Jumamosi, 6 Septemba 2014

DAAAH MWENYEZI MUNGU ATUNUSURU NA HIZI AJALI ZINAZOTOKEA MARA KWA MARA

samahani kwa picha hizi ajali iliyotokea jana huko Msoma na kuua watu 36 na kujeruhi wengine 76


Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Kilari Mkoani Mara likiwa limeumia vibaya sana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini Musoma leo  mchan.

Watu 36 wamepoteza maisha papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya sana.Kwa mujibu wa Ripota wetu aliyekuwa eneo la tukio,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni  kuwa Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni, hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.

Ndani ya gari hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.
Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
Umati wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 36 kupoteza maisha wakishuhudia tukio hilo la ajali.


Guldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.

Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
 
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.

Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokozi ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.

Jumanne, 2 Septemba 2014

KUNA VITU VYA KKUIGA LAKINI HIVI VINGINE DAAAAAH...TAZAMA MWENYEWE

Harusi ya kipekee ndani ya maji

Katika mtaa,mdogo wa Shanghai, kilichokuwa kiwanda cha kushona nguo sasa kimegeuka, ishara ya mabadiliko ya kuchumi yanayoshuhudiwa nchini China.
Katika eneo hili, wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi ndogondogo kujikimu kimaisha na hata kuuza bidhaa zao nje , lakini kazi mpya imeanza kufanyika hapa.
Biashara hii ni moja ya biashara ambazo zinasukuma uchumi wa China kwa kuwafanya watu kutumia pesa zao.
Duka lililofunguliwa hapa linaitwa Mr Wedding ...Biashara ndogo ambayo inawaajiri watu 16 ni sehemu ya sekta ambayo imekuwa ikinawiri kuliko nyinginezo katika historia ya nchi hii.
Kulingana na taarifa za serikali, soko la biashara za bidhaa za harusi , pesa zinazotumika kwa sherehe aina zote za harusi imekuwa kwa kasi na kuwa na thamani ya dola bilioni 130 kila mwaka.
Duka hili la Mr Wedding halijaachwa nyuma kwani nalo linataka kipande cha mapato kutoka kwa sekta hiyo. Tofauti ya biashara yake ni kwamba maharushi hupata huduma ya kipekee kutoka kwa duka lake.
'Mtindo tofauti wa picha'
''Watu wanaweza kupigwa picha ndani maji wakiwa katika hali yoyote, '' asema mmiliki wa duka hili Tina Liu.
"maharusi huonekana wakielea ndani ya maji, na picha hizi huwapendeza wengi sana. ''

Tina Liu mmiliki wa duka la Mr Wedding
Hawa ni wateja wake, Lin Enxiao na He Huan.
Ndoa yao haijawa tayari kwani wataoana mwaka ujao, lakini wapenzi wengi wachina wanasema wameamua kujipiga picha zao za harusi mapema ili wasipate tatizo lolote.
''Marafiki wetu wengi walijipiga picha katika eneo kavu,'' asema YY. "sisi tulitaka kitu tofauti. ''
Watu wanapofikiria kuhusu picha za harusi, wao hutaka kujipiga sehemu kavu kuliko kuta nyeupe au nyasi, '' asema Lamea.
"sisi tunahisi vyema kubadili mtindo huo.''

Sio mara ya kwanza kuona watu wakipigwa picha wakiwa ndani ya maji wala China sio nchi ya kwanza kuanzisha mtindo huu, ila China imeanza kuitumia kwa njia ambayo imewapendeza wengi.
'Vipodozi visivyoharibiwa na maji'
Kuna studio nyingi za picha zinazotoa huduma hii nchini China, soko lina ushindani mkali lakini baadhi ya wafanyabiashara hawana maadili ya kazi.
''Baadhi ya wafanyabiashara wana uelewa wa kazi na ni wabunifu lakini huwa hawadumu kwa sababu wanakosa maadili ya kazi. ''
Duka hili la Mr Wedding lina wabunifu wengi ambao huwa wanawapendekezea maharusi namna ya kupigia picha , wakitumia muda mwingi kuwapodoa na kuwapamba nywele maharusi.
"tunapendekeza bibi harusi akiwa ndani ya maji avalie gauni nyeupe na ndefu. Na sisi hutumia vipodozi ambavyo haviwezi kuharibiwa na maji. ''

Kisha maharusi hawa wanatembezwa na kuingizwa ndani ya tenki ya maji ambako wanapigiwa picha.
Tenki hiyo huwa na maji ya vuguvugu na mtu wa kuwasidia maharusi pia huwa ndani ya tenki hiyo ambamo wanapigiwa picha.
Tina alianza kazi hii mwaka 2003 wakati huo akipiga picha tu za kawaida za harusi kabla ya kuanza kuwapiga picha watu wakiwa ndani ya maji.
Kila biashara zina changamoto zake. Kwa Tina lazima awe na maarifa ya utenda kazi ili kazi yake iweze kunawiri.