Jumatano, 18 Septemba 2013
habari za hivi punde:Jeshi la Nigeria lawaua wapiganaji 150
Wanajeshi 9 wangali hawajulikani waliko baada ya makabiliano makali kuzuka kati ya wapiganaji na wanajeshi hao mjini Borno
Jeshi la Nigeria, linasema kuwa limewaua wapiganaji
150 wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram wakati wa msako
dhidi yao wiki jana.
Makabiliano yalitokea wakati jeshi lilipokuwa
linafanya msako dhidi ya wapiganaji hao katika jimbo la Borno Kaskazini
Mashariki mwa nchi.Katika taarifa yake, jeshi lilisema kuwa takriban wanajeshi 16, walifariki wakati walipofanya shambulizi la kwanza dhidi ya kambi ya wanajeshi hao ambako walipata silaha nzito
Wanajeshi wengine wa serikali wanasemekana kutojulikana waliko. Aidha jeshi lilisema pia liliweza kumuua kamanda wa wapiganaji hao Abba Goroma.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa, jeshi kwa kawaida huongeza chumvi idadi ya wapiganaji waliouawa kwa lengo la kuonyesha kuwa wanajeshi waliouawa kwenye mapigano walikuwa wachache.
Boko Haram ilianza harakati zake mwaka 2009 katika jimbo la Borno ambalo hadi sasa liko chini ya sheria ya hali ya hatari
TCRA WAANZA KUWANOA MA BLOGGERS TANZANIA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akiwasilisha
mada ya kwanza juu ya Ukubwa wa Sekta ya Mawasiliano hapa nchini wakati
wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers)
hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu
ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es
Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akifafanua jambo wakati wa Warsha ya
siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Bloggers) hapa
nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi wa Sekta ya Washangiaji na Watoa Huduma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Dkt. Raynold Mfungahema akiwasilisha
mada wakati wa Warsha ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando
(Bloggers) hapa nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa
Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza
B,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Viongozi na Bloggers wakiwa wanafuatilia kwa umakini Mafunzo
Baadhi ya Viongozi na Bloggers wakiwa wanafuatilia kwa umakini Mafunzo
Sehemu ya Wapiga Picha kutoka Vyombo mbali mbali vya habari wakiendelea na zoezi la kuchukua matukio mbali mbali wakati wa Warsha
ya siku mbili kwa wamililiki wa magazeti tando (Blogggers) hapa
nchini,iliyoanza rasmi leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,Uliopo eneo la Sinza B,jijini Dar es
Salaam.
Kutoka Kulia ni Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joesph Mwaisango akiwa na Blogger Rashid Mkwinda wakifuatilia kwa umakini mafunzo
Baadhi ya Bloggers wakifuatilia Jambo kwa umakini
Kutoka kushoto ni Fredy Anthony ambaye anatokea Blogs za Mikoa pamoja na Muwakilishi wa Full Shangwe Blog
Kutoka kushoto ni Dotto Kahindi kutoka Blog ya Tabia Nchi akiwa na Adela Kavishe
Mkurugenzi wa Google Africa Joe Mucheru akitoa mada wakati wa Mafunzo kwa Bloggers
Mmoja ya watoa Maada katika Maswala ya Mitandao ya Kijamii Liz Wachuka akizungumza jambo wakati wa Mafunzo kwa Bloggers.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akijibu Maswali ambayo yaliulizwa na Bloggers wakati wa semina hiyo
Meza kuu wakifuatilia Mada kwa umakini
Liz Wachuka Akijibu maswali yaliyo ulizwa na Bloggers
Afisa Habari wa TCRA Doris Saivoye akizungumza Jambo wakati wa Mafunzo kwa Bloggers.
Wabunge wa Nigeria wapigana bungeni
Wabunge wa bunge la waakilishi Nigeria wamerushiana ngumi wakati wa
vikao vya Jumanne baada ya kuzuka bungeni suitofahamu kuhusu mrengo wa
wabunge waliojitenga na chama tawala. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa
vyombo vya habari nchini humo.
Chama tawala cha PDP kimekuwa kikikumbwa na mgogoro wa ndani kwa muda sasa
Kituo kimoja cha kibinafsi cha televisheni, pamoja na vituo vingine
vilionyesha picha za mbunge mwanamke akimtosa kidole usoni kwa ghadhabu
mbunge mwenzake wakati mbunge mwanamume akionekana akichukua kiti nusura
kumgonga mwenzake.Wabunge wengine walionekana wakipigana ngumi.
Mgogoro inasemekana ulianza baada ya
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)