Ijumaa, 6 Septemba 2013

FASTJET YAJA KWA NGUVU MPYA


Kampuni ya Ndege ya FastJet kutaoa huduma za usafirri wa Ndege kwa bei nafuu

Kama umeshafanya maandalizi ya safari yako kati ya Dar es Salaam na Johannesburg tarehe 27 mwezi Septemba, tuambie kwanini ungependa kwenda Afrika ya Kusini, kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Nauli zinaanzia Tsh 160,000 (Bila gharama ya kodi), Safari zitaanza tarehe 27 Septemba, na itapaa mara tatu kwa wiki. Tembelea www.fastjet.com ili kufanya maandalizi ya safari yako sasa.


Safari zingine ambazo inatarajia kuzitoa ni Dar Es Salaam-Mbeya kwa Tshs 32,000/= na Dar Es Salaam-Kilimanjaro kwa Tshs 32,000/=

WACHIMBA MIGODI AFRIKA KUSINI WAREJEA KAZINI

Wachimba migodi wanaounga mkono chama cha wafanyakazi nchini Afrika Kusini

Wengi wa wachimba migodi wa dhahabu ambao wamekuwa wakigoma tangu Jumanne nchini Afrika Kusini wamerejea kazini baada ya waajiri wao kukubali kuwapa nyongeza ya mishahara.
Kwa mujibu wa maafisa wa chama cha kitaifa cha wafanyakazi, kampuni nne kati ya saba zimekubali kuwapa nyongeza wafanyakazi hao ambayo inaaminika kuwa asilimia 8.

Chama hicho kilikuwa kinataka 60%, wakati waajiri wao wakipendekeza kuwapa asilimia sita ikiwa sawa na kiwango cha mfumuko wa bei nchini humo.
Wachimba migodi walikuwa wametishia kuwa mgomo wa muda mrefu ungesababisha migodi kufungwa na maelfu ya watu kupoteza kazi zao, kufuatia kushuka kwa bei ya dhahabu.

Wanasema kuwa bei ya kuzalisha madini hayo imepanda kwani wamelazimika kuchimba mita nyingi chini ya ardhi kupata madini hayo.
Kwa miaka mingi Afrika Kusini ilikuwa nchi yenye kuzalisha dhahabu nyingi kuliko nchi yoyote duniani uikiwa ni asilimia 68 mapema miaka ya sabini lakini mambo yamebedilika sasa ikiwa inazalisha tu asilimia sita ya dhahabu yote duniani, hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la AFP

Chama cha wafanyakazi NUM kinawakilisha takriban asilimia 64 ya wachimbaji wa dhahabu kote nchini humo.
Mwaka jana wananchi wengi waliachwa vinywa wazi wakati polisi walipowaua wafanyakazi 34 wa migodi ya platinum wakati wa mgomo haramu ulioitishwa na chama hasimu cha wafanyakazi.

TAZARA MBEYA SACCOS YATOA MIKOPO YA PIKIPIKI (BODABODA) MKOA WA MBEYA

Hayawi hayawi sasa yamekuwa-ndoto zatimia

Madereva wakiwa na furaha isiyo kifani baada ya kupata pikipiki

Meneja wa TAZARA MBEYA SACCOS Ndg Philemon Kaduma (kulia) na Mjumbe wa Bodi ya Chama Ndg Dennis Ngaraguza (kushoto) wakikabidhi pikipiki kwa madereva.

Meneja wa TAZARA MBEYA SACCOS Ndg Philemon Kaduma (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya Chama Ndg Dennis Ngaraguza (kulia) wakitoa maelezo jinsi watakavyo nufaika na mikopo hiyo ya pikipiki

 Mjumbe wa Bodi ya Chama cha TAZARA MBEYA SACCOS Ndg Dennis Ngaraguza akiwapongeza wajasiriamali hao na jinsi ya kuzitumia pikipiki hizo  ili ziweze kuwanufaisha na kuinua maisha yao.

Ofisi za TAZARA MBEYA SACCOS LTD zilizopo Iyunga-Mbeya kandokando mwa barabara ya Tunduma-Mbeya
 

HAYA NDIYO YALIYOTOKEA BUNGENI JANA







Baada ya kuibuka mvutano mkali bungeni jana, kati ya Naibu Spika, Job Ndugai na wabunge wa Kambi ya Upinzani, wasomi, wanaharakati, Chama cha Madaktari Tanzania (Mat), Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), vimesema kinachoendelea sasa ndani ya Bunge ni masilahi ya vyama vya siasa siyo taifa.

Walitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuwataka askari kumtoa nje ya Ukumbi wa Bunge, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Mbowe aligoma kukaa chini na kuungwa mkono na wabunge wa upinzani, akishinikiza kuahirishwa kujadiliwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, hadi hapo Zanzibar itakaposhirikishwa, muda mfupi baada ya wabunge kupiga kura na 156 kutaka ujadiliwe na 56 wakitaka uondolewe.

Wabunge hao wa upinzani kutoka vyama vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi, juzi walitoka nje ya Ukumbi wa Bunge wakishinikiza kuahirishwa kujadiliwa kwa muswada huo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally alisema mvutano huo umejaa masilahi ya wanasiasa kwa kila upande kujaribu kuvutia kwake.

“Mvutano ule hauzungumzi kabisa mwafaka wa Bunge la Katiba, binafsi nadhani Bunge la Katiba linatakiwa kuwa na wabunge wapya kabisa na wasiotoka katika chama chochote cha siasa,” alisema
Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya alisema: “Marekebisho hayo yanafanyika kwa ajili ya mustakabali wa Muungano wetu, kama Zanzibar hawakushirikishwa, uwekwe utaratibu wa jambo hilo kufanyika ili kipatikane kitu bora, siyo bora Katiba.”

Alisema nchi zilizoendelea zimepata mafanikio kwa kuwa zina Katiba nzuri ambazo zinaweza kudumu kwa miaka 100 kabla ya kufanyiwa marekebisho..