Jumatatu, 30 Septemba 2013

CHUO KILICHOVAMIWA NIGERIA KILIKOSA ULINZI

mauaji ya Nigeria

mauaji ya Nigeria 

Maafisa wa utawala nchini Nigeria wanasema kuwa hapakuwa na ulinzi katika chuo cha mafunzo ya kilimo nchini Nigeria ambako hadi wanafunzi 50 waliuawa Jumapili.
Wanafunzi waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu katika mabweni yao katika jimbo la Yobe , Kaskzini Mashariki mwa Nigeria.
Afisaa mmoja aliambia BBC kuwa serikali itashirikiana na jeshi kuhakikisha kuna ulinzi katika shule.

HALI YA WASIWASI KENYA YATANDA...SERIKALI YATAKA WAKIMBIZI WAONDOLEWE


Kambi ya wakimbizi ya Dadaab, Kenya

Kamati ya bunge inayohusika na ulinzi na uhusiano na mataifa ya kigeni imependekeza kufungwa kwa kambi za wakimbizi nchini Kenya, ikisema zinatishia usalama wa nchi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndungu Githinji amesema kuwa wana habari kuwa kambi zilizoko kwenye mipaka ya Kenya hutumika kuwapa mafunzo wapiganaji wa kiislamu.
Kenya inahifadhi wakimbizi wa kisomali zaidi ya nusu milioni katika kambi za Dadaab zilizoko kwenye mpaka na Somalia.

WALIOSHIRIKI MJADALA SPESHELI WA WESTGATE JINSI GANI WAKENYA WANAKABILIANA NA MASHAMBULIZI YA KIGAIDI

 http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/29/130929102537_sk_westgate_special_06_976x549_bbc_nocredit.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/29/130929102924_sk_westgate_special_07_976x549_bbc_nocredit.jpg
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/29/130929102418_sk_westgate_special_05_976x549_bbc_nocredit.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/29/130929102045_sk_westgate_special_02_976x549_bbc_nocredit.jpg
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/29/130929102206_sk_westgate_special_03_976x549_bbc_nocredit.jpg
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/09/29/130929101915_sk_westgate_special_01_976x549_bbc_nocredit.jpg

MATUKIO KATIKA PICHA

SIMBA FC v JKT RUVU...AMRI KIEMBA AKIWANIA MPIRA DHIDI YA NASHON NAFTALI WA JKT RUVU UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM JANA JUMAPILI.
SIMBA WALIIBUKA NA USHINDI WA MAGOLI 2-O
MITAA YA KUNDUCHI KANDO KANDO YA NEW BAGAMOYO WATU WAKIENDELEA KUJENGA NA KUFANYA SHUGHULI ZA MACHIMBO LICHA YA SERIKALI KUZUIA KUFANYA HIVYO

LIGI KUU BARA..SIMBA YANG'ARA NA KUKAA KILELENI, TANZANIA PRISON NA AZAM ZACHOSHANA NGUVU UWANJA WA SOKOINE MBEYA 29/09/2013

 TIMU ZOTE MBILI ZIKIPASHA MISULI UWANJA WA SOKOINE MBEYA
 TANZANIA PRISON FC
 WACHEZAJI WA AZAM FC WAKIELEKEA KWENYE VYUMBA VYA KUBADILISHIA NGUO
 VIKOSI VYA TIMU ZOTE MBILI KAMA VINAVYONEKANA

 WACHEZAJI WA AZAM FC WAKIWA NI WAGENI WA PRISON WAKIJIANDAA KUPITA NA KUWASALIMIA WACHEZAJI WA PRISON
 MPIRA UMEANZA
 JUKWAA KUU LA UWANJA
 MASHABIKI WA TANZANIA PRISON WAKIFUATILIA MCHEZO KWA MAKINI
 GOLIKIPA WA AZAM AKIWA CHINI BAADA YA KUFANYIWA MADHAMBI
PRISON WAKISHANGILIA BAADA YA KUZIFUMANIA NYAVU ZA AZAM KUPITIA MCHEZAJI WAO MAHILI PETER MICHAEL
 PETER MICHAEL AKIWASOGELEA MASHABIKI KWA FURAHA
 WACHEZAJI WA AZAM FC WAKIWA WAMEDUWAA WAKIWA HAWAAMINI KILICHOTOKEA
 SHANGWE KWA UPANDE WA MASHABIKI WA PRISON ZATAWALA

 DAKIKA 45 ZA AWALI TIMU ZIKIWA ZINATOKA NJE YA UWANJA NA PRISON WAKIWA MBELE KWA BAO MOJA LA KUONGOZA
 DAKIKA YA 55 KIPINDI CHA PILI KIPRE TCHETCHE AKIWASAWAZISHIA GOLI TIMU YAKE YA AZAM
 WACHEZAJI WA AZAM WAKISHANGILIA GOLI LILILOFUNGWA NA KIPRE TCHETCHE
 MCHEZO ULIENDELEA KWA TIMU ZOTE MBILI ZIKILISAKAMA LANGO LA MWENZAKE BILA MAFANIKIO
 WACHEZAJI WA PRISON WAKIMZONGA ZONGA REFA
 DAKIKA ZIKIWA ZIMEBAKI ZA MWAMUZI WENYE ROHO NYEPESI WAKIJIANDAA KUTOKA NJE YA UWANJA
 HADI MWISHO WA MCHEZO TANZANIA PRISON 1-1 AZAM FC KUTOKA KULE JIJINI DAR ES SALAAM NA KUACHA UWANJA HUU WA SOKOINE KUENDELEA KUTAWALIWA NA DROO ZA KILA MCHEZO

PICHA ZOTE NA : MWANDISHI HURU