Jumanne, 22 Oktoba 2013

YANGA WALITANGULIA JE WALIFIKA?


Baadhi ya mashabiki walizima kwa mshangao wa kilichokuwa kinaendelea uwanjani
Ama kweli kutangulia si kufika,au kama wanavyosema wakongomani kuwa KOKENDE LIBOSO,EZA KOKOMATE.
Usemi huo ulidhihirika hapo jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya Mabingwa watetezi Ligi kuu soka Tanzania Bara Timu ya Yanga,pamoja na kutangulia kufunga bao 3 dhidi ya Simba hadi mapumziko,walijikuta wakiambulia sare ya bao 3-3 hadi Mwisho wa mchezo baada ya Simba kusawazisha bao zote katika Kipindi cha Pili.
Huku Simba wakiwa wamepoteana hasa idara ya Ulinzi,ilianza kuruhusu wavu wake kutikishwa katika dakika ya 14 baada ya Mchezaji wake wa msimu uliopita Mrisho Ngasa kutia chuma wavuni kufuatia pasi ya Didier Kavumbagu.