Jumatatu, 18 Novemba 2013

SEMA KENYA NI MOJA YA PROGRAMU NZURI SANA INYAOFANYIKA KENYA KWA UDHAMINI WA BBC..ONA HII HAPA

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/17/131117131846_skembubehindscenes_pict_1_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Sema Kenya ni kipindi cha mjadala kinachoangazia maswala ya utawala na maendeleo.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/17/131117132035_skembubehindscenes_pict_2_976x549_bbc_nocredit.jpg
Kipindi hiki kinahakikisha wananchi wa kawaida wanapata jukwaa la kuuliza viongozi wao maswali tata, ana kwa ana.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/17/131117132208_skembubehindscenes_pict_3_976x549_bbc_nocredit.jpg
Utafiti na ubora wa kipindi ni wa hali ya kipekee.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/17/131117133034_skembubehindscenes_pict_5_976x549_bbc_nocredit.jpg
Kipindi kimeweza kutamba kote nchini kutokana na utaalam ulipo kwenye uandalizi.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/17/131117133224_skembubehindscenes_pict_6_976x549_bbc_nocredit.jpg
Muda mwingi unatumiwa kurekodi na kusimulia kipindi hiki ili kueleza mambo kama yalivyo.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/17/131117133559_skembubehindscenes_pict_7_976x549_bbc_nocredit.jpg
Kila kinapopeperushwa, kipindi hiki kinazidi kuboreshwa ili Wakenya wazidi kujadiliana na viongozi wao, kusudi utawala bora ufikiwe.

HII NDIYO AJALI ILIYOTOKEA MAENEO YA WAMI MKOANI MOROGORO

 
Ajali mbaya ya noah iliyotokea alfajiri leo eneo la Wami ranch,Sokoine,barabara kuu ya Moro- Dodoma.Ambapo watu Saba wamefariki na wengine kujeruhiwa

MAAFA YA KIMBUNGA YAIKUMBA MAREKANI

 
kimbunga nchini Marekani chasababisha uharibifu mkubwa
Kimbunga kikali kimeyakumba maeneo kadha ya Marekani, kikiharibu majengo na magari katika majimbo ya Illinois, Indiana na Kentucky.
Watu wapatao watano wameuawa katika kimbunga hicho na inahofiwa kuwa mamia ya watu huenda wamejeruhiwa katika kimbunga hicho kikali.
Idadi kubwa ya watu wanasemekana kunasa katika majengo.
Wataalam wa hali ya hewa wanasema kimbunga hicho kitaathiri watu milioni 53 katika maeneo hayo.

WATU 50 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA NDEGE URUSI

 
Gari ya kubebea wagonjwa ikitoa huduma uwanja wa ndege
Ndege ya abiria imeanguka katika uwanja wa ndege katika mji wa Kazan, nchini Urusi na kuua watu wote 50 waliokuwa katika ndege hiyo.Ndege hiyo aina ya Boeing 737 iliruka kutoka mji wa Moscow na ilikuwa ikijaribu kutua lakini ikawaka moto saa moja usiku kwa saa za huko.
Wizara ya matukio ya dharura imesema kulikuwa na abiria 44 na wafanyakazi sita wa ndege hiyo ya shirika la Tatarstan Airlines.
Wachunguzi wanajaribu kuona kama kulikuwa na makosa ya kiufundi au huenda ya kibinadamu yaliyosababisha ajali hiyo.
Afisa wa kamati ya uchunguzi Vladimir Markin ameiambia Televisheni moja nchini Urusi, Rossiya 24 TV, kwamba wataalam wanachunguza kubaini kama ajali hiyo imesababishwa na matumizi ya mafuta mabaya, au hali mbaya ya hewa.
Mvua ilikuwa ikinyesha katika mji wa Kazan wakati ndege hiyo ilipoanguka.
Kwa mujibu wa orodha rasmi ya wasafiri wa ndege hiyo, miongoni mwa waliokufa ni Irek Minnikhanov, mtoto wa kiume wa rais wa Jamhuri ya Tatarstan,nchini Urusi.
Aleksander Antonov, ambaye aliongoza Idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi, ni miongoni mwa abairia wa ndege iliyoanguka.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza, imethibitisha kuwa raia mmoja wa Uingereza amekufa katika ajali hiyo.
Miongoni mwa waliokufa wamo watoto wawili.
Rais Vladimir Putin wa Urusi ametuma salaama zake za rambirambi kwa ndugu na jamaa wa waathirika.
Tume ya serikali imeundwa kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.
Taarifa zinasema, rubani wa ndege hiyo Rustem Salikhov mwenye umri wa miaka 47, alijaribu mara kadhaa kutua kabla ya kuanguka kwa ndege hiyo.
Shirika la habari la Urusi limeripoti kuwa wafanyakazi walisema hawakuwa tayari kutua kwa sababu ya matatizo ya kiufundi.
Mwandishi mmoja wa habari ambaye alisafiria ndege hiyo mapema Jumapili kabla ya safari iliyotokea ajali, kutoka Kazan kwenda Moscow ameiambia televisheni moja nchini Urusi kwamba kulikuwa na mtetemo mkubwa wakati ndege hiyo ikitua mjini Moscow.
"Tulipokuwa tukitua haikujulikana kama kulikuwa na upepo mkali, japokuwa mjini Moscow, hali ya hewa ilikuwa nzuri au kulikuwa na tatizo la kiufundi au ndege yenyewe," amesema Lenara Kashafutdinova.
"Tulisukwasukwa huku na kule, ndege ilitua. Mtu aliyekuwa amekaa karibu nami alikuwa mweupe kama shuka kutokana woga uliompata."
Ndege hiyo imekuwa ikitoa huduma tangu mwaka 1990.
Uwanja wa ndege wa Kazan - mji mkuu wa Tatarstan - umefungwa tangu kutokea jali hiyo na hautarajiwi kufunguliwa hadi Jumatatu mchana.
Mji wa Kazan upo kilomita 720 mashariki mwa Moscow.