Kwa mara ya kwanza kabisa tangu Kenya kujipatia uhuru, idadi ya wanawake imeongezeka kwa kiwango kikubwa katika bunge.
Katiba mpya inapiga marufuku ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya wanawake.
Hivi nafasi ya wanawake ya kuongoza, kumiliki mali na kuendeleza jamii
katika njia ya kipekee, inalindwa katika katiba.
Kwa mara ya kwanza kwa miaka hamsini ya kuwa jamhuri, Kenya imewapa
wanawake uongozi katika wizara kuu kama vile wizara ya mambo ya kigeni
na wizara ya ulinzi.
Taasisi kama mahakama ya juu na tume ya umma pia zinafuata katiba katika kuwapa wanawake nafasi za kipekee.
Mjadala huu ulijadili iwapo sera hizi zimefanikiwa katika mfumo wa serikali za ugatuzi.
Wanawake walio uongozini walielezea changamoto wanayoyapata kazini na kujibu maswali kuhusiana na mchango wao.
Joan Birika, Bobby Mkangi, Emma Mburu na Priscilla Nyokabi walikuwa
kwenye jopo. Edwin Saka ni mojawapo wa wageni maalum walioalikwa.
Msimulizi ni Joseph Warungu.
Katiba
mpya ya Kenya inatilia maanani usawa wa wanawake katika vitengo tofauti
ya maisha. Mjadala huu ulimulika mchango wa wanawake viongozi na
kuchambua jinsi sera za katiba mpya zinafanikiwa kuendeleza usawa wa
kijinsia.