Jumatano, 25 Septemba 2013

TETEMEKO LA ARDHI LAUA WATU 270 PAKISTAN


Zaidi ya watu 300 wamejeruhiwa

Tetemeko kubwa la ardhi limewauwa watu 270 katika mkoa wa Kusini Magharibi wa Balochistan nchini Pakistan.

Tetemeko hilo la kipimo cha 7.7-lilipiga Jumaanne alasiri . Nyumba nyingi zilibomolewa na watu wengi walipaswa kulala nje

Baada ya tetemeko hilo ,kisiwa kidogo kiliibuka nje ya mwambao karibu na bandari ya Gwadar.

Watu walikusanyika ufukweni kushuhudia kisiwa hicho kipya ambacho kinakadiriwa kua na urefu wa mita 200 na upana wa mita 100 na kiinuka mita 20 kutoka upeo wa bahari .

Balochistan ndio mkoa mkubwa wa Pakistan lakini ukiwa na watu wakaazi wachache kupita yote
Eneo hilo hukumbwa na mitetemeko ya mara kwa mara na mnamo mwezi wa Aprili watu 35 waliuwawa katika tetemeko ambalo kitovu chake kilikua Kusini Mashariki mwa Iran mnamo mwezi wa April

Tetemeko hilo lilikua la nguvu hata watu wa miji iliyo mbali ya Karachi, Hyderabad, na mji mkuu wa India, Delhi walihisi mtikisiko wake.

Vijiji vizima inaarifiwa vilifyekwa katika wilaya ya wakaazi masikini ya Awaran
Msemaji wa serikali ya Balochistan, Jan Buledi, amesema waliopatwa na maafa zaidi ni katika mji wa Awaran na vijiji vinavyouzingira na ameonya idadi ya vifo huenda ikaongezeka. Takriban watu 340 wamejeruhiwa.

Msemaji huyo amesema kuna ukosefu mkubwa wa huduma za matibabu na hospitali hazina nafasi za kutosha kuwatibu majeruhi .

Alisema helikopta zinawasafirisha majeruhi mahututi hadi mjini Karachi na wengine wanahudumiwa katika wilaya jirani.

Jeshi la Pakistan lilikua miongoni mwa makundi ya kwanza kutoa msaada kwa kua tayari limekua huko miaka kadhaa sasa kwa sababu ya uasi wa watu wanaotaka kujitenga kwa mkoa huo wa Balochistan.

Jeshi limesema limetuma zaidi ya wanajeshi 200 , wana matibabu na mahema kutoka mji mkuu wa mkoa huo Quetta, lakini shughuli za uokozi zinatatizwa kwa hali ya milima ya eneo hilo.

SHAMBULIO LA WASTGATE LAATHIRI MASHINDANO YA MAGONGO



Mashindano ya magongo 

Mashindano ya magongo kwa mataifa ya Afrika yaliyopangiwa kuanza Alhamisi wiki hii mjini Nairobi huenda yakaahirishwa kutokana na mkasa wa jumba la Westgate lililovamiwa na magaida wa Al Shabaab, na zaidi ya watu sitini kuuawa

Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa magongo cha Kenya Nashon Randiak anasema shirikisho la kimataifa,FIH, lina wasiwasi kuhusu usalama wa wachezaji mjini Nairobi baada ya magaidi wa Al Shabaab kulivamia jengo la kibiashara la Westgate jijini Nairobi.

Licha ya Randiak kuwaeleza kwamba hali sasa ni shwari baada ya magaidi wote kuuwa na wanajeshi wa Kenya shirikisho la kimataifa limesema linataka mkuu wa polisi nchini Kenya kuwahakikisha usalama wa wachezaji.

Randiak ameshangazwa na msimamo huo akisema mashambulizi ya magaidi hutokea kote duniani hivyo anashangaa ni kwanini hili la Kenya linachukuliwa ni kama la kipekee..

Mataifa yanayotarajiwa kushiriki kwa wanaume ni Kenya, Ghana na Afrika Kusini na kwa wanawake ni Kenya, Tanzania,Ghana na Afrika Kusini. Timu ya Tanzania ikiongozwa na katibu wa chama cha magongo mkoa wa Dar es salaam Mnonda Magani tayari imeshawasili mjini Nairobi.
Timu ambazo zimejiondoa kwa sababu mbali mbali na sio hiyo ya Westgate ni pamoja na Nigeria, Namibia, Misri na Ushelisheli.

HIVI NDIVYO WAKENYA WANAVYOSHIRIKI MAZISHI YA WAHANGA WA WESTGATE


NCHINI SUDAN WANANCHI WAFANYA MAANDAMANO KUPINGA KUONDOLEWA KWA RUZUKU YA MAFUTA



Waandamanaji wanapinga hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya mafuta

Polisi nchini Sudan wamewatifulia gesi ya kutoa machozi waandamanaji katika Mji Mkuu 

Khartoum, huku wengi wakiendelea kukasirishwa na kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta.
Walioshuhudia maandamano hayo walisema kuwa waandamanaji waliteketeza jengo moja la Chuo 

Kikuu na vituo kadhaa vya petroli. Pia waliziba njia kuu ya kuelekea uwanja wa ndege.
Watu wawili wameuawa tangu maandamano hayo kuanza Jumatatu wakati Serikali ilipotangaza 

WATANZANIA TUACHE KUCHAGUA KAZI

WAENDESHA BODA BODA 300 WILAYANI RUNGWE WATUNUKIWA VYETI VYA UDEREVA PAMOJA NA LESENI.

Baadhi ya Pikipiki zinazoendeshwa na vijana Wilayani Rungwe waliotunukiwa vyeti na Leseni na Mkuu wa Wilaya hiyo Crispin Meela baada ya kumaliza mafunzo.
Afisa Biashara wa Wilaya ya Rungwe, Prince Mwakibete akisoma majina ya madereva wanaostahili kutunukiwa vyeti na mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crispin Meela.  
Dereva wa Bodaboda Baraka Mwasile akisoma risala kwa niaba ya madereva wenzie kabla ya kuanza kwa zoezi la kuwatunuku Vyeti na Leseni zao.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Noel Mahyenga akizungumza na Madereva wa bodaboda na kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ili akabidhi vyeti na Leseni.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crispini Meela akizungumza na Madereva wa bodaboda kabla ya kuanza kwa zoezi la kuwatunuku vyeti na leseni za kuendeshea pikipiki kwa vijana 300 wa Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe akimkabidhi cheti dereva wa bodaboda kwa niaba ya wenzie 300 katika hafla iliyofanyika nje ya jengo la ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Tukuyu mjini.
Baadhi ya madereva wa Bodaboda wakifuatilia kwa makini zoezi la kutunuku vyeti lililokuwa likifanywa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe.



IMEELEZWA kuwa

SOMA TAARIFA YA RAIS WA KENYA KUHUSU WASHUKIWA WA UGAIDI "WASTGATE"

 
RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA 
 
Askari wa Kenya wakiwa juu ya jengo la Westgate jana kuwasaka magaidi walioteka watu tangu Jumamosi
Wakati jengo la ghorofa tatu lililovamiwa na magaidi likiripotiwa kuanguka jana na kuua watu sita, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema mwanamke mmoja raia wa Uingereza na Wamarekani wawili au watatu wanashukiwa kuongoza shambulizi la kigaidi lililofanywa katika jengo la biashara eneo la Westgate, Nairobi, Jumamosi iliyopita.
 
ASKARI ALIVYOJITAHIDI KUOKOA ZAIDI YA WATU 100 KENYA
MMOJA WA MAJERUHI AKIOKOLEWA

SERIKALI YA KENYA YATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO



Baadhi ya wakenya waliopoteza jamaa zao katika shambulizi la Westgate

Kenya inaanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kwa waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi.
Rais Uhuru Kenyatta pia ameseama kuwa bendera zitapepershwa nusu mlingoti kwa heshima ya waliopoteza maisha yao katika mashambulizi hayo.