Ijumaa, 28 Februari 2014

IJUE AFRIKA KWA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227135608_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Maelfu ya wakimbizi ambao wamekuwa wakitoroka nchi ya Sudan Kusini kutokana na vita nchini humo wamehamia Uganda. Mpigaji Picha, Fredric Noy, anayefaifanyia kazi Idara ya wakimbizi ya Umoja wa mataifa, anatumia picha, kufarisia maisha ya ukimbizi ya Atem Angang na familia yake.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227135641_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
Mji wa Bor alimokuwa anaishi Matiop Atem Angang ndilo lililokuwa la kwanza kudhibitiwa na waasi pindi vita vilipozuka Sudan Kusini mnamo Desemba 15. Yeye pamoja na familia yake kubwa ya watu 15, akiwemo mamake wa miaka 95, watoto wake sita pamoja na familia ya dadake walitoroka kutoka nchini humo.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227135715_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
 Bor, mji mkuu wa Jimbo la Jonglei, umekuwa chini ya udhibiti ambao umekuwa ukibadilika kati ya waasi, na serikali mara kwa mara, na imewaacha watu wengi wakiwa wamepoteza maisha. Tangu makubaliano ya kusitisha mapigano kuafikiwa Januari, pande hizo mbili zimekuwa zikilaumiana. Familia ya Bw. Angang imesafiri kwa muda wa wiki moja kwa kutumia dau na lori ili kufika Uganda. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227135749_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
Mpakani, walipelekwa kwa kituo cha Shirika la Umoja wa Kimataifa linalotetea haki za kibinaadam lililoko Adjumani, kaskazini mwa nchi hiyo. Wananchi wengi wa Sudan Kusini wanatoroka nchi hiyo, na hii imekifanya kituo hicho kujaa wakimbizi wapya kila uchao. Umoja wa mataifa unasema kuwa takriban watu 860,000 wametoroka kutoka Sudan Kusini tangu kuibuka kwa vita nchini humo.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227141622_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
Lori linalowasafirisha wakimbizi kutoka Sudan, akiwemo Bw. Angang na familia yake, linavuka daraja kabla ya kufika kituo cha uhamiaji cha Dzaipi. Lori hizo husafiri hadi mara nne kwa siku kati ya mipakani na kituo hicho cha uhamiaji.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227135915_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
Maafisa wa Uganda wanajaribu kuondoa vifaa vya vita kutoka makao hayo, huku wakipekua vitu walivyonavyo wakimbizi wanaofika.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227140002_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
Mamake Angang’, Apiou Angar, ambaye ni mkongwe, anakutana na rafiki yake wa zamani wakiwa safarini. Bor, mji ambao ulikuwa unajivunia idadi ya watu 25,000, sasa umebaki mtupu.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227140034_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
"Hii familia ina bahati sana ikilinganishwa na zile ambazo itabidi zingoje kwa majuma mawili ili ziweze kuhama na kuenda kuanza maisha mapya katika makao mageni,” hii ni kulingana na Shirika la kutetea haki za kibinaadam la Umoja wa mataifa. Bw. Angang amepiga hema (kulia) kutumia vifaa alivyobeba kutoka Bor. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227140549_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
Famililia hii haijazoea makali ya baridi nyakati za usiku, ila walivumilia. Asubuhi ilipofika, akisaidiwa na mkalimani, Bw. Angang aliweza kuisajili familia yake na Shirika la msalaba mwekundu la Uganda.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227140826_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
Baada ya kulala chini ya hema ambayo haiwezi kuwakinga kutokana na makali ya baridi kwa siku mbili, watoto wake wanakuwa wagonjwa. Katika kituo cha afya kilichoko karibu, wahudumu wa afya nchini humo wamekuwa wakiwahudumia wagonjwa kwa masaa 12 kutokana na uongezekaji wa idadi ya wakimbizi
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227140905_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
Mpwa wa Bw. Angang ambaye ana miezi sita, Nyalet Deng, anachunguzwa na daktari wa kiliniki inayopata ufadhili kutoka kwa shirika la Medicines Sans Frontieres (MSF) iwapo anaugua utapiamlo. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227140942_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
Baada ya siku tatu katika kituo cha uhamiaji, familia hiyo inawasili katika makao ya Nyumanzi-mahala ambapo watapaita nyumbani pindi watakavyoendelea kuishi Uganda.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227141048_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
Wakati ambapo Bw. Angang na familia yake inangoja kando ya barabara kupewa kipande cha ardhi, wanapiga hema itakayowasaidia kujikinga dhidi ya makali ya jua la mchana.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/02/27/140227141126_trekking_uganda_976x549_bbc_nocredit.jpg
Bw. Angang anaugua malaria, na sasa itambidi bintiye wa miaka 18 kuendea chakula cha mwezi cha familia hiyo kutoka kwa Shirika la chakula duniani. Familia nzima ya Bw. Angang inangoja kwa matumaini iwapo majadialiano ya kusitisha vita nchini Sudan Kusini kati ya serikali na waasi mjini Addis Ababa, Ethiopia,yatavuna matunda.