Jumamosi, 29 Novemba 2014

LIVE: KUTOKA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE...MH. RAIS AWASILI SALAMA NCHINI TANZANIA KUTOKA NCHINI MAREKANI KWA MATIBABU

Photo: #HABARI Rais Jakaya Kikwete awasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere akitokea nchini Marekani kwa matibabu. Apokelewa na wakazi wa DSM

Anaongea na waandishi wa habari pamoja na wananchi waliopo uwanjani 

@jmkikwete : Waambieni watanzania kuwa nimerudi na afya nzuri ingawa bado najiuguza sehemu niliyochanwa.

@jmkikwete : Nimefanyiwa upasuaji wa tezi dume, Tezi ambayo wanayo wanaume pekee wanawake hawana,si Busha kwa inavyosemekana 

@jmkikwete : Ni kawaida yangu kufanya uchunguzi wa afya, hata mwaka 1984 nilipotoka China, nilifanya ukaguzi wa vyote

@jmkikwete : Ni kawaida yangu kufanya uchunguzi wa afya, hata mwaka 1984 nilipotoka China, nilifanya ukagauzi wa vyote

@jmkikwete : Wasukuma wanaamini kuwa ni ugonjwa ule wa kula madafu, siyo hivyo

@jmkikwete : Tulishauriana na madaktari, tukakubaliana kufanya upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins ambao ni mabingwa

@jmkikwete : Kwa upande wangu hali niliyokuwa nayo ni hatua ya Kwanza ya Saratani ambayo inatibika kwa upasuaji 
 Rais Jakaya Kikwete awasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere akitokea nchini Marekani kwa matibabu. Apokelewa na wakazi wa DSM

Anaongea na waandishi wa habari pamoja na wananchi waliopo uwanjani

  • jmkikwete : Waambieni watanzania kuwa nimerudi na afya nzuri ingawa bado najiuguza sehemu niliyochanwa.

  • jmkikwete : Nimefanyiwa upasuaji wa tezi dume, Tezi ambayo wanayo wanaume pekee wanawake hawana,si Busha kwa inavyosemekana

  • jmkikwete : Ni kawaida yangu kufanya uchunguzi wa afya, hata mwaka 1984 nilipotoka China, nilifanya ukaguzi wa vyote

  • jmkikwete : Ni kawaida yangu kufanya uchunguzi wa afya, hata mwaka 1984 nilipotoka China, nilifanya ukagauzi wa vyote

  • jmkikwete : Wasukuma wanaamini kuwa ni ugonjwa ule wa kula madafu, siyo hivyo

  • jmkikwete : Tulishauriana na madaktari, tukakubaliana kufanya upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins ambao ni mabingwa

  • jmkikwete : Kwa upande wangu hali niliyokuwa nayo ni hatua ya Kwanza ya Saratani ambayo inatibika kwa upasuaji

BUNGE LILIGUBIKWA NA UTATA PALE AMBAPO SELIKARI ILISHINDWA KUTOA KAULI ZAKE ZA KUWAWAJIBISHA WASHUTUMIWA WA SAKATA LA ESCROW HAPO JANA..!

Vurugu hizo zilianza saa 04:42 usiku hadi saa 04:49 usiku wakati Spika Anne Makinda alipolazimika kuahirisha Bunge.
Dodoma. Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana usiku kilivunjika baada yavurugu kutawala ukumbini humo.
Vurugu hizo zilianza saa 04:42 usiku hadi saa 04:49 usiku wakati Spika Anne Makinda alipolazimika kuahirisha Bunge hadi leo saa tatu asubuhi.
Chanzo cha vurugu ni kutokana na ugumu wa kutokukubaliana na azimio la tisa, lililolenga kumwajibisha moja kwa moja Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Azimio la PAC lilitaka Waziri Muhongo aadhibiwe kwa kufukuzwa kazi kutokana na tuhuma zilizokuwa zinazomkabili ikiwamo kulidanganya Bunge.
Hata hivyo, baadhi ya wabunge wengi wakiwa wa CCM walitaka waziri huyo asiadhibiwe na Bunge bali achukuliwe hatua na mamlaka iliyomteua.
Wakati ubishani huo ukiendelea, ikiwa imefika saa 4.42 usiku Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisimama na Spika Makinda alimruhusu kuzungumza.
“Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, lakini leo (jana) kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi,” ilikuwa ni kauli ya Mbowe.
Mara baada ya kutoa kauli hiyo, wabunge wote wa upinzani walisimama na kuanza kupiga kelele kwamba wezi waondoke…tunataka fedha zirudi…tunataka fedha zirudi…vijana msilale…vijana msilale.

Jumatano, 26 Novemba 2014

SAMAHANI KWA TAARIFA NA PICHA HIZI...LAKINI WATAZAMAJI WA BLOG HII MNATAKIWA MFAHAMU!

 
daaah very sad...ajali mbaya ya magari makubwa iliyotoke mpakani mwa Congo DRC na Zambia
 


NEWS ALERT: MAHAKAMA KUU IMESIMAMISHA MJADALA WA RIPOTI YA ESCROW KUJADILIWA BUNGENI UPDATES:


Tumepata taarifa muda huu kutoka kwa mtu aliyeko Mahakama Kuu kuwa 
 
kutokana na taarifa iliyokuwa inaelezwa kuwa jopo la majaji watatu wa 
 
Mahakama Kuu watasikiliza kesi iliyofunguliwa na IPTL na PAP kuzuia bunge 
 
kujadili suala la Escrow.



Imeamriwa na Mahakama Kuu chini ya jopo la majaji watatu kuwa 
 
wamesimamisha mjadala wa Ripoti ya Escrow hadi hoja za msingi zitakapo 
 
fanyiwa kazi.
CHANZO: ITV TANZANIA