KENYA YAMSAKA SAMANTHA LEWTHWAITE
Polisi wa kimataifa Interpol, wamemuweka mwanamke aliyeshukiwa kuongoza
mashabulizi ya kigaidi nchini Kenya raia Muingereza Samantha Lewthwaite,
kwenye orodha ya watu wanaosakwa
sana duniani.
UN YAJADILI AZIMIO KUHUSU SYRIA
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linajadili rasimu ya azimio kuhusu
silaha za kemikali za Syria baada ya Marekani na Urusi kukubali
mapendekezo ya azimio hilo.
AFUNGWA MIEZI SITA JELA KWA WIMBO WA MATUSI TUNISIA
Msanii wa kizazi kipya nchini Tunisia, Ahmed Ben Ahmed, anayejulikana
kwa jina la kiusanii, Klay BBJ, amehukumiwa jela kwa miezi sita kwa
kuwatusi maafisa wakuu kupitia kwa
muziki wake.