Jumanne, 10 Desemba 2013

HAYATI MANDELA AFANYIWA IBADA MAALUM

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210130349_7_mandela_memorial_getty.jpg 
Melfu ya watu nchini Afrika Kusini walijiunga na zaidi ya viongozi 90 wa dunia kwa ibada maalu ya hayati Nelson Mandela.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210130340_2_mandela_memorial_getty.jpg
Ibada hiyo ilifanyika katika uwanja wa michezo wa FNB mjini Johannesburg
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210130338_1_mandela_memorial_afp.jpg
Rais wa Marekani Barack Obama alisema kuwa Mandela ameifunza dunia umuhimu wa kutenda badala ya kusema sana pamoja na umuhimu kwa kuwa na mawazo mazuri ingawa ya kutenda. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210132221_17_mandela_memorial_reuters.jpg
Alipoondoka ukumbini, Rais Obama aliamkuana na Rais wa Cuba, Raul Castro ishara kubwa sana kati ya marais wa nchi hizo mbili ambazo zimekuwa zikizozana kwa zaidi ya nusu karne
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210130425_11_mandela_memorial_reuters.jpg
Mandela alifariki Alhamisi iliyopita, akiwa na umri wa miaka 95. Nchi hiyo imeandaa shughuli mbali mbali za kumuenzi Mandela kabla ya kuzikwa Jumapili.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210092246_mandela_memorial_reuters_9.jpg
Aliyekuwa anaendesha hafla hiyo Cyril Ramaphosa alisema kuwa safari ndefu ya Mandela imekamilika na sasa anaweza kupumzika
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210130351_8_mandela_memorial_ap.jpg
Askofu mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu,mmoja wa waliopigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, alisema Mandela alikuwa mtu wa kupatanisha watu pindi alipoondoka gerezani. 'Tumepata afueni kuwa matatizo yake ya kiafya yamekwisha' alisema Tutu
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210130431_14_mandela_memorial_getty.jpg
Ibada hii ilikuwa moja ya mkusanyiko mkubwa wa viongozi wa dunia kushuhudiwa hivi karibuni. Katika hotuba yake , katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban ki Moon, alisema kuna huzuni tele kwa umma kumpoteza Mandela
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210132219_16_mandela_memorial_reuters.jpg
Kulikuwa na hofu kuwa watu wangeamrishwa kurejea nyumbani , lakini mvua kubwa ilisababisha sehemu za uwanja kuwa bila watu
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210130344_4_mandela_memorial_ap.jpg
Mjane wa Mandela Graca Machel, alishangiliwa sana alipoonyeshwa kwenye skirini kubwa akiingia uwanjani
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210130433_15_mandela_memorial_getty.jpg
Pia kulikuwa na shangwe na vigelegele huku watu wakiimba Winnie Winnie Madikizela Mandela aliyekuwa mkewe Mandela. Alimpa pambaja na kumbusu Graca
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210132223_18_mandela_memorial_reuters.jpg
Hata hivyo Rais Jacob Zuma alizomewa mara kwa mara ilipokuwa zamu yake kuhutubia wananchi. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210130347_6_mandela_memorial_afp.jpg
Tangu kifo cha Mandela mji wa Johannesburg umekuwa ukishuhudia mvua lakini hiyo haikuwakatiza tamaa wananchi waliofurika uwanja wa michezo wa FNB 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210092248_mandela_memorial_getty_10.jpg
Umati wa watu uliimba na kucheza kama ishara ya kuenzi maisha ya Mandela 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210130355_10_mandela_memorial_ap.jpg
Ambao hawakuweza kufika uwanjani waliiona ibada hiyo kwenye televisheini zao nyumbani kote nchini Afrika Kusini 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/10/131210130345_5_mandela_memorial_ap.jpg
Mandela atazikwa siku ya Jumapili tarehe 15
Katibu mkuu wa UN, Ban Ki Moon , Rais Barack Obama na Jacob Zuma

Zaidi ya maraisa tisini wameungana na wananchi wa Afrika Kusini katika misa ya wafu ya Nelson Mandela na kusimulia kumbukumbu zao kwa Shujaa huyo wa Afrika.
Akiongea kwenye mkusanyiko huo mjini Soweto, Rais wa Marekani Barack Obama alimtaja Mandela kuwa shujaa na mkombozi wa Afrika na shujaa shupavu kuwahi kuonekana katika karne ya ishirini.
Alisema maisha ya Mandela lazima yawe mfano mzuri kwa dunia nzima hasa vita alivyopigania kuhakikisha utu wa watu unaheshimiwa.
Jamaa za Mandela wamemtaja baba yao Mandela kama mtu aliyetaka watu kuwa sawa.
Mmoja wa wajukuu wa Mandela alikariri shahiri la kusisitiza mshikimano wa watu. Obama alishangiliwa ingawa Rais Jacob Zuma anayehutubia wananchi alizomewa mara kwa mara.
Uwanja ambako misa hiyo inafanyika, haukujaa watu kutokana na mvbua kubwa iliyonyesha.
Maelfu ya watu wamehudhuria misa hiyo katika uwanja wa FNB.
Afrika Kusini imeandaa shughuli mbali mbali za kumuenzi Mandela kabla ya siku ya kuzikwa kwake nchini Afrika Kusini siku ya Jumapili.
Misa ya leo ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya viongozi wa kimataifa iliyoshuhudiwa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.
Viongozi wengine Watakaohudhuria misa ya wafu ya Mandela:
Watu wengi walikaidi hali mbaya ya hewa ambapo mvua kubwa imenyesha huku wakikusanyika uwanjani humo wakisubiri kwa muda mrefu kabla ya misa hiyo kuanza muda mfupi uliopita.
Waliohudhuria misa hiyo wamesemekana kuwa wenye furaha wakiimba nyimbo na kutaja jina la Mandela kwa shangwe unaweza kudhani ni mkutano wa kisiasa.
Misa hiyo itafanyika katika uwanja ambako Nelson Mandela alionekana kwa mara ya mwisho hadharani.
Misa hiyo itaonyeshwa kwenye skrini kubwa nje ya uwanja ili kuzuia msongamano wa watu.
Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na kwa wengi yeye ni shujaa na mkombozi wa Afrika Kusini.