
Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 30, viongozi wa Marekani na Iran wamezungumza moja kwa moja.
Rais Barack Obama na mwenzake wa Iran, Hassan
Rouhani, wamezungumza kwa simu kwa muda wa robo saa; na kwa mujibu wa
Bwana Obama walieleza azma yao ya kutatua mzozo wa muda mrefu kuhusu
mradi wa nuklia wa Iran.
Ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kutoka ofisi ya Bwana Rouhani ulionesha hisia kama hizo.
Taarifa kutoka Iran zinaonesha kuwa tukio hilo limefurahiwa nchini humo, hasa kati ya washauri wakuu wa Bwana Rouhani.

RAIS JAKAYA M. KIKWETE AKISAINI KITABU CHA RAMBIRAMBI CHA WAHANGA WA MLIPUKO WA WASTGATE SIKU YA JANA HUKO NEW YORK MAREKANI.
AFISA HABARI WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NDUGU OWEN MWANDUMBYA AKIONGEA NA MAAFISA HABARI WENGINE WA BUNGE JIJINI DAR ES SALAAM HAPO JANA IJUMAA 
