NEWS ALERT, PICHA: NDEGE YA FASTJET YAFANYA (SURVEY) KATIKA ANGA YA UWANJA WA KIMATAIFA WA NDEGE SONGWE JIJINI MBEYA.
Ndege kubwa ya Fastjet ikiwa inaonekana angani wakati ikifanya survey juu ya uwanja wa kimataifa wa Songwe Mbeya
Hizi ni Ngazi maalum kabisa ambazo zinatarajiwa kutumika wakati ndege ya Fastjet itakapo anza safari zake mkoani Mbeya.
Wanaosalimiana
ni Watumishi wa Eneo la uwanja wa Ndege na Aliye vaa Nguo za Blue
pamoja ni Bwana Mwaipopo mdau mkubwa wa Mbeya yetu Blog.
Huyu Bwana mdogo anaitwa Eric Mwaisango nae alikuwepo kushuhudia ndege ya Fastjet
Hili ni eneo la Nje ya la Uwanja wa kimataifa wa Songwe Mbeya
****
Leo
asubuhi majira ya saa Mbili na nusu Ndege ya Fastjet kwa Mara ya kwanza
kabisa ilishuhudiwa na watu wachache katika Uwanja wa wa Ndege wa
Kimataifa wa Songwe ambapo ilikuwa ikifanya Survey angani bila kutua.
Ndege
hiyo ambayo ilipita jirani kabisa na uwanja huo kwa Takribani ya zaidi
ya mara tatu , ilifanya hivyo kwa sababu za kitaalam, hata hivyo hiyo
ilikuwa ni amsha amsha huku siku chache zijazo ndege hiyo itatua kwa
mara ya kwanza na Rasmi Jijini Mbeya katika uwanja wa Ndege wa Songwe.
Kwa
nyakati Tofauti Baadhi ya Abiria waliokuwa wakijiandaa na kusafiri
katika uwanja huo na Ndege zengine walionekana kuwa na furaha na
kuzungumza mambo tofauti ikiwa na pamoja na kufurahishwa na hatua ya
Ndege ya fastjet kuanza safari zake mkoani Mbeya na kusisitiza kwamba
itakuwa ni Mkombozi mkubwa kutokana na bei zao kuwa chini na safari za
uhakika.
Timu
nzima ya Mbeya yetu Blog ilifika uwanjani mapema na kushuhudia kile
kilicho onekana uwanjani hapo, na mpaka wanaondoka uwanjani hapo ndege
hiyo ilikuwa tayari imesha anza safari za kurejea jijini Dar es salaam.
Je Mwananchi na Mkazi wa Mbeya na Mikoa ya Jirani unasemaje kuhusiana na Fastjet kuanza safari za kuja Mbeya hivi karibuni???