Ijumaa, 13 Septemba 2013

Padre Mwang'amba wa Kanisa Katoliki Zanzibar kamwagiwa tindikali huko Mlandege katika cafe ya Sun Shine.



kisiwa cha zanzibar

Polisi huko visiwani Zanzibar wanachunguza tukio la kasisi wa kanisa katoliki kushambuliwa kwa tindikali.
Imeelezwa kuwa Kasisi huyo Anselmo Mwang'amba, alimwagiwa tindikali akitoka mgahawa mmoja wa kutumia mtandao mjini Zanzibar. Tukio hilo linatokea ndani ya mwezi mmoja tangu wasichana wawili wa kiingereza kushambuliwa.
Hili ni janga jingine kwa Zanzibar ambayo imekuwa ikizongwa na matukio ya aina hii kwa muda sasa.
Mkurugenzi wa upelelezi wa Zanzibar, Yusufu Ilembo ameieleza BBC kuwa bado hawajakamata mtu yoyote kuhusika na tukio hilo ingawa amethibitisha kuwa uchunguzi tayari umeanza.
Ameeleza kuwa Kasisi Mwang'amba aliungua usoni na mabegani na kwamba anaendelea kutibiwa.
Katika miaka ya karibuni Zanzibar imekabiliwa na mikasa ya watu kushambuliwa hivi na kuzua hisia kuwa chuki za kidini.
Mapema mwaka huu kasisi mwingine wa kanisa katoliki alishambuliwa kwa risasi na kuuawa.
Mwezi uliopita Zanzibar ilitikisika kutokana na wasichana wawili wangereza kushambuliwa kwa tindikali na watu wasiojulikana.
Kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu pia alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.

Cape Verde yaadhibiwa na FIFA


Kikosi cha Cape Verde hakitashiriki mchuano wa kombe la dunia mwaka 2014
 
Cape Verde imebanduliwa nje ya kinyanganyiro cha kufuzu kwa dimba la dunia Mwakani kwa nchi za Afrika.
Kwa mujibu wa tovuti ya shirikisho la soka duniani FIFA, Cape Verde ilikosea kwakumshirikisha mchezaji aliyekuwa amepigwa marufuku katika mechi yao dhidi ya Tunisia Jumamosi iliyopita
Kwa mujibu wa FIFA Fernando Verela hakufaa kucheza katika mechi hiyo waliyoshinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Tunisia . FIFA sasa imebadilisha matokeo hayo na kuipa Tunisia ushindi mkubwa wa mabao 3-0 .
Cape Verde ilipo kundi B ilikuwa inaongozwa na Tunisia kama inavyoonekana hapa chini.
Kundi B
Tunisia - 14
Cape Verde - 9
Sierra Leone - 8
Eq Guinea - 2
Kauli hiyo imeipa Tunisia alama za kutosha kuipiku Cape Verde kutoka kileleni mwa kundi B ikiwa na alama 14 .Cape Verde ni ya pili na alama 14.
Shirikisho la soka la Cape Verde lilimetozwa faini ya dola $ 6400 .

UNHCR - Tanzania haijawafukuza wakimbizi


wahamiaji haramu wahamishwa TZ sio wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, ofisi ya Tanzania limekanusha taarifa katika baadhi ya vyombo vya habari kwamba, Tanzania imewarejesha nyumbani kwa nguvu, wakimbizi 25,000 wa Burundi mwezi mmoja uliopita.

MWANAMKE AMCHOMA MOTO MWANAUME ALIYEMBAKA



 Mwanamke mmoja aliyebakwa alikuwa anaact kama anataka kumsamehe mwanaume aliyembaka miezi michache iliyopita akiwa amemtishia kisu.Mwanamke huyo aliamua kumkaribisha nyumbani kwake ili wafahamiane vizuri na pia wajadiliane maamuzi kuhusu kesi yao ya ubakaji nje ya maamuzi ya mahakama.

 Habari zilizokusanywa na Reportghananews.com zinasema kuwa,mwanaume huyo alipofika tu,mwanamke (aliyebakwa) alimpa sehemu ya kukaa alafu akamwambia kwamba anaenda kumwandalia chakula,ila alikuwa na kisasi akilini mwake.
Mwanamke huyo aliyebakwa alipanga na kaka zake kumpa fundisho mbakaji huyo.  
Kwa msaada wa kaka zake alimmwagia mafuta ya taa mbakaji huyo na kumchoma moto.

‘Changudoa’, ombaomba 200 wakamatwa Dar


Mgambo wa Jiji wakiwateremsha ombaomba kwenye gari baada ya kuwakamata katika operesheni maalumu Dar es Salaam jana na kuwafikisha kwenye Mahakama ya Jiji ambapo walisomewa shtaka la uzururaji

Ombaomba zaidi ya 200 na wasichana wanaofanya biashara ya ngono maarufu kama ‘dada poa’  usiku wa kuamkia jana walikamatwa kwenye operesheni maalumu ya kuwaondoa katika maeneo mbalimbali ya jiji,iliyofanywa kwa ushirikiano wa Polisi na askari wa jiji.
Ombaomba na kinadada hao walikamatwa kwenye

AFRIKA KATIKA PICHA WIKI HII

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/08/12/130812094722_wiki_hii_picha_976x549_bbc_nocredit.jpg
Katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, siku hiyo ya Jumanne mtoto akitembea na bunduki bandia kwenye ufuo wa bahari ya Lido
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/08/12/130812095223_wiki_hii_picha_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Mnamo siku ya Jumapili, kijana huyu anaonekana akicheza na mpira katika kambi ya watu walioachwa bila makao kufuatia mapigano katika mkoa wa Kivu Kaskazini karibu na mji wa Goma
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/08/12/130812095442_wiki_hii_picha_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Siku mbili baadaye mama huyu anaanda Ugali katika mji katika kambi nyingine karibu na mji wa Goma
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/08/12/130812095628_wiki_hii_picha_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Mwanamume mmoja Mashariki mwa mji wa Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria anapuliza ala yake ya muziki wakati wa sherehe za Idd 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/08/12/130812095703_wiki_hii_picha_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Mji wa Maiduguri ni kitovu cha harakati za Boko Haram na hii ndio mara ya kwanza kwa sherehe za idd kufanyika mjini humo tangu kundi hilo kuanza harakati zake
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/08/12/130812095535_wiki_hii_picha_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Mwanamke anawaelekeza vipofu watatu ambao huimba wakati wakiomba pesa katika soko moja mjini Bamako, Mali 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/08/12/130812095041_wiki_hii_picha_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Familia ambazo nyumba zao ziliharibiwa kwenye mafuriko mjini, Khartoum, wanapumuzika kwenye vitanda vyao kando ya barabara Jumanne. Mashirika ya misaada yalisema kuwa watu 11 walifariki na wengine 98,500 wameathiriwa na mafuriko hayo ambayo chanzo chake ni mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha tangu tarehe moja hadi nne mwezi huu
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/08/12/130812094645_wiki_hii_picha_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Mashua ya uvuvi kwenye ufuo wa bahari katika mji mkuu wa Senegal , Dakar ikielekea baharini siku ya Jumanne ambako boti moja iliharibika na kuvuja mafuta. Hali ingali kudhibitiwa na tayari imezua wasiwasi kuhusu uharibifiu wa mazingira

Maji mapya Kenya: Laana au baraka?

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/12/130912141813_kenya_maji_1_976x549_bbc_nocredit.jpg
Visima vikubwa vimegunduliwa chini ya ardhi katika eneo kame la Turkana Kaskazini mwa Kenya . Hii ni kwa mujibu wa tangazo la serikali ya nchi hiyo. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/12/130912141855_maji_2_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Serikali inakadiria kuwa visima hivyo vilivyopatikana kwa kutumia picha za satelite , huenda vikakidhi mahitaji ya maji kwa nchi nzima kwa kipindi cha miaka sabini.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/12/130912141930_maji_3_976x549_bbc_nocredit.jpg
 Watu wa jamii ya Turkana ni watu wa kuhamahama na huathirika mno wakati wa ukosefu wa mvua kwani ina maana kuwa wanakosa maji kwa mifugo wao.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/12/130912142343_maji_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Ugunduzi huo wa maji ulitangazwa wakati wa ufunguzi wa kongamano la kimataifa kuhusu maji nchini Kenya lililoandaliwa na shirika la Unesco. Shirika hilo lilishirikiana na serikali ya Kenya pamoja na shirika la maendeleo la Japan JICA
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/12/130912142127_maji_6_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Waziri alisema kuwa kipaombele kinapewa mwanzo kukidhi mahitaji ya watu wa eneo hilo. ''Tunatarajia kuwa maji yataweza kupatikana katika kipindi cha mwezi mmoja ujao,'' alisema waziri . 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/12/130912142048_maji_5_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Maji hayo pia yatatumiwa kwa kilimo cha unyunyiziaji na viwanda. Hivi maajuzi mafuta yaligunduliwa Turkana na kulifanya eneo hili kuonekana kuwa na utajiri wa rasilimali. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/12/130912142011_maji_4_976x549_bbc.jpg
Licha ya rasilimali hizi, wakaazi wa eneo hili wanaishi katika umaskini mkubwa mbali na kuhisi kuwa wametengwa .Wanatarajia kuwa serikali itaweza kuwashirikisha katika uamuzi wa ambavyo rasilimali hizi zinaweza kutumika ili kuwafaidi wakaazi 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/12/130912142424_maji_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Wanaharakati wanataka serikali ielewe umuhimu wa kushirikisha wakaazi na kuwapa fursa wao wenyewe kusema ambavyo wanataka rasilimali zao zitumike

Mogadishu hali ni tete..watu wahamishwa kwa nguvu


 


Wakimbizi wa ndani nchini Somalia
Maelfu ya watu wanaondoshwa kwa nguvu kutoka kutoka kambi za muda mjini Mogadishu kutoa nafasi kwa maafisa wa mji huo kufanya shughuli za usafi na ukarabati.
Hii ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty.
Shirika hilo limesema kuwa watu wameendelea kuondoshwa kwa nguvu, katika miezi ya hivi karibuni licha ya maafisa wa serikali kukosa kupata maeneo mbadala salama ambako watu hao wanaweza kuhamia.
“Hili halipaswi kuwa linafanyika kwa watu waliotoroka mji mkuu wakitafuta usalama tena kuhamishwa mkwa nguvu.
Hali hii imesababisha visa vingi vya ukiukwaji wa haki za binadamu.
“Serikali ina wajibu wa kulinda watu hawa wasiojiweza na kuhakikisha usalama wao,’’ alisema Gemma Davies, mtafiti mkuu wa shirika hilo la Amnesty International.
Zaidi ya watu 300,000 wanaishi katika kambi za muda mjini Mogadishu ambako wanajihifadhi kutokana na ukame, njaa na vita vya miaka mingi nchini Somalia ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu.
Mnamo mwezi Januari, mwaka 2013, serikali ya Somalia, ilitangaza mpango wa kuwahamisha maelfu ya wakimbizi wa ndani kutoka Mogadishu katika kambi zilizo nje ya mji ili kutoa nafasi kwa ukarabati wa mji huo.
Mpango wa serikali hata hivyo ulionekana kuwa na dosari ikizingatiwa shughuli yenyewe ya kuwahamisha wakimbizi hao, muda na eneo salama ambalo wangepelekwa.