Jumatano, 23 Oktoba 2013

HIVI UNAJUA KUWA MAPENZI NA NDOA HAZINA UKOMO?

MBUNGE CCM AOLEWA NA KINDA
MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rosweeter Kasikila (60), amejikuta kwenye kashfa nzito ya kufunga ndoa na kijana, kinda wa miaka 26, Michael Christian.
Ndoa hiyo ambayo ilifungwa katika Kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG), linaloongozwa na Mchungaji Getrude Rwakatare ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM, imebaki kuwa gumzo na kuwaacha hoi baadhi ya mawaziri, wabunge wanaoifahamu pamoja na majirani wanaoishi na mbunge huyo.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya wanandoa hao na majirani wanaowazunguka, vililiambia gazeti hili kuwa ndoa hiyo ilifungwa Septemba Mosi mwaka 2011, na imebaki kuwa siri kabla ya wawili hao kukorogana.
Kabla ya wawili hao kuamua kufunga ndoa, mbunge huyo kutoka mkoani Rukwa, mwenye makazi yake Bagamoyo mkoani Pwani, alikuwa akimtumia Michael kwenye shughuli mbalimbali na muda wote alikuwa akiishi nyumbani kwa mbunge huyo.
Inaelezwa kuwa mbunge huyo ambaye ana familia ya watoto wawili ambao kiumri wanalingana na Michael, alianza uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo kwa siri kubwa na baadaye alifanikiwa kumshawishi wafunge ndoa huku akimuahidi kumpa huduma mbalimbali anazotaka.
Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao waliamua kufunga ndoa katika Kanisa la TAG baada ya mbunge huyo kufanikiwa kumshawishi Mchungaji Rwakatare kwamba ndoa hiyo itakuwa siri, hasa kutokana na tofauti ya kiumri kati yao.
Hata hivyo ndoa hiyo kwa sasa imekumbwa na mgogoro mkubwa, huku mbunge huyo akidaiwa kuzuia kila kitu cha mumewe huyo, hasa vyeti vyake vya shule kama njia ya kumbana warudiane.

JE, SHEREHE ZA HARUSI HAPA TANZANIA ZIKOJE? TAZAMA HAWA WENZENU

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/22/131022142327__70620118_gg_weddingguests_13-1.jpg 
Glenna Gordon anasema: "harusi za Nigeria ni sawa na ilivyo nchi yenyewe ya Nigeria: Kubwa, Zenye kelele na zenye furaha tele. Muziki pia ni wa sauti ya juu na chakula ni kizuri sana. Hakuna kilicho kimya Nigeria na hiyo bila shaka ni kweli ya harusi. ''
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/22/131022142525__70625898_gg_weddingguests_17.jpg 
''Baadhi ni kubwa zilizogharimu pesa nyingi na nyengine ni za kufurahisha,'' anasema mpiga picha huyo ambaye amefanya kazi katika maeneo mengi ya Afrika.  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/22/131022142544__70625900_gg_weddingguests_02.jpg 
Licha ya hali, kila mtu hujitosa uwanjani akiwa amevalia mavazi yake mazuri zaidi  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/22/131022142412__70620130_gg_weddingguests_09-1.jpg 
"wageni kwenye harusi hizo huvalia vyema tu kama bibi harusi. Nyingi ya harusi hizo pia huwa na watu waliovalia mfano wa mavazi ya nyumbani au aso-ebi katika lugha ya Yoruba, moja ya lugha maaruufu wanazoongewa watu katika maeneo ya Kusini.''  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/22/131022142425__70620131_gg_weddingguests_04-1.jpg 
"marafiki wa bibi harusi wote huvalia nguo za kufanana, marafiki za mamake huvalia nguo tofauti na marafiki za mume pia hufanya hivyo.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/22/131022142442__70620132_gg_weddingguests_03-1.jpg  
''Kutumia simu yangu ya iPhone ilinisaidia sana kwa sababu kutumia kamera kubwa inaweza kuleta kuzuizi kati ya mwenye kupigwa picha na kamera''
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/22/131022142458__70620133_gg_weddingguests_07-1.jpg
Nilitaka kitu binafsi kuwezesha wenye kupigwa picha kukutana na wageni na kuwapiga picha wakiwa katika mazingira yale ya sherehe.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/22/131022142513__70620134_gg_weddingguests_16-1.jpg
Unaweza kuona picha zaidi za Gordon kwenye istaghram yake @glennagordon.