena kuonesha kuwa ni kichwa ngumu.

Jumamosi, 6 Septemba 2014

DAAAH MWENYEZI MUNGU ATUNUSURU NA HIZI AJALI ZINAZOTOKEA MARA KWA MARA

samahani kwa picha hizi ajali iliyotokea jana huko Msoma na kuua watu 36 na kujeruhi wengine 76


Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Kilari Mkoani Mara likiwa limeumia vibaya sana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini Musoma leo  mchan.

Watu 36 wamepoteza maisha papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya sana.Kwa mujibu wa Ripota wetu aliyekuwa eneo la tukio,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni  kuwa Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni, hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.

Ndani ya gari hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.
Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
Umati wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 36 kupoteza maisha wakishuhudia tukio hilo la ajali.


Guldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.

Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
 
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.

Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokozi ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.