Bao la kwanza la Ujerumani lilipokewa kwa vifijo na nderemo na mashabiki
waliokuwa wamejaa pomoni kushuhudia timu yao ikimenyena na mabingwa
mara sita wa kombe la dunia Brazil
Mechi hii ilikua ya kwanza ya nusu fainali katika kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil
Wengi wamesema wachezaji wa Ujerumani walikuwa 'balaa' yaani walikuwa wakali katika mechi hiyo
Kipa wa Ujerumani hakuwa na chochote cha kufanya kwani hali ilikuwa ngumu kweli.
Ilikuwa sherehe kila pembe ya dunia kutoka kwa mashabiki wa Ujerumani na
hata nyumbani baada ya timu yao kuingiza mabao matano katika dakika za
kwanza 29 za mechi hiyo
Mabao yaliendelea kuingizwa hadi yakafika saba mwishoni mwa mechi.
Brazil hata hivyo walikomboa bao moja la kupanguzia machozi, ila
halikutosha kuondoa aibu waliyoipata katika mchuano huu ambao umewaacha
wengi vinywa wazi
Mashabiki wa Brazil walikuwa wanajionea giza uwanjani magoli yakiingizwa na Ujerumai kutoka pembe zote za uwanja
Ujerumani sasa watajiandaa kumenyana na mshindi wa mechi kati ya Uholanzi na Argentina Brazil itasalia kupigania nafasi ya tatu
Huzuni ulitanda Brazil na kote duniani kwa mashabiki wa Brazil
Lakini nahodha wa muda wa Brazil David Luiz amewataka mashabiki wa timu
hiyo kote duniani kuwasamehe wachezaji waliokuwa uwanjani
Selecao,walipoadhibiwa kichapo cha mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi
ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Kwa sasa hadi fainali za kombe la dunia ni sherehe kote kote nchini Ujerumani
ENDELEA KUFUATILIA MATUKIO ZAIDI YA KOMBE LA DUNIA KUPITIA HAPAHAPA BLOG YA KIJANJA
NITAWALETEA TENA MATUKIO YA BRAZIL KUTAFUTA NAFASI YA TATU AMA YA NNE!