Jumapili, 15 Septemba 2013

Obama awasiliana na rais mpya wa Iran

Obama akizungumza juu ya Iran
Rais wa Marekani Barack Obama 
Rais Obama anasema ameandikiana barua na rais mpya wa Iran, Hasan Rouhani.
Akihojiwa na televisheni ya Marekani, ABC, Bwana Obama alisema Iran inafahamu kuwa sera ya Iran ya kujaribu kuunda silaha za nuklia ni swala kubwa zaidi kwa Marekani kushinda silaha za kemikali zilizotumiwa na Syria.
Rais Obama ametokeza mara nyingi kwenye televisheni za Marekani katika wiki za karibuni kuwakumbusha watu tishio la silaha za kemikali za Syria.
Jumapili aliulizwa jee Iran itafikiria vipi msuko-suko wa Syria?.
Rais Obama alisema amewasiliana na rais mpya wa Iran, Bwana Rouhani.
Na alisema kuna tofauti baina ya Iran na Syria.
Alikiri kuwa mradi wa nuklia wa Iran unavotishia Israil, ni jambo lilo karibu na masilahi ya Marekani kushinda silaha za kemikali.
Aliongeza kusema kuwa mashindano ya kumiliki silaha za nuklia yanaweza kutibua sana eneo hilo.
Akilinganisha Iran na Syria, Rais Obama alisema anafikiri Iran inatambua kwamba kuna njia ya kusuluhisha maswala haya kidiplomasia, ingawa alikiri kuwa ni vigumu kuzungumza na Iran.


KWA UFUPI na MATUKIO KATIKA PICHA

Wapiganaji wa Seleka  mjini Bangui waliponyakua madaraka mwezi March
Brazzaville yatuma askari zaidi CAR
Congo-Brazzaville imezidisha zaidi ya mara dufu idadi ya askari wake katika kikosi cha kuweka amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wenyeviti wa vyama vya Siasa vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi leo wamekukutana na wahariri na waandishi wa habari kueleza mikakati na mbinu watakazozitumia kunusuru Taifa lisiingie kwenye utungaji wa Katiba Mpya itakayobeba masilahi ya chama tawala.
Askofu Ignatius Kattey 
Askofu aachiliwa huru huko Nigeria
Kiongozi mmoja wa kanisa la Anglikana la Nigeria ambaye alitekwa nyara zaidi ya majuma mawili yaliyopita, ameachiliwa huru.
 
Polisi Simiyu yatoa ripoti ukatili wa Dagashida, fisi wakoleza mauaji
Wananchi wa Simiyu wakiwa kwenye mkutano wa pamoja kujadili suluhisho la mauaji ya kikatili eneo lao
 
Dawa ya Mifugo yatengeneza GONGO Dar...!
Jiko maarufu kama mtambo wa Gongo  

Shambulizi la maguruneti lawaua 2 Rwanda


 Watu wawili wameuawa katika mashambulizi ya guruneti mjini Kigali Rwanda.
Mwathiriwa wa kwanza alifariki katika shambulizi la kwanza lililotokea Ijumaa katika soko moja mjini humo.
Shambulizi hili pia liliwajeruhi watu 14 kwa mujibu wa taarifa za polisi.
Guruneti lengine lililipuliwa katika eneo hilohilo Jumamosi na kumuua mtu wa pili huku

HAYA YATAISHA LINI?

Wanajeshi wakivizia wapiganaji wa MNL Zamboanga, Ufilipino
Jeshi la Ufilipino linasema limewazunguka wapiganaji wanaodhibiti mji wa Zamboanga, kusini mwa nchi, baada ya siku sita za mapigano ambayo yamepelekea watu zaidi ya laki saba kuhama makwao.
Mwandishi wa BBC Barani Asia anasema risasi zimekuwa zikifyatuliwa wakati wote huku jeshi likijongelea maeneo mawili ya mwisho yenye mapigano mjini Zamboanga.
Takriban watu 65,000 inajulikana wameuwawa.
Jeshi limeripoti kuwa wengi waliouwawa ni wapiganaji wa kundi la Moro National Liberation Front, MNLF.
Raisi Benigno Aquino na makamu wake wamezuru eneo hilo Jumamosi ili kufanya majadiliano ya kutafuta amani, lakini kwa sasa inaarifiwa wanaongoza jeshi wakati linakabiliana na wapiganaji.