Zaidi ya miaka 10 tangu kuzuke mapigano Darfur zaidi ya wenyeji milioni mbili wamelazimika kutoroka makwao
Hamisa alitoroka nyumbani kwake mwaka wa 2003 baada ya wavamizi
kuwashambulia na bunduki.Alitorokea milimani akiwa amembeba mmoja wa
wajukuu wake
Ukulima ndio uti wa mgongo wa Wasudan Kusini.Kukuibuka vita mifugo mimea na mali ya watu huporwa na kuharibiwa.
Kuna zaidi ya kambi 27 katika eneo la kati la Darfur
Kufuatia mapigano yaliyodumu kwa muda mrefu sasa wakimbizi wameanza
kujenga nyumba za kudumu katika kambi hizo za wakimbizi wa ndani kwa
ndani
Amina (aliyevalia nguo ya kijani kibichi)anaonekana hapa miaka 7 iliyopita katika kisima cha Khamsa.
Bado tunakabiliwa na changamoto tele baada ya kuishi hapa kwa zaidi ya
miaka 10''anasema Amina ambaye mwenyewe anamtoto mwenye umri wa miak 9
Kupata mapato kambini ilikuwa ngumu sana wakati huo kwa Yusuf ambaye alikuwa amejifunza kuoka mikate .
Kwa sasa ameoa na anafamilia ya watoto watatu.
Haja akiwa na kifunga mimba wake Horan mwaka wa 2007 katika kambi ya Hassa Hissa
Licha ya kuhama kutoka mako moja hadi mengine maisha bado ni yaleyale tu
kwa Haja sasa yeye pamoja na wajukuu wake ni vijakazi wa nyumbani.
Rawia alitoka kwakwe mikono mitupu pamoja na mumewe na wanawe .Alikuwa ni mabaki ya chakula na pipa la kutekea maji.
Mapigano haya huko Darfur yanapembe tofauti kwa hivyo ni vigumu kusuluhisha.
Kuna wale wanaopigana na serikali,kunawale wanaopigana kwa misingi ya Dini.
Kwa mujibu wa UN zaidi ya watu 390,000 walitoroka makwao mwaka huu.
Mkataba wa kusitisha mapigano ya mwaka wa 2011 haukudumu kwani waarabu hawaamini wakristu weusi ambao wengi ni wakulima.
Wanawake wa Darfur wakijipaka Hinna tayari kwa hserehe kambini.
Viongozi wa jamii wanapewa heshma lakini wanasema ukosefu wa ajira
umepelekea vijana kuwapuuza na wakati mwengine hata kuwakaidi.
endelea kutembelea blog yako ya kijamii inayokuletea matukio yanayoikumba jamii kwa ujumla