Jumatatu, 18 Agosti 2014

EBOLA...WAGONJWA WALIOTOROKA WATAFUTWA



Mmoja wa wanaume waliovamia kituo hicho na kumbeba mgonjwa
Kituo kilichotengwa na kuwekewa kwa sababu ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola, kimeshambuliwa na zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.
Watu kama 20 hadi 30 waliowekwa hapo kuangaliwa kama wana dalili za Ebola walitoroka baada ya kituo hicho kuporwa Jumamosi usiku.
Kituo kiko kwenye mtaa wa West Point, wenye wakaazi wengi.
Washambuliaji walipora magodoro na vitu vingine.
Mwandishi wa BBC katika kanda hiyo anasema pengine washambuliaji walikerwa kuwa kituo hicho kimewekwa katika mtaa wao.
Mafisa wakuu nchini Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.