Vikosi vya usalama nchini Misri,
vimekabiliana na wapiganaji wa kiisilamu baada kuingia katika mji
ulioko viungani vya mji mkuu Cairo wa Kerdasah.
Duru zinasema kuwa wanajeshi hao waliingia mjini
humo ambako polisi 11 waliuawa mwezi jana kukabiliana na kile
walichokiita magaidi.Mauaji hayo yalitokea wakati aliyekuwa rais Mohammed Morsi alipoondolewa mamlakani na jeshi.