Jumamosi, 11 Julai 2015

CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO TAZARA MBEYA SACCOS LTD KIMETOA MIKOPO KWA WANACHAMA WAKE YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 60

WAFUATAO NI BAADHI YA WANACHAMA WALIONUFAIKA NA MIKOPO HIYO.
Bwana Yusto Barnabas (kushoto)

Bi.Teddy Ndimbo

Bwana Luka Mahenge (kushoto)

 Bi. Bupe Kalinga

Bwana. Godfrey Mwakalindile (Kulia)

Bi. Rose Mwandiwa (Kulia)

Bi. Erikanali Nyari..(Kulia) akiwa badala ya Deborah Nyari

Bi. Salome Magwaza (katikati)

Endelea kutembelea blog hii kwa habari zaidi

HABARI KUBWA LEO-CCM KUMFIA KIKWETE WIKI HII?.MIPANGO YA KUASI CCM YAVUJA NI YAWASAKA URAIS,SOMA HAPO KUJUA


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika hivi karibuni picha na maktaba.
HATMA ya Chama cha Mapinduzi CCM kuendelea salama au kufikia tamati na kuingia kwenye mpasuko mkubwa kutokana na Makada wake wanaotaka Urais ndani ya Chama hicho ni itabianika wiki hii.(Mtandao huu unaripoti) anandika KAROLI VINSENT endelea nayo
              Baada ya Kamati kuu ya chama hicho CC  kinachotarajiwa kukutana Alhamisi ya Terehe 9 ya wiki hii ambapo kwa mujibu ya Ratiba ya chama hicho inaonyesha pamoja na mambo mengine kamati itakuwa na jukumu moja tu la  “Kufyeka” majina ya takribani 38 ya makada walioomba ridhaa ya kutaka urais kwenye Chama hicho na kubakisha majina matano.
        Taarifa kutoka ndani ya CCM zinasema kwa sasa chama hicho kipo kwenye presha kubwa kutoka kwa makada wake ambao wamejiapiza kwa udi na Uvumba lazima wapite na kuwa Mgombea wa Urais ambao taarifa zinasema Makada hao wanaojiapiza  ni wale wanakubwa na Kashfa za ufisadi pamoja na kukiuka kanuni za chama.
        Makada hao wakiongozwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa Ufisadi wa Kampuni ya tata ya kufua Umeme ya Richmound Edward Lowassa ambaye mara kwa mara kupitia Kambi zake kwamba akisema “hakuna wakulita jina lake ndani ya CC”
          Mbali na Lowassa Kada mwengine wa CCM ambaye amekuwa akijiipiza pia hakuna wakulikata jina lake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimatifa Benard Membe  ambapo naye amekuwa ajisifu kuwa lazima apite na kuwa Rais.
       Kwa Mujibu wa Vyanzo vyetu vilivyopo ndani ya CCM zinasema kwa sasa chama hicho,kimekuwa na Presha kubwa ambapo kwa sasa wanatafakari ni njia gani watatumia kuwachagua wagombe ambapo watakiaacha chama hicho  salama,
   “Yaani wiki hii ndio chama chetu  kitakuwa salama au ndio kitameguka maana kwa sasa chama kimekuwa na makundi makubwa sana ambayo kusema kweli hata kamati kuu sijui itakuja na jibu gani,ukitazama kuna makada wengi wamekubwa na kashfa kubwa za ufisadi wamekuwa ana nguvu tena wamepanga hata kufanya uasi endapo majina yao yatakatwa”
   Taarifa zanasema Kada ambaye amekuwa akiogopesha Chama hicho ni Edward Lowassa ambapo  kwa sasa amekuwa na Nguvu kubwa sana ndani ya chama hicho kutokana na mipango ambaye ameiandaa,
        “Huyu bwana kusema kweli basi tena hawamuwezi,maana amekuwa na makundi makubwa ndani ya chama chetu amewanunua wajumbe wa Mkutano mkuu kwa pesa nyingi sana,yaani amevunja kanuni ya wazi za chama,amejigeuza kama kiongozi mkuu wa chama,yaani mapaka sasa chama kinamwogopa sana”
     Kwa mujibu taarifa kutoka kambi ya Lowassa zinasema kwa sasa wamepanga hata kufanya “uasi”endapo kamati kuu ya CCM wakimkata mgombea wao.
        “Sisi tunangojea kwa hamu siku hiyo ya tarehe 9 ndugu,ndio utaona makubwa hapa nchini,yaani tunajua kwenye kamati ya CC  kunawatu hawamtaki Lowassa na wamepanga kumkata jina lake,nakuhakikishia hatukubali na ukitaka kuamini ngojea uone”
              Kwa mujibu wa ratiba ya CCM inaonyesha baada ya kamati kuu ya ccm kupendekeza majina matano,kinachofuata ni Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi CCM nayo itayakata majina mawili kati ya matano na kubakiza majina matatu ambayo yanapigiwa kura siku ya tarehe 11 na 12 ya jumamosi na jumapili na kupatikana mgombea Mmoja wa Urais pamoja na Makamu wake.
     Taarifa za kiuchunguzi kutoka ndani ya Kambi ya Lowassa zinasema endapo Lowassa akipitishwa na Kamati kuu CC kinachofuata ni kutafuta kura za wajumbe 175 wa NEC kwa udi na Uvumba.

“Ujue sisi tunajua kabisa Lowassa akipita tu CC tayari Safari ya Matumaini imefanikiwa maana tumeshapata kura 175 za wajumbe wa NEC basi tumefanikiwa nakuhakishishi tutazipata kura hizo,tatizo ni kamati kuu ndugu,”