Angalau watu wawili wameuawa katika ghasia kati ya polisi na waandamanaji katika mji mkuu wa Ukraine Kiev.
Makabiliano hayo ya Jumatano, yalianza baada ya polisi kuanza kuvunja maandamano ya moja ya makundi ya wanaharati
Viongozi wa mashitaka walithibitisha kuwa watu wawili walifariki
kutokana na majeraha ya risasi. Ni watu wa kwanza kufariki kutokana na
vurugu tangu kuanza Novemba mwaka jana kutokana na mapendekezo ya
serikali kujiunga na muungano wa Ulaya
Makabiliano hayo yanakuja baada ya siku moja ya kubuniwa sheria mpya za
kuharamisha maandamano wiki jana. Bunge liliidhinisha sheria hizo wiki
jana na kusababisha vurugu mpya
Mamia ya watu wamejeruhiwa ingawa baadhi ya vurugu zimelaumiwa kwa kundi moja linalounga siasa kali
Ghasia za Jumatano, zilianzia katika sehemu ndogo ya barabara kuelekea katika majengo ya bunge .
Muda mfupi baada ya saa mbili asubuhi, baada ya usiku wa amani, polisi
walivamia sehemu ambako waandamanaji hao walikuwa wamekita kambi
Polisi baadaye walichukua hatua zao, baada ya makabiliano makali na waandamanaji lakini ilipofika mchana na kuvunja vuzuizi
Waandamanaji walianza, kuwatupia mabomu ya petroli na mawe wakati polisi
wa kupambana na ghasia nao waliwatupia magurunedi na risasi za mipira
Moshi mweusi ulifuka kutokana na magurudumu kuteketezwa wakati wa vurugu
hizo mjini Kiev, huku picha za magari ya kivita yakitumiwa kupambana na
waandamanaji hao.