Ijumaa, 5 Desemba 2014

NAWEZA KUSEMA SIKU ZA KUFUNGA MWAKA HUWA NA MAMBO MENGI....HII NI AJALI ILIYOTEKEA HIVI PUNDE ENEO LA MLIMA NYOKA HAPA MKOANI MBEYA

Lori la Mafuta lenye namba za Usajiri T332 AGA ambalo Dereva wake Godfrey Lyimo (33) alikuwa amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi, Hapa Lori hilo la mafuta liliwa Limepinduka.

Basi la Mbukio Missio muda mfupi baada ya kupata ajali ambayo ilisababishwa na Dereva wa Basi hilo, Hapa vijana wakiwa wamechukua magazeti wakificha jina la Basi hilo lisitambulike kwa wale wanaokuja kushuhudia ajali hiyo, Nia na lengo la kufanya hivyo haijafahamika mpaka sasa.
Baadhi ya Abiria , Washuhudiaji pamoja na Askari wakiwa eneo la Mlima Nyoka ambapo ajali ilipo tokea
Watu 50 wamenusurika kifo baada ya basi la Mbukio Mission waliokuwa wakisafiria kugongana na lori la mafuta katika eneo la Mlima Nyoka hapa mkoani Mbeya hivi karibuni...
Chanzo na ITV Tanzania

Jumatano, 3 Desemba 2014

HIPI PUNDE....MLIPUKO MKUBWA WATOKEA HUKO MOGADISHU-SOMALIA

 
Mlipuko mkubwa umetokea katika mji wa Mogadishu nchini Somali karibu na uwanja wa ndege.
Duru zimearifu kuwa mlipuko huo huenda umesababishwa na mtu aliyejitolea muhanga aliyejilipua ndani ya gari.
Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al- Shaabab mara kwa mara hutumia milipuko ya magari, lakini kufikia sasa halijakiri kuhusika na mlipuko huo.
Haijajulikana ni watu wangapi wameuwawa.

CHANZO NA: BBC SWAHILI

Aliyewakosoa Sasha na Malia ajiuzulu...!

Sasha na Malia walikosolewa kwa kuvalia sketi fupi mbele ya umati katika White House
Mfanyakazi katika chama cha Republican nchini Marekani amejiuzulu baada ya kukosolewa kwa kuwatuhumu wanawe Rais wa Marekani Barack Obama , Sasha na Malia kwa kuwaambia kuwa wamekosa ustaarabu.
Elizabeth Lauten, afisaa mkuu wa mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher, alijiuzulu Jumatatu.
Bi Lauten, aliwakosoa watoto wa Obama Sasha na Malia kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya watoto hao kuonekana wakiwa wamevalia sketi fupi kwenye hafla ya jioni.

Rais Obama na mkewe wamejitahidi sana kuwalinda watoto wao kutokana na ndimi kali za vyombo vya habari
Baadaye Lauten alifuta maandiko yake ambayo baadaye aliyataja ya kuumiza moyo na kuudhi.
Bi Lauten pia alikuwa amewakosoa Sasha na Malia kwa kusema walionekana wasio na furaha walipokuwa wamesimama na baba yao katika hafla ya maankuli katika Ikulu ya White House.
Wakati watu wengi walihisi kwamba Sasha na Malia hawakua na furaha kuwa na baba yao katika hafla ile na hata kulizungumzia swala hilo kwenye mitandao ya kijamii,Bi Lauten aliamua kujitoa
kimasomaso na kuwakosoa wasichana hao kupitia kwa Facebook.

Sasha na Malia ni miongoni mwa vijana wadogo sana kuwahi kuwa katika ikulu ya White house
Mwanamke huyo akiomba msamaha, alisema baada ya kufanya maombi na hata kuzungumza na wazazi wake na kisha kusoma maandiko yake kuwahusu Sasha na Malia, alihisi kweli aliwakera wasichana hao.
"ningependa kuomba radhi kwa wote niliowaudhi kwa matamshi yangu, na nina ahidi kujifunza na kubadilisha mwenendo wangu, '' alisema Lauten.

chanzo na BBC Swahili

Jumanne, 2 Desemba 2014

JIONEE MOJA YA VIVUTIO VIKUBWA VYA KITALII KISIWANI PEMBA...HAPA NI PICHA ZA HOTEL YA KISASA KABISA ILIYOPO CHINI YA BAHARI

 


 

 


Kisiwa cha Pemba nchini Tanzania kimekuwa maarufu kwa kilimo cha karafuu visiwani Zanzibar kwa miaka mingi tangu enzi za utawala wa Kiarabu visiwani humo.
Hata hivyo zao hilo limekuwa likikumbwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za kushuka kwa bei ya karafuu katika soko la dunia na hivyo kuathiri uchumi wa Zanzibar.
Katika kukabiliana na hali hiyo, serikali ya Zanzibar imekuwa ikitilia umuhimu sekta ya utalii, ambapo huko kisiwani Pemba kumejengwa hoteli ya aina yake, ambayo moja ya vyumba vyake kimejengwa chini ya bahari.
PICHA NA:Mwandishi wa BBC Salim Kikeke alitembelea hoteli hiyo.

Jumatatu, 1 Desemba 2014

JE, INATOSHA TU KUWAWAJIBISHA WAHUSIKA WA SAKATA LA ESCROW? MIMI SIJUI..WATANZANIA WANA MAJIBU ZAIDI!

 
 Waziri mkuu Mh. Mizengo P. Pinda.

Bunge la Tanzania mwishoni mwa wiki limehitimisha mkutano wake wa 17 ambao pamoja na mambo mengine lilijadili taarifa maalum ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC kuhusu taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na miamala iliyofanyika katika akaunti ya ESCROW ya TEGETA pamoja na umiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL na kutoa maazimio juu ya sakata hilo.
Miongoni mwa maazimio manane ya Bunge ni kuchukuliwa kwa hatua za kisheria dhidi ya watu wote watakaobainika kuhusika na upotevu wa fedha hizo, kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 300 zilichotwa katika akaunti hiyo iliyokuwa iliyokuwa kwenye Benki Kuu ya Tanzania na ikimilikiwa kwa pamoja na IPTL na Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO.
Baadhi ya viongozi na maafisa wa serikali kama vile mawaziri, majaji, wabunge, wenyeviti wa kamati za Bunge, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi wanatuhumiwa kunufaika na mabilioni ya fedha kutoka akaunti ya Escrow na hivyo hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao kwa mujibu wa sheria za nchi.
Pia wabunge wametaka mikataba mibovu ya kuzalisha umeme kati ya TANESCO na makampuni binafsi ya kufua umeme iwasilishwe bungeni au kamati zake kwa lengo la kutekeleza vyema wajibu wake wa kuisimamia na kuishauri serikali.
Kwa miaka mingi TANESCO imekuwa ikilalamika kulipa gharama kubwa za umeme na kusababisha kupanda kwa gharama za matumizi ya nishati hiyo hapa nchini.

Endelea kufuatilia!