Jumanne, 17 Desemba 2013

MANGARIBA 38 WAKAMATWA HUKO MOSHI MKOANI KILIMANJARO

 
Ukeketaji hufanywa katika sehemu nyingi Tanzania licha ya kuharamishwa
Maafisa wakuu mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wamewakamata wanawake 38 waliopatikana wakiwakeketa wasichana katika eneo hilo.
Haijulikani idadi ya wasichana waliokuwa wanakeketwa , lakini ripoti zinasema kuwa walikuwa kati ya umri wa miaka 3 na 16.
Ingawa ukeketaji ambao umeharamishwa huendelezwa katika sehemu nyingi za Mara na Dodoma nchini hapa nchini , hilo sio jambo la kawaida mjini Moshi.
Inaarifiwa wanawake hao walikamatwa Jumapili walipokuwa wanacheza dansi ya kitamaduni wakiwazingira wasichana ambao ndio walikuwa wamekeketwa tu.
Baadhi ya wasichana inaarifiwa bado walikuwa wanavuja damu na wengine wakiwa wanauguza majeraha.
Ukeketaji umeharamishwa hapa nchini tangu mwaka 1998 ingawa bado unaendelezwa katika baadhi ya sehemu mabalimbali za nchi.
Inakisiwa asilimia 15 ya wasichana pamoja na wanawake wamekeketwa hapa nchini.

WAJUE VIONGOZI WANAWAKE WANAOTIFUA KIVUMBI DUNIANI

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/16/131216115939_michelle_bachelet_976x549_afp.jpg 
Michelle Bachelet amechaguliwa kama Rais wa Chile kwa muhula wa pili na kumshinda mpinzani wake Evelyn Matthei kwa kura nyingi
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/12/131212132037_1_joyce_banda.jpg
Joyce Banda alichaguliwa kama Rais wa kwanza mwanamke Kusini mwa Afrika April 2012. Akawa rais wa Malawi alipomrithi mtangulizi wake aliyefariki kutokana na mshtuko wa moyo
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/12/131212132039_2_ellen_johnson_sirleaf.jpg
Rais wa Liberia,Ellen Johnson Sirleaf, 72, alitajwa kama mmoja wa washindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2011. Alichaguliwa kama Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika mwaka 2005 miaka miwili baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 14 Liberia
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/12/131212132041_3_sheikh_hasina.jpg
Sheikh Hasina alichaguliwa kwma waziri mkuu wa kwanza wa Bangladesh kwa muhula wa pili mwezi Januari mwaka 2009. Lakini mwaka 2008 chama chake cha Awami, kilipata ushindi mkubwa dhidi ya mpinzani wake Begum Khaleda Zia.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/12/131212132043_4_park_geun-hye.jpg
Korea Kusini imemchagua rais wake wa kwanza mwanamke Park Geun-hye, kwenye uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali Disemba mwaka 2012. Babake Park Chung-hee alitawala nchi hiyo kwa miaka 18
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/12/131212132044_5_yingluck_shinawatra.jpg
Waziri mkuu wa Thailand, ingluck Shinawatra dadake mdogo waziri mkuu aliyeondolewa mamlakani Thaksin Shinawatra, aliongoza chama chake cha upinzani kuweza kushinda uchaguzi uliofanyika Julai 2011.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/12/131212132046_6_helle_thorning-schmidt.jpg
Helle Thorning-Schmid alichaguliwa kama waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa Denmark, baada ya chama chake kupata ushindi kwenye uchaguzi uliofanyika Septemba mwaka 2011. Thorming alikosolewa hivi karibuni kwa kujipiga picha na waziri mkuu wa Uingereza Cameron na Rais Barack Obama kwenye ibada maalum ya hayati Mandela
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/12/131212132048_7_dalia_grybauskaite.jpg
Dalia Grybauskaite alichaguliwa kama rais wa kwanza wa Lithuania katika uchaguzi mkuu wa Mei 2009. Alishinda kwa kura 69%
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/12/131212132050_8_angela_merkel.jpg
Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel anajulikana kama kiongozi asiyekuwa na mbwe mbwe nyingi na kusababisha watu kumuita..Mutti..mama wa taifa. Markel anajiandaa kwa muhula wa tatu baada ya kushinda uchaguzi wa Septemba 22
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/12/131212132338_11_cristina_fernandez.jpg
Rais wa Argentina, Cristina Fernandez alishinda uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba mwaka 2007 ushindi ambao wengi walisema ulitokana na umaarufu wa mumewe aliyekuwa Rais Nestor Kirchner. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/16/131216100742_dilma.jpg
Rais wa Brazil Dilma Rousseff alichaguliwa kama rais wa kwanza mwanamke nchini Brazil alipochukua hatamu za uongozi kutoka kwa Luiz Inacio Lula da Silva mwaka 2011. Alikuwa mkuu wa majeshi kabla ya kuteuliwa na kumrithi Rais De Silva
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/12/131212132344_14_portia_simpson-miller.jpg
Kiongozi wa upinzani nchini Jamaica, Portia Simpson-Miller alishinda uchaguzi uliofanyika Disemba mwaka 2011 kwa idadi kubwa ya kura. Alikuwa waziri mkuu wa Jamaica kabla ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2007
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/12/12/131212132346_15_kamla_persad-bissessar.jpg
Kamla Persad-Bissessar alichaguliwa kama waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa Trinidad and Tobago, wakati chama chake kilishinda uchaguzi kwa idadi kubwa ya kura mwezi Mei mwaka 2010
Wananchi nchini Chile wamemchagua Michelle Bachelet kama rais wao kwa muhula wa pili.
Wananchi wa Chile wameendeleza kasi ya kuwachagua viongozi wanawake mtindo ambao unaendelea kukuwa katika mataifa ya kilatino.
Na hawa hapa ni baadhi ya wanawake ambao wako mamlakani duniani.