Jumanne, 3 Septemba 2013

Club ya Arsenal yafanikiwa kumsajili Mesut Ozil

Mesut Ozil
Ozil mwnye umri wa miaka 24 ameungana na Club ya Arsenal akitokea Real Madrid.
Meneja wa Club ya Arsenal..Arsene Wenger amesema tumefanikiwa kupata saini ya Mesut Ozil, yeye ni mchezaji mkubwa mwenye ubora wa kila Club na wa kimataifa pia.

"Nimesema kwa kipindi chote cha majira ya kiangazi tumekuwa tukifanya juhudi za kupata wachezaji wenye kiwango cha juu kwa ajili ya club hii. Hii ilihusisha watu wengi ndani na nje ya club yetu na nimepata ushirikiano mkubwa katika maamuzi ya club mambo yanayohusu mpira wa miguu"
"Mesut ana kiwango kikubwa cha juu katika kucheza mpira na atakuwa msaada mkubwa kwa club yetu kufikia malengo.Mesut atajiunga na Arsenal baada ya kucheza mechi yake ya kimataifa na timu yake ya Ujerumani na kuwa nasi kama mchezaji wa Arsenal"...alisema Meneja huyo wa Arsenal