Kutekwa kwa mji wa Konna nchini Mali kulisababisha Ufaransa kupeleka
wanajeshi wake huko kushika doria...hali hii ndiyo ilimpa furaha isiyo
na kifani mtu huyu kwani waasi walikuwa wameweka sheria za kiisilamu
zilizoharamisha mambo mengi
Timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles ndiyo iliyowaondoa mashabiki hawa
kutoka katika viti vyao baada ya kushinda kombe la taifa bingwa Afrika.
Kombe hilo lilikuwa limewakwepa kwa miaka 13
Zimbabwe ilikwenda kwenye debe mara mbili, kupigia kura kura ya maamuzi
na uchaguzi mkuu. Mugabe ndiye aliyeshinda na huyu ni mmoja wa mashabiki
wake
Nchini Afrika Kusini mambo yalikuwa mitindo mipya na ya kisasa kwenye mashindano ya mitindo ambayo vijana hawa walishiriki.
Eneo la Mashariki mwa Congo lilivamiwa na waasi wa M23 kwa karibu mwaka
2013 wote, lakini mwishoni baada ya juhudi nyingi za jeshi la DRC na UN
waasi hao walisalimu amri baada ya kupata kipigo kikali.
Mnamo mwezi Juni, jeshi la Senegal lilimkaribisha Rais Barack Obama kwa
ziara yake ya Afrika akianzia nchini humo na kisha kuelekea Afrika
Kusini na Tanzania.
Shambulizi la kigaidi lilikumba Kenya mwezi Septemba ambapo watu zaidi
ya sitini na tano waliuawa baada ya wanamgambo wa Al shabaab kuteka
jengo la westgate kwa zaidi ya siku tatu
Maombi yalifanywa kote nchini humo hali ilipozidi kuwa mbaya
Disemba dunia iliomboleza kifo cha hayati Nelson Mandela alipofariki
akiwa na umri wa miaka 95.Alizaliwa kijijini Qunu na alizikwa tarehe 15
mwezi Disemba.
Mjane wa Mandela Garaca Machel na aliyekuwa mke wa Mandela Winnie
Mandela wakiomboleza kifo cha mzee Mandela wakati wa mazishi ya shujaa
huyo wa Afrika