Jumapili, 13 Oktoba 2013

MATUKIO KATIKA PICHA

WANAFUNZI WA SHULE MBALIMBALI ZA SEKONDARI JIJINI DAR ES SALAAM WALIVYOSHEREHEKEA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI
KIUNGO WA SIMBA NASSORO MASOUD SAID "CHOLLO" AKIWANIA MPIRA DHIDI YA KIUNGO WA PRISON YA MBEYA JEREMIAH MGUNDA MCHEZO WA LIGI KUU ULIOFANYIKA JANA UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM
SIMBA WALITOKA KIFUA MBELE KWA BAO 1-O.

HIVI NDIVYO INDIA ILIVYOHARIBIWA NA KIMBUNGA

Kimbunga Phailin kikipiga Orissa na Andhra Pardesh
Maafisa wa India wanaoshughulika na kazi za uokozi wameanza shughuli zao baada ya Kimbunga Phailin kupiga majimbo ya mashariki na kusababisha mafuriko kwenye miji na vijiji.

Wakuu wanasema wasaidizi wametumwa maeneo yaliyopigwa na kimbunga katika majimbo ya Orissa na Andhra Pardesh, kuwaokoa wale wanaofikiriwa wamenasa chini ya vifusi.
Miti iliyoporomoka imeuwa kama watu saba.

Lakini waandishi wa habari wanasema matayarisho na operesheni kubwa iliyofanywa ya kuwahamisha watu kabla ya kimbunga, imenusuru maisha.

Uharibifu uliotokea bado haujulikani kwa ukamilifu na waya za umeme na mawasiliano zimekatika katika maeneo mengi.
Kimbunga cha mwaka 1999 kiliuwa watu 10,000 katika jimbo la Orissa.