Jumatatu, 4 Novemba 2013

TUFANYE NINI JUU YA DRC NA WAASI WA M23?

MAPIGANO MAPYA YANAENDELEA HUKO DRC  KATI YA MAJESHI YA M23 NA SERIKALI YA DRC
 
Maelfu ya wananchi wamelazimika kutoroka makwao kutokana na mapigano makali yanayoendelea mpakani mwa DRC na Uganda
Mapigano makali yamezuka kati ya majeshi ya serikali ya Congo na waasi wa M23 katika mpaka wa mashariki na taifa la Uganda.
Mapigano makali yameripotiwa kutokea wakati majeshi hayo ya serikali yanapojaribu kuchukua udhibiti wa maeneo yaliosalia mikononi mwa waasi wa M23.
Mwandishi wa BBC Issac Mumena aliyeko katika eneo hilo la mpaka wa Uganda na DRC anasema kuwa mapigano hayo yamesababisha maelfu ya wakimbizi kuvuka na kuingia nchini Uganda kutafuta usalama na matibabu kwa wale waliojeruhiwa.
Waasi wa M23 mnamo siku ya Jumapili walitoa wito kwa wapiganaji wao kusitisha vita ili kuruhusu mazungumzo ya amani kufanyika kati ya viongozi wa kundi hilo na waasi hao.
Hata hivyo, kwa mujibu mwa mwandishi wa BBC hakuna dalili ya kufanyika mazungumzo ya amani.
Anasema kuwa hali ni tete sana katika eneo la mpakani.
Inaarifiwa kuwa waasi hao wanaonekana kujibu vikali mashambulizi makali kutoka kwa wanajeshi wa serikali na hali ni mbaya kuliko siku za awali, na taarifa zinasema kuwa wanajeshi wanakaribia kushinda vita vyao dhidi ya waasi hao.
Mapigano ya hivi sasa yanakuja baada ya wanajeshi wa serikali kudhibiti baadhi ya miji iliyokuwa imetekwa na waasi hao baada ya kuwafurusha.

WATANZANIA TUNATAKIWA KUOMBA UKATILI WA KUTUPA WATOTO NAMNA HII UTOKOMEZWE

PICHA HII NI MTOTO ALIYETUPWA NA MAMA WA MTOTO AMBAYE AKUWEZA

KUJULIKANA MARA
MOJA USIKU WA KUAMKIA LEO ENEO LA NDANYELA  JIJINI MBEYA


 BAADHI YA WATU WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO

HILI NDILO ENEO ALILOTUPWA KICHANGA HUYO

PICHA NA Free Media to Blogs

KUFAIL MTIHANI SIYO KUFAIL MAISHA...ONA JINSI MWANAFUNZI ALIVYOJINYONGA HADI KUFA KUOGOPA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE

 
Mwanafunzi aliyekuwa akisoma  shule  ya  sekondari  Sabasaba  mjini  Iringa akijiandaa kurudia  kufanya  mtihani  wa  taifa  wa kidato  cha nne kupitia  kituo  cha Krelluu mjini  Iringa Khamis Mkundo  mkazi  wa Mwangata  C katika manispaa ya  Iringa amejiua kwa kujinyonga  kwa kamba kwa kile  alichodai  kuchoshwa na kufeli  mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.

Katika  barua  yake  ndefu aliyoiandika  kijana  huyo amesema  kuwa amefanya  hivyo si kwa kujipendea  ila amechukizwa na hatua yake ya  kufeli mara kwa mara  hivyo  kuamua  kujiua ili  kuepuka aibu katika mtihani ujao ambao anaamini angefeli.

Shemeji  wa  kijana  huyo Aden Tagalile ameueleza mtandao  matukiodaima.com  kuwa  tukio  hilo limetokea mida ya saa 12 na saa 1  usiku wa  leo baada ya kuwepo kwa mazungumzo ya muda  mrefu  kwa kijana  huyo kuonyesha kuchukia hatua yake ya kuendelea kuristi  mtihani  wa kidato cha nne  bila mafanikio.

Kijana huyo  alisema hajapenda  kuona anaendelea  kufeli na kuwa  yupo tayari kwa lolote  kukwepa aibu ambayo ipo mbele  yake.
 
Hata  hivyo kufuatia mazungumzo hayo, kijana huyo aliagana na ndugu zake akiwemo kaka  yake anayeishi nae kwa kila mmoja kuondoka nyumbani  hapo kabla  ya kijana  huyo kukutwa amejinyonga.

Mwenyekiti  wa serikali  ya mtaa huo Sarehe Mgimwa amethibitisha  kutokea kwa kifo  hicho na kuonyesha ujumbe ambao kijana  huyo ameuacha .
 
 
 
 
HII NI BARUA ALIYOIANDIKA KABLA HAJAJINYONGA AKIWATAJA BAADHI YA 

MARAFIKI NA WAZAZI WAKE AKIWATAKIA MAISHA MEMA 

CHANZO..Matukio Daima.com

M23 YAWATAKA WAFUASI KUSITISHA MAPIGANO

Wanajeshi wa serikali ya DRC katika vita dhidi ya M23 
Kiongozi wa wapiganaji wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ametangaza kuwa watasitisha mapigano katika vita vyao na jeshi la serikali.

Bertrand Bisimwa alisema kwenye taarifa kwamba anawasihi wapiganaji wote haraka waache uhasama na wanajeshi, ili kuwezesha mazungumzo ya amani kuendelea.

Wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, hivi karibuni wamewasukuma nyuma wapiganaji na kuwatoa katika ngome zao nchini.

Mazungumzo ya amani yanafanywa mjini Kampala, Uganda.