Alhamisi, 3 Oktoba 2013

BREAKING NEWS..NDEGE YA ABIRIA YAANGUKA NIGERIA NA KUUA WATU WATANO



Ndege iliyokuwa imewabeba watu 27 imeanguka baada ya kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mjini Lagos.
Duru zinasema kuwa watu 5 wamefariki huku shughuli ya uokozi ikendelea na mtu mmoja akipata matibabu kwa majeraha mabaya aliyopata.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Associated Airlines, iliyokuwa na uwezo wa kubeba watu 30 ilianguka muda mfupi tu baada ya kuruka na kulipuka.
Aidha ilikua inaelekea mjini Akure Kusini Magharibi mwa nchi, kwa mujibu wa msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani nchini humo.

TAZAMA NDEGE NDOGO ILIYOANGUKA GONGOLAMBOTO DSM MAPEMA MCHANA WA LEO

Ndege ndogo ya Kampuni ya Aslum imeanguka eneo la Gongolamboto DSM ikiwa kwenye mafunzo ya vitendo kwa mwanafunzi wa urubani.Ndege hiyo ilikuwa na rubani 1 na mwanafunzi 1.

MATUKIO KATIKA PICHA

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA (KULIA) AKIPOKEA MWENGE WA UHURU KUTOKA KWA MWAKILISHI  WA WILAYA YA MBEYA  DR. NORMAN SIGALA TAYARI KWA KUUKIMBIZA KATIKA WILAYA YA MBOZI NA BUSEKELO MKOA WA MBEYA
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKIWAHUTUBIA WANANCHI WA HUKO KIJIJINI KAGUNGA KATIKA ZIARA YAKE MAALUM MKOANI KIGOMA.
WAZIRI MKUU AKIWAPUNGIA MKONO WANANCHI WA KIGOMA MARA TU YA KUWASILI KWENYE UWANJA WA NDEGE KIGOMA KUANZA ZIARA YAKE  MAALUM YA SIKU SITA. WAZIRI AMEONGOZANA NA MKEWE  MAMA TUNU PINDA (NYUMA YAKE), MKUU WA MKOA WA ISSA MACHIBYA (KUSHOTO) NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA KIGOMA DR. AMAN WALLD KABOUROU (KULIA)


PIKIPIKI ILIYOTENGENEZEWA MWAMVULI MAALUM IKIWA IMEBEBA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI  KATIKA BARABARA YA MOROGORO JIJINI DAR ES SALAAM
SHEKHE PONDA ISSA PONDA AKIINGIA KATKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI  MOROGORO 
MAKAMU WA RAIS, DR. MOHAMED GHARIB BILALI (KUSHOTO) AKISALIMIANA NA WAZEE WALIOHUDHURIA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WAZEE DUNIANI KITAIFA MAADHIMISHO HAYO YALIFANYIKA MKOANI TANGA KATIKA MJI WA KOROGWE.